Polisi Moro lasema linachunguza madai ya Askari Polisi kumshambulia Mwananchi anayemiliki banda la kuonesha mpira

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,110
12,571
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafuatilia malalamiko ya Wolter Fuime (32), Mkazi wa Mjimwema ambaye analalamika kushambuliwa na Askari Polisi waliokuwa doria.

Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Alex Mkama-SACP amesema Mei 26, 2024 Askari Polisi walifika kwenye banda la Wolter analotumia kuonyesha video majira akidai waliend kufanyia kazi taarifa fiche kuwa eneo hilo linatumiwa kufanya matendo yaliyo kinyume na maadili ikiwemo kuonyesha picha za video zisizo na maadili kwa Watoto na kumkamata mmiliki huyo wa banda na baadae kumwachia kwa dhamana.

Mkama amesema “Baadaye Mkama alilalamika kutojisikii vizuri, hivyo akaomba hati ya kutibiwa, akapewa, kwa kuwa kila hati ya matibabu inayotolewa lazima kuwe na uchunguzi, hivyo tumechukua hatua ya kulichunguza suala hilo kubaini ukweli.”
 
Back
Top Bottom