Askari Polisi akamatwa na noti bandia zenye thamani ya Sh. 870,000

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,256
16,306
Askari Polisi Ezekiel Dinoso (32) mkazi wa tarafa ya Mgeta, wilayani Mvomero mkoani Morogoro amekutwa na noti bandia za Sh 10,000 zenye thamani ya Sh 870,000, akijiandaa kuzitumbukiza katika akaunti ya mtandao wa Tigo Pesa katika duka mojawapo eneo la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema jana kuwa tukio hilo ni la Mei 14, mwaka huu saa 1:00 usiku katika eneo la Mawezi , Manispaa ya Morogoro.

Mtuhumiwa alikutwa katika duka la Hadija Hamis (35) mkazi wa Chamwino, wakati alipohitaji kuwekewa fedha hizo, mwenye duka alimtilia shaka hivyo kuarifu Polisi.

Mtuhumiwa alipokamatwa na askari baada ya kutolewa taarifa Kituo cha Polisi, alikutwa akiwa na noti bandia 87 za Sh 10,000.

Alitaja namba za noti hizo ni BX 7287490 zikiwa noti 22 , BX 728792 zikiwa noti 20, BX 728791 noti 19 na BX7287487 zikiwa noti 15 na kufanya jumla ya thamani ya Sh 870,000 ambazo ni bandia.

Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Rashidi Shabani (30) na Michael Lukasa (39), wote wakazi wa Ngerengere wanashikiliwa na Polisi kwa kuwakuta na nyama ya nyati kilo 300 na silaha aina ya gobole iliyotumika kumuulia mnyama huyo.

Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Matei, alisema walikamatwa Mei 14, mwaka huu saa 2:00 usiku katika kijiji cha Kinonko, kata ya Gwata, wilaya ya Morogoro.

Matei alisema, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jitihada zinazofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kukomesha vitendo vya uhalifu.
 
Na polisi nao wanajihusisha na uhalifu, tutakimbilia wapi sasa jamani
HAHAHA NIMEBAKIA.. NASHANGAA YAANI HAWA JAMAA SIJII NI MISHAHARA MIDOGO AMA NI KUAMUA TU YAANI UKIFIKA PALE POLISI AMA UKIWA NA TATIZO UTAWATAMBUA .. RUSHWA NI JAMBO LA KAWAIDA KABISAA .. NA NINAIMANI HUWA MAJAMBAZI NI MARAFIKI ZAO..
 
Aaah kumbe jamaa alisema,ni kawaida askar polisi kuwa na,note za bandia
AMESEMA MAMBO KAMA HAYA YAKUWA NA NOTI BANDIA NI KAWAIDA ATII HUKO JESHI LA POLISI NDO MAANA NIKASHANGAA NA NIKAMUULIZA KUWA YE NI POLISI ILI ANIELEWESHE NI KAWAIDA KIVIPI ILA KALA KONA HAHAHA
 
Jitayarishe kujibu hoja siku ukitiwa mikononi kwa makosa ya mitandao
HAHA ACHA UOGA WAKO HUU NDO UNAOUMIZA WATZ WENGI.. MI JUZ KATI ASKARI KANIOMBA RUSHWA KANILAZIMISHA NIKAMUNULIE BIA ILI KUMKAMATA MHALIFU WANGU SIKUMPA HATA SEN TANO NA BADO NAZUNGUSHWA HADI LEO NIKITAKA KUMUUONA MKUU WA KITUO SIKUBALIWI NAAMBIWA ETI NITASUMBUKA SANA , ETI KUMKAMATA MTUHUMUWA NIMPE 25000 NDO TWENDE KISA GANI !?SASA KWANI HAWALIPWI MSHAHARA ?KODI ZETU ZINAWEKA MAFUTA KWENYE MAGARI YA POLISI KWANINI WANIULIZE KAMA NINA USAFIRI?????????????????? UKIENDA POLISI ALMOST KILA KITU UNAKILIPIA.......... ANZIA KOPI ZA KARATASI UNAANDIKIWA MOJA UNAAMBIWA UTOE 5... POLISI NI WEZI KABISAAAA AU HICHO CHOMBO HAKIWEZI KUJIENDESHA? MTUHUMIWA WAKO UNALIPA,
KWENDA KUMKAMATA,LOSS REPORT UNATOA KOPI HATA KUMI ZA 100/=

KWANINI SASA? HAWANAGA BAJETI AU BAJETI YA HICHI KITENGI INAENDA WAPI HATA HUU NI WIZI NA UHALIFU
 
Back
Top Bottom