Serikali iunde tume kuchunguza tuhuma za mauaji yanayodaiwa kufanywa na askari wa hifadhi ya pori tengefu la Selous. Hali ni mbaya

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,644
35,972
Selous hifadhi ya pori tengefu au pori la akiba kwasasa ndilo pori linalotegemewa sana na TAWA.

Kama kawaida ya binadamu hakosi alternative pale anapozidiwa njaa au shida.

Vijana wanaingia kwenye hifadhi mbalimbali kutafuta chochote kitu ili wapate kujinasua aidha kwenye njaa au wajinasue kwenye ufukara.

Sasa vijana wanaoshikwa huko Selous lango la Liwale wanauwawa kama paka mwitu tu.

Nisiandike sana haya ila kama serikali hii inapenda haki basi ikachunguze suala hili. Waende wilaya ya Liwale wapo vijana ambao walishuhudia wenzao wakikatwa miguu porini, kupigwa risasi na mateso mengine.

Ni unyama sana. Ukifika wilaya ya Liwale hata mtoto mdogo anajua kuwa askari wa hifadhi ya Selous wameua wananchi. Serikali hii kama itapuuzia haki, nasema katika Roho, haitasimama.

Nilisema wakati wa serikali ya Magufuli na ninasema wakati huu. Serikali hii ikipuuzia haki haitasimama. Itaanguka soon.

Sibariki vitendo vya kijangiri, kukata miti au kuchimba madini kwenye hifadhi ila mtu akivunja sheria Askari sio hakimu.
 
Selous hifadhi ya pori tengefu au pori la akiba kwasasa ndilo pori linalotegemewa sana na TAWA .
Kama kawaida ya binadamu hakosi alternative pale anapozidiwa njaa au shida.
Vijana wanaingia kwenye hifadhi mbalimbali kutafuta chochote kitu ili wapate kujinasua aidha kwenye njaa au wajinasue kwenye ufukara.
Sasa vijana wanaoshikwa huko Selous lango la Liwale wanauwawa kama paka mwitu tu.
Nisiandike sana haya ila kama serikali hii inapenda haki basi ikachunguze suala hili. Waende wilaya ya Liwale wapo vijana ambao walishuhudia wenzao wakikatwa miguu porini, kupigwa risasi na mateso mengine.
Ni unyama sana.
Niko tayari kutoa code muhimu za watu ambao wataifanikisha hiyo time.
Serikali hii kama irapuuzia haki, nasema katika Roho, haitasimama.
Nilisema wakati wa serikali ya Magufuli na ninasema wakati huu. Serikali hii ikipuuzia haki haitasimama. Itaanguka soon.
Sibariki vitendo vya kijangiri, kukata miti au kuchimbo madini kwenye hifadhi ila mtu akivunja sheria Askari sio hakimu.
Hata kama wa.ekosea kiasi gani sheria zetu za taifa haziruhusu kuua na kutesa.Wakamatwe wapelekwe mahakamani ili na wengine wajifunze. Sasa kumkata mguu mmoja tena mafichoni sio suluhu pia ni kinyume cha haki za binadamu.

Mwingine kapita hapo kutafuta kuni tu.
 
Unakiri ni majangili na ushahidi upo sasa jibu la jeuri yao iweje? Hao wakatwe miguu na mikono kbsa
Wewe makosa unayofanya maaskari wangekuua ingekuwa sawa?
Umekosa mara ngapi. Tena kama haitoshi si ajabu unaishi kwa kufanya vidili haramu.
Baba yako una hakika chakula chote alicholeta nyumbani kulikuwa cha halali?
Wangemuua
 
Utawala wa Sheria - hakuna aliye mkubwa mbele ya sheria. Mahakama ndio chombo pekee cha haki na utoaji maamuzi ya migogoro ya kisheria. Pelekeni watuhumiwa mahakamani na sio kumalizana nao maporini.
 
Nimekuja kugundua hawa askari wa kulinda wanyama pori wanaogopwa sana huko kwenye maeneo yao, inaaminika kwenye hizo jamii zilizozunguka hifadhi, hao askari wana haki ya kumuua yeyote watakayemkamata amekiuka sheria za maeneo hayo, hii haki sijui wameipata wapi.
 
Wewe ni binadam kweli yaan mtu anaenda kuwinda swala ili apate kitowewo akikamatwa adhabu iwe kukatwa miguu au mikono kweliii kwa nini asipewe adhabu ambazo ni fair

...hivi kweli sisi binadamu tunaakili sawasawa jaman.
Huyu mchangiaji kakosa malezi bora
Akili imeharibika
 
Wewe ni binadam kweli yaan mtu anaenda kuwinda swala ili apate kitowewo akikamatwa adhabu iwe kukatwa miguu au mikono kweliii kwa nini asipewe adhabu ambazo ni fair

...hivi kweli sisi binadamu tunaakili sawasawa jaman.
Mnachekesha hao watupwe mtoni waliwe na mamba wandenge, wamaku, wamwe, wamako wanajuana na mamba hio ndio mahakama inawafaa sana. Mnaakili kuvunja Sheria ila kupewa ruziku hamtaki,

Nida kumahwelu mkavune liwali mle na mamba
 
Wewe ni binadam kweli yaan mtu anaenda kuwinda swala ili apate kitowewo akikamatwa adhabu iwe kukatwa miguu au mikono kweliii kwa nini asipewe adhabu ambazo ni fair

...hivi kweli sisi binadamu tunaakili sawasawa jaman.
Hawa ndio waliopewa mamlaka za kushika mabunduki tazama fikra zao
 
Ni kweli hili lizungumziwi ,maaskari wanyamapori wanaua watu kadri wapendavyo wakimkuta uko kwenye hifadhi
 
Nimekuja kugundua hawa askari wa kulinda wanyama pori wanaogopwa sana huko kwenye maeneo yao, inaaminika kwenye hizo jamii zilizozunguka hifadhi, hao askari wana haki ya kumuua yeyote watakayemkamata amekiuka sheria za maeneo hayo, hii haki sijui wameipata wapi.

Wanasema nafuu jambazi kuliko jangili. ukikutana na jangili msituni sijui anaokota kuni, sijui anachuma matunda sijui anapembe za ndovu, yaani akiwa na silaha akikuona askari anaanza na wewe. Askari game anaua mtu kwa kujihami hasa pale anapotumia silaha ya moto
 
Nimekuja kugundua hawa askari wa kulinda wanyama pori wanaogopwa sana huko kwenye maeneo yao, inaaminika kwenye hizo jamii zilizozunguka hifadhi, hao askari wana haki ya kumuua yeyote watakayemkamata amekiuka sheria za maeneo hayo, hii haki sijui wameipata wapi.
haya kayataka makamu wa Rais aliwaambia wachukue hatua kali wavamizi! mburundi hana huruma
 
Unajua hayo unayoongea yanaweza kukutokea puani we mwenyewe kwa kuwa hili ni jukwaa la wazi watu wote wanakusoma?
Ujeuri na nyara za serikali hakunaga kamwe adhabu Kali zitolewe, mawazo yangu sio lazima yafanane na yako. Wana uhuru wa kufuata ushauri unaofaa na unaokubalika kisheria, maoni yangu si Sheria Kwa mamlaka husika. Hao hukumu inawafaa ya kifo kuua wanyama ni reciprocal Kwa hao majangili simple as that.
 
Back
Top Bottom