Askari wa dolia wa Hifadhi ya Serengeti wakamata kiongozi wa jeshi la polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari wa dolia wa Hifadhi ya Serengeti wakamata kiongozi wa jeshi la polisi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KIBURUDISHO, Mar 23, 2012.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Ni habari niliyoipata toka kwa mdau wangu anayepatikana huko kuwa askari waliokuwa doria wamemkamata Afisa usalama wa taifammoja, OCD akiwa na vijana wake saba ila wanne walifanikiwa kutoroka wakiwa wamekwenda kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na sheria.
   
 2. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Siku nyingne tutamkamata waziri wa nishati akichimba madin kinyume cha sheria.
   
 3. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,535
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  wamezidiana maslai...itakua huyo afande amekaa muda mrefu bila kotoa ten%
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Siyo Zuberi wa hapa A town kweli?

  Natamani sana angekuwa yeye!

  KIBURUDISHO,ni OCD wa mkoa upi?

  Ofisa wa usalama wa taifa!
  Mmmmhh! Kuna kazi kweli kweli!
   
 5. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Ndio mambo ya Chukua Chako Mapema?
   
 6. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,291
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  bora hao wayachimbe ni watanzania, kuliko wazungu wanaojichukulia madini dezooo!!!
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Kamanda! Hili la huyu fisadi polisi imekuwaje tena?
   
 8. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Wawaachie wachimbi kisha watuletee vyandarua !
   
 9. V

  Visionmark Senior Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua ni nini, KIBURUDISHO? kuna bwana mmoja alishawahi kuniambia kuwa maeneo mengi nchini mwetu ambayo yametengwa kama hifadhi au mbuga za wanyama yana madini mengi sana na hasa hifadhi ya Seregeti. Ndani ya hifadhi ya Seregeti kuna pahala madini ni mengi sana, Vigogo wanajua hili na huwa wanaenda kwa siri kuchukua hayo madini wakishirikiana na hawa wanaowaita "Wawekezaji" na sehemu hiyo ina ulinzi mkali sana!
   
 10. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh; mtoa mada hebu weka bayana tusaidiane kuwajuza watanzania ukweli wa jambo hili anaweza patikana mdau mwingine mwenye ujazo wa ziada akatukamilishia hii taarifa; tukio hilo limetokea ktk hifadhi gani na ni lin?
   
 11. i

  issenye JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Maofisa polisi mbaroni kwa kuchimba madini Serengeti [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 24 March 2012 12:35 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Anthony Mayunga, Serengeti
  MAOFISA waaandamizi wa Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na watu wengine watano wamekamatwa wakichimba dhahabu katika eneo Kilimafedha ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti (Senepa).

  Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), zinasema watu hao walikamatwa wakiwa na sururu, koleo, nyundo, viroba 10 vipya na kifaa cha kupimia dhahabu.

  Tukio hilo limetokea Machi 23, asubuhi na maofisa hao walikamatwa wakiwa na gari la polisi.

  Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi alithibitisha kukamatwa kwa maofisa hao (majina tunayo) na kufafanua kuwa watu hao wanahojiwa na mamlaka husika ili kukamilisha taratibu.
  “Nimepata taarifa kutoka kwa mhifadhi wa Senapa, nilikuwa safarini, wameniambia kuwa wanaendelea kuwahoji. Kwa ujumla hatutaliachia suala hilo, mamlaka zilizotakiwa kulinda maliasili ndizo zihusike kuhujumu! Wakibainika kuhusika lazima sheria ichukue mkondo wake,”alisema na kuongeza:

  “Kama watakuwa wamehusika kuchimba madini ndani ya hifadhi hawashindwi kuungana na majangili kuua wanyama kama tembo na wengineo. Kesho nitakuwa ofisini, nitafute nitakueleza zaidi maana sisi hatuna vyombo vya kisheria tutawapelekea wahusika kama itathibitika.”

  Habari zaidi zinaeleza kuwa hadi jana jioni maofisa hao walikuwa bado wakihojiwa katika ofisi ya Mhifadhi Mkuu wa Seronera.

  Imeelezwa kwamba maofisa hao waandamizi wa usalama waliondoka mjini Mugumu wakiwa na vijana wanaodaiwa kuwatumia kwa kazi hiyo na kupitia katika Lango la Fort Ikoma
  wakiwa na gari hilo likiwa limefungwa turubai na ndani wakiwemo watu watano ambao hawakukaguliwa kama utaratibu unavyoagiza.

  “Wamefika hapa getini saa 12 asubuhi wakiwa wamefunga turubai wakidai wako watatu dereva na kuwa wanakwenda kikazi Serena lodge, hatukuwakagua kwa kuwa maofisa wanafahamika, tuliwaamini,” alisema mmoja wa watu waliokuwa kwenye lango hilo.

  Alisema baada ya maofisa hao kupita walitoa taarifa sehemu mbalimbali za uongozi wakidhani kuwa kulikuwa na ugeni unaotembelea hifadhini humo.

  “Maofisa walipokataa kuwa hakuna mgeni ndani ya hifadhi ilibidi askari wa doria kuanza kufuatilia maeneo yote ikiwamo eneo la Kilimafedha ambako wanyama kama Faru huhifadhiwa, ndipo walipowakuta vijana wakichimba huku maofisa hao waliokamatwa wakiangalia,” alisema mtoa habari huyo.

  Ilidaiwa kuwa ofisa mwandamizi wa polisi wilaya aliyekamatwa alikutwa akiwa na bastola na alipohojiwa alidai kuwa walikuwa wanafuatilia watu wanaodaiwa kuingia na bunduki eneo la hifadhi.

  Baadhi ya askari wa hifadhi hiyo wamedai kuwa mtandao wa watu hao ni mkubwa ukihusisha pia baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali ambao ndiyo wanunuzi na wafadhili wa matukio hayo yakiwemo ya ujangili wa meno ya tembo.

  Walisema sababu za kusaka bunduki bila mhifadhi wala askari wengine kuwepo hazikuwa na maana kwa watu hao ambao awali, walieleza kuwa wanakwenda eneo la Seronera tofauti na walipokamatiwa.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema hajapata taarifa za tukio hilo kwa kuwa alikuwa kwenye kikao.

  Kwa upende wake, Mhifadhi wa Senapa,
  Mtango Mtahiko hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akisema alikuwa hajapata taarifa kamili.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 12. i

  issenye JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Maofisa polisi mbaroni kwa kuchimba madini Serengeti [/TD]

Loading...