waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 190
- 451
Askari polisi katika mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wanadaiwa kuvamia mgodi wa Kitalu B, unaomolikiwa na mfanyabiashara, Joel Saitoti na kutembeza kichapo kwa wafanyakazi na kisha kuwapora madini zaidi ya kilo nne waliokuwa wamezalisha .
Akiongea kwa uchungu Meneja wa mgodi huo ,Martin Msigwa kutoka kampuni ya Gem and Rock Venture alisema kuwa askari polisi walivamia mgodi wao wakiwa na watu zaidi ya 30 na kuwashambulia kwa kipigo na kisha kuwapora madini kinyume cha sheria.
Alifafanua Kuwa sakata hilo ,lililotokea machi 13 mwaka huu,wakati wanaendelea na uzalishaji wa madini hayo ambapo askari hao wakiwa ameambatana na wachimbaji wengine waliwavamia na kuanza kuwapiga wafanyakazi wa kampuni hiyo wakilazimisha watoe madini waliokuwa wamezalisha zaidi ya kilo nne.
Alisema kabla ya askari hao kufika, alikuja mkaguzi wa baruti, Ezekiel Isaac ambaye alifanikiwa kuvunja geti la Mtobozano akipitia mgodi wa Franone Mining na kuingia kitalu B inayomilikiwa na kampuni ya Gem and rock bila kufuata taratibu .
"Baada ya kufika walikuta shughuli za uzalishaji zikiendelea na kutaka wapatiwe madini wakilazimisha yapitie mgodi wa Kitalu C,lakini vijana wetu waligoma kuachia madini hayo wakidai sio utaratibu wa kawaida kwakuwa mkaguzi wa baruti alikuwa mwenyewe alishirikiana na wafanyakazi wa Franone ,bila kuwepo askari polisi,jeshi la wananchi (JWTZ) na usalama wa taifa kama ilivyozoeleka"
Naye meneja msaidizi wa mgodi huo,Enock Nanyaro alidai kuwa kabla ya tukio hilo Machi 10 mwaka huu majira ya saa 10 jioni alipokea barua iliyotumwa kupitia mtandani wa WhatsApp kutoka kwa afisa mkaguzi wa baruti Ezekiel Isaac kwenda kwa meneja Nanyaro ikiitaka kampuni hiyo kusimamisha uzalishaji katika Kitalu B ili kupisha uchunguzi baada ya kuwepo malalamiko ya kuwepo kwa hewa chafu inayotokana na mlipuko wa baruti.
Nanyaro alisema kuwa uongozi wa mgodi huo uliamua kujibu barua hiyo kwa njia hiyo hiyo ya whatsup wakimweleza Mkaguzi huyo kuwa umbali waliopo ni zaidi ya mita 580 kutoka mgodi wa Franone kwa hiyo sio kweli kwamba moshi wa baruti unawafikia.
"Tunashangaa kuona kampuni ya Franone wakilalamika kuhusu moshi wa baruti wakati wapo umbali mkubwa na sisi kama ni hivyo kwanini migodi mingine ya jirani kama mgodi wa Deo Minja ,Sunday na Papaking hawalalamiki"???
Naye Wilbart Mosses mfanyakazi wa mgodi huo wa Gem and Rock Ventures amesikitishwa kuona mkuu wa usalama Mererani (DCO) kutoa amri kwa askari aliokuwa ameongozana nao kuanza kuwashambulia kwa kipigo kikali na kupokonywa madini yetu ambayo ndio ujira wetu na kuondoka nayo.
Mosses alimwomba rais Samia suluhu Hasan kuingilia kati sakata hilo ili kupata haki yao ya msingi kwani wamechoka kuonewa mara kwa mara pindi wanapoanza uzalishaji wa madini.
Endd...
Pichani mmoja ya mwanaapolo aliyeambulia kichapo cha polisi akionesha majeraha mgongoni
Wengine ni viongozi wa mgodi huo na baadhi ya wanaapolo waliopewa kichapoView attachment 2555395View attachment 2555398