Naamka asubuhi leo tarehe 19 April nakwenda kujinunulia gazeti langu la Mwananchi gazeti hili limepambwa na picha moja kubwa inayoonyesha askari wawili wakike na watatu wakiume wakiwa wamempiga Tanganyika jeki mama mmoja na chini kuna maandishi yanayosomeka: Mtuhumiwa chini ya ulinzi halafu chini yake kuna maneno yasemayo mwanamke akiwa amedhibitiwa na askari magereza wa mkoa wa Morogoro baada yakudaiwa kufanya fujo! sasa kinachonishangaza ni kuwa kweli askari watano kumshika mwanamke mmoja tu? askari wa bongo wanahitaji mafunzo ya ziada sasa.
Pengine huyo mama hana adabu!
Nashangaa!!Kivipi mkuu?Unashabikia jambo kama hili karne hii?Aaagh..!
Pengine huyo mama hana adabu!
"Chini ya Ulinzi" ni msemo wa wanajeshi nashangaa polisi na magereza wanautumia bila kuelewa maana yake.Je askari magereza ana mamlaka ya kumuweka mtu chini ya ulinzi? Do they have the power to arrest.
Nadhani hawana mamlaka hayo, huyu mama anaweza kufungua kesi na kupata pochi ya kutakata. Sheria inawapa mamlaka ya delea na wafungwa tuu na si vinginevyo