Askari Polisi nao ni binadamu

Askari Polisi nao ni binadamu

naona mnahangaika kupindisha ukweli....ila watanzania wa leo sio wale wa zidumu fikra za mwenyekiti....kila mtu anajua nini kinaendelea....
 
Tatizo baadhi wanatumika vibaya,kisiasa,pia wanadhalilisha utu kwa kutendea ukatili watuhumiwa,mfano video matukio karibuni kukamata ,kupiga kwa fedheha wafuasi wa CDM.
 
kwanza wewe unaijua risasi au unadhani ni manati yanayotumia mawe
hakuna Raia anayeruhusiwa kumiliki Sub machine Gun, AK 47 NK
ni watu maalum tu ndio wanaruhusiwa na hawafyatui bila AMRI ya FIRE
Hoja hupingwa kwa hoja mkuu.
 
Suala hapa si nani kafyatua risasi. Suala ni roho mbaya kiasi gani kwa binadamu kufanya kitendo kinachosababisha mauti kwa mtu asiyekuwa na hatia. Hii roho ya kutaka kuua kwa jambo ambalo halina mashiko ni aibu au ni woga uliovuka mpaka. Kwa nini Watz tusijifunze kwa wenzetu wa kenya. Hivi ni watu wangapi wangeweza kupoteza maisha wakati jamaa akionyesha ukalulu wa kujiapisha kuwa rais kwenye jukwaa kama la kuendeshea mnada wa mitumba? Mungu ilaze roho ya mja wako Akwilina kwenye raha ya milele.
 
Habari za muda huu ndugu zanguni mabibi na mabwana(wakuu) humu ndani ya chama, poleni na mihangaiko ya hapa na pale katika kutafuta girisi(by mkulu voice) ili kutatua mkazo huu wa vyuma ambao unatuandama awamu hii.

Kwanza napenda kutoa pole(kama binadamu) kwa kuondokewa kwa bahati mbaya dada yetu(mwanafunzi) wa NIT kwani ni katika mazingira tatanishi sana Mungu aiweke roho yake mahali pema. Pasipo kupoteza muda ndugu zangu baada ya vuguvugu la siku chache zilizopita za uchaguzi na binti kupigwa risasi kuna mambo machache ya kuambizana na kujifikirisha hapa.

Sasa katika hili tatizo lililotokea ni kweli imetokea kiasi kwamba kuna baadhi ya raia wanadai walishuhudia wakati risasi inapenya katika mwili wa mwanafunzi ila tujiulize maswali haya;

1.Je, kuna uthibitisho gani kama askari ndiye aliefyatua risasi maana Kamanda Mambosasa amebainisha kuwa yawezekana ile risasi haikutoka mikononi mwa askari ila watu wasiojulikana ambapo ukiangalia kwa jicho la pili utaona Kamanda anaweza kuwa sahihi maana mashuhuda wote hawakuona kama ilitokea upande wa polisi kwani kulikuwa na vuguvugu na hivyo watu wabaya wakatumia nafasi hiyo.

2.Kama askari ndio waliofyatua risasi je matumizi ya silaha kwa askari yapoje? Kwanini wachunguzwe askari wa chini waliotumia silaha za moto katika hiyo ghasia wakati silaha zinaizinishwa na wakuu wa jeshi la polisi kabla ya kuzitumia(huwaruhusu kutumia) na kuachishwa waachishwe waliotumia?

Ndugu zangu tujaribu kuangalia kiubinadamu haya maswali mawili kuhusiana na haya matukio, yaani uhakika wa aliyepiga risasi na hukumu kwa askari waliotenda ilhali ruhusa ya matumizi ya silaha hutoka juu ambapo wawajibishwaji wangeanzwa na maafisa wa jeshi kwanza.

Niko tayari kukosolewa kwa huu waraka mfupi kuhusiana tukio lililotokea siku chache zilizopita.

[HASHTAG]#Africanar[/HASHTAG]
Huna tofauti na shetani falauni wewe
 
huijui hiyo silaha wala uzito wake ukidhani ni manati, utatembea nayo AK47 Kinondoni Mkwajuni begani au mfuko wa suruali? tena saa 11 jioni ndani ya maandamano. Hebu msitetee ujinga wa buk 7 hao ni POLISI hao 6 tu
kwahyo unasapot ama vp mkuu
 
N video ngap zinathibitisha vitendo vya rushwa n wangap mtaanii wapo jela kwa kesi ambazo sio zao eeeh mbn unajitoa ufahamu mkuu
si askari wote hata hvyo siyo sheria ya jeshi kupakazia kesi ni baadhi yaa askari watovu wa nidham tuu
 
Back
Top Bottom