Asante, hata mimi nimeiona picha, kweli ni udhalilishwaji wa hali ya juu, naomba wale wanaofuatilia mambo ya unyanyasaji kama huu waingilie kati mambo kama haya ya aibu kubwa.
Naamka asubuhi leo tarehe 19 April nakwenda kujinunulia gazeti langu la Mwananchi gazeti hili limepambwa na picha moja kubwa inayoonyesha askari wawili wakike na watatu wakiume wakiwa wamempiga Tanganyika jeki mama mmoja na chini kuna maandishi yanayosomeka: Mtuhumiwa chini ya ulinzi halafu chini yake kuna maneno yasemayo mwanamke akiwa amedhibitiwa na askari magereza wa mkoa wa Morogoro baada yakudaiwa kufanya fujo! sasa kinachonishangaza ni kuwa kweli askari watano kumshika mwanamke mmoja tu? askari wa bongo wanahitaji mafunzo ya ziada sasa.
ngoja nikatafute hilo gazeti, sijui ntalipata!Nami nimeiona mpk ile nguo yake ya ndani inaonekana.Wanamdhibitije huyu wakati hana hata silaha?Au sifa kwa boss alikuwa karibu.
Naamka asubuhi leo tarehe 19 April nakwenda kujinunulia gazeti langu la Mwananchi gazeti hili limepambwa na picha moja kubwa inayoonyesha askari wawili wakike na watatu wakiume wakiwa wamempiga Tanganyika jeki mama mmoja na chini kuna maandishi yanayosomeka: Mtuhumiwa chini ya ulinzi halafu chini yake kuna maneno yasemayo mwanamke akiwa amedhibitiwa na askari magereza wa mkoa wa Morogoro baada yakudaiwa kufanya fujo! sasa kinachonishangaza ni kuwa kweli askari watano kumshika mwanamke mmoja tu? askari wa bongo wanahitaji mafunzo ya ziada sasa.
Kumbe Tanganyika jeki bado inatumika!!!!!!!!!!!!!
Pengine huyo mama hana adabu!