Askari kanzu

Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,234
531
Kama neno hili ni tafsiri ya neno la Kiingereza "Plain cloth police officer", je hili vazi "KANZU" linahusianaje/linalandanaje na kutokuvaa sare?
 
Tafadhali Mh. Gurta: kwa Kiingereza andika "Plainclothes officer". Hata "detective" itafaa.
 
Kama neno hili ni tafsiri ya neno la Kiingereza "Plain cloth police officer", je hili vazi "KANZU" linahusianaje/linalandanaje na kutokuvaa sare?
Hili neno limekuwapo tangu enzi za ukoloni. Maana yake, kama wachangiaji wengine walivyosema, ni askari anayevaa kiraia (njagu, jasusi, usalama wa taifa etc). Enzi za ukoloni ulikuwa unaweza kukuta jamaa kavaa kanzu na kibaraghashia kumbe jamaa ni askari (plainclothes officer) aliyepo kazini. Staili hii iliendelea hata baada ya uhuru ingawa nadhani siku hizi watu wengi hawatumii sana hili neno.
 
Back
Top Bottom