Askari aliyezuia wizi bandarini Dar atekwa

badala ya kusifia wizi umegunduliwa nyie mnapindisha maneno. Miaka iliyopita tulisikia watu wakilizwa shaba zao uliona mtu kushikwa? Funguka. Huo wizi mpaka zambia wakasusa kupitisha shaba zao hapa hakuna aliyekamatwa, sasa tunaona kikwete akiwashika, si hao tu, juzi juzi tuliona shaba imekamatwa morogoro. Na bado mtazidi kumchukia kwa kufichuwa madudu yenu.

wewe toa mapovu tu, wewe, jk na wenzio (nyinyiemu) woote ni dhaifu tu,na kuna siku yaja ambapo mtaturudishia tanganyika na tutawanyonga mchana kweupe. Piga keleeleeeeeeee lakini ujue siku yaja mark my words. Tanzania ni ya watanzania woote na sio ya kikundi kidogo cha watu.
 
Fidelis Butahe na Jannifer Summi | 11 September 2012 MMOJA wa askari wa bandari, Cornell Kufahaizuru aliyeshiriki operesheni ya kuzuia jaribio la wizi wa shaba na mafuta Bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, juzi ametekwa na watu wanaodaiwa ni wahusika wa jaribio hilo.Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe zilieleza kuwa juhudi za kumtafuta zinafanywa na vyombo vya dola nchini.Licha ya Dk Mwakyembe,chanzo kingine cha habari cha kuaminika kutoka Kitengo cha Ulinzi na Usalama katika bandari hiyo, kimethibitisha kutokea kwa tukio hilo.Waziri Mwakyembe alisema Kufahaizuru alitoweka siku moja baada ya kupambana na katika zoezi la wizi huo, hajulikani alipo."Juhudi za kumtafuta huyo kijana na waliomteka zinaendelea, lakini mpaka sasa hajapatikana ingawa kuna taarifa zisizo rasmi zinazoeleza kuwa kuna maeneo huwa anaonekana," alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:"Uhalifu wa aina hii ni mpya kabisa, huu ni ukurasa mpya wa uhalifu nchini lazima tupambane nao, unaweza kuufananisha na zile filamu za nchini Nigeria."Awali, askari mmoja katika kitengo cha ulinzi bandarini hapo kwa sharti la kutotajwa, alidaiKufahaizuru alitekwa na watu wasiojulikana juzi.Alisema jana kuanzia saa 7:00 mchana walianza kupokea ujumbe mfupi wa maneno kutoka simu ya askari huyo, ukitoa masharti ya kuachiwa kwa wahusika wote waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la wizihuo.Chanzo hicho kinadai kuwa, watekaji hao wametoa saa 24 kutimizwa kwa sharti hilo na iwapo halitatekelezwa kwa wakati, wametishia kumuua askari huyo.Kuhusu hatua zilizochukuliwa mpaka sasa za kumwokoa askari huyo, chanzo kingine cha habari kutoka ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, kimedai kuwa wanafanya kila linalowezekana na wameshaanza rasmi msako mkubwa wa kuwasaka wale wote wanaohusika na utekekaji huo na wanatarajia kuwanasa muda wowote.Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Bandari, Mranda hakukanusha wala kukubali na kudai kuwa yuko safarini akirejea Dar es Salaam. Jumamosi iliyopita, watu 10 wakiwamo polisi wawili walikamatwa kwa tuhuma za kutaka kuiba shaba katika bandari hiyo.Shaba hiyo iliyokuwa katika kontena, inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh1 bilioni na ilikuwa iibwe saa 9:00 usiku wa kuamkia juzi.Tukio hilo linadaiwa lilikuwa likiratibiwa na polisi kadhaa wakiwamo wa Kikosi cha Mamlaka Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), walioingiza bandarini kichwa cha treni pamoja na watu wengine wanane kwa ajili ya kutekeleza wizi huo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi, askari wa bandari walipata taarifa za kuwapo kwa uhalifu huo na kwenda eneo hilo na walikuta watuhumiwa hao wakipakia shaba hiyo.
Nape akiiona hii atasema ni chadema, nchi inaongozwa na mzaifu sasa kila kitu ni zaifu
 
Isjekuwa ndio hao wakina Rama wametumwa na Vasco, hii nchi haiaminiki. Magamba at work


Send via ...................
sigpic4261000_2.gif
 
HIVI KUNA NCHI DUNIANI HAINA WIZI???????? Kila KIKWETE. hata mkeo siku ukisikia amezaa na mwanaume mwingine utasema KIKWETE
 
umetokea wizi wa shaba mnasema KIKWETE, mwizi amekamatwa mnasema tena KIKWETE. sasa mlitaka TANZANIA KUSIWE NA WEZI? au wezi wasikamatwe?????? Utawala wa NYERERE watu wameiba wakaitwa wahujumu wa UCHUMI, utawala wa MWINYI watu wameiba sana na akaitwa RUKSA, utawala wa MKAPA watu wameiba sana sana kwenye EPA, NDEGE YA RAIS, KIWIRA, MIGODI YOTE etc. Wanamuogopa mkapa coz alikuwa mtemi. Sasa KIKWETE kawapa uhuru waa kuongea mnachonga. sasa tatizo ni nini UPOLE, UKABILA au UDINI?????
 
Kuna gazeti limeripoti amepatkana Iringa!!!! Hebu tupate taarfa zaidi. Alifikaje Iringa? Na yuko hali gani?
 
''Nimepewa orodha ya watu wanaoiibia TRA na kule bandarini.......nawajua kwa amajina'' Jakaya Mrisho Kikwete , 2010

Hata wale wa madawa ya kulevya na wanaofadhili ujambazi si majina anayo? Hadi anakaribia kuondoka madarakani amewafanyia kitu gani? Papa msofe alipokuwa na dili chafu na kina mtoto wa ndama, marehemu Mpakanjia, na wengiine kwani serikali hawafahamu? Kama itasema haifahamu basi hatuna idara ya usalama wa taifa!!! Au kwa kuwa wakati wa uchaguzi ndiyo wafadhili wakuu?
 
Hongera Intelijensia yetu. Inamudu kujua sms wanazotumiwa wabunge wa CCM zinatoka wapi, lakini wanashindwa kuelewa sms ya mtekaji nyara wa askari mwenzao.

Jeshi la polisi linakuwa na askari wakati wa kuzima mikutano, lakini halina askari wa kulinda usalama wa raia.

Nchi hii ni bomu la wakati, muda wowote linaweza kulipuka, tukae mkao wa kufa!
 
Kitu kimoja watu wengi msichokijua...hao mnaoita Mapolisi ni MAJAMBAZI WAKUBWA....narudia hao ni MAJAMBAZI wakubwaaaaaa.....na kwasababu ya udhaifu wa hii serikali eti wao ndio mnaita walinzi wa usalama....

I agree with you mkuu. Yaani TZ ukiona Polisi unakosa amani maana unakuwa umeona jambazi. Ni watu hatari kwa raia wema. Kila kukicha hawaishi kuwabambika watu kesi na wakinusa pesa mahali wanaziendea kwa nguvu. Haya ni matokeo ya uongozi legelege.
 
Hata wale wa madawa ya kulevya na wanaofadhili ujambazi si majina anayo? Hadi anakaribia kuondoka madarakani amewafanyia kitu gani? Papa msofe alipokuwa na dili chafu na kina mtoto wa ndama, marehemu Mpakanjia, na wengiine kwani serikali hawafahamu? Kama itasema haifahamu basi hatuna idara ya usalama wa taifa!!! Au kwa kuwa wakati wa uchaguzi ndiyo wafadhili wakuu?

Mkuu hapo kwenye red, huyu jamaa anayejulikana kwa kufadhili ujambazi aitwaye Massawe, polisi wanamuogopa kama ukoma na hatujuwi ana uhusiano gani na wakuu wa nchi. Kuna siku moja kijana mmoja aliyefahamiana na Massawe kwa kumfanyia kazi zake za kawaida alikamatwa na polisi akiwa amebeba bidhaa fulani na polisi wakawa wanataka rushwa. Kijana akampigia simu Massawe kuwa nimekamatwa na polisi, Massawe akanyanyua simu na kumpigia kamanda wa polisi wa Kinondoni akimwambia "Haloo, anataja jina la kamanda, hao mbwa wako wamemkamata kijana wangu waambie wamwachie haraka sana, kamanda akawapigia simu wale polisi wakamwachia haraka sana yule kijana huku wakimwambia, aaah kumbe ndo maana ulikuwa na jeuri eeeeh, tuachie basi angalau ya kunywea maji". Kwa ujumla hatuko salama kwa kuwategemea polisi, ni MUNGU tu mwenye kutulinda sasa waTZ.
 
Mimi naamini hamna ujambazi wowote mkubwa unaofanyika hapa Tanzania bila kuhusisha Polisi.. I am telling you siku polisi wakiamua kusema no..ujambazi utaisha siku hiyi hiyo. Otherwise itakuwa ni movies tu zinazotofautiana na seasons na stellings.. Makamando wangine ni wasanii tu..huku wanakula cha juu!!!

Ni kweli mkuu. Si uliona jinsi walivyosafisha barabara ya Nyerere hivi juzi ili wale majambazi waibe pesa pale CBA na kutokomea kirahisi! Kule Mwanza majambazi wanaishi mapangoni kule Bugando na polisi wanajua hilo ndo maana mtu wao wa karibu akiibiwa huwa hawakawii kuwakamata au kupata vitu vilivyoibiwa. Ndo maana mtu anaweza kuvamia na majambazi na kituo cha polsi kiko karubu na piliso wanakuja saa moja baada ya kupewa taarifa. Huko mwanza pikipiki za polisi ndo hutumika kusambaza dawa za kulevya.
 
Askari ambae alitoa taarifa za kufanikisha kuwakamata maaskari polisi majambaz wakiiba kontena la shaba bandarini nae ametekwa na mapolisi hao wezi,askari uyo wa bandari ndugu cornel kufahaizuru aliyeshiriki opereshen ya kuzuia jaribio la wizi wa shaba na mafuta bandari ya dar es salaam mwishoni mwa wiki jana,je mh mwakyembe alisema mapolisi hao wez jumatatu wangefikishwa kortini mbona kimya ? wenye updates zozote kuhsu mkasa huu watujuze wadau hapa jamvini
 
Huyu jamaa na wengine mbona wana habari zake mm nashauri wamtafute mke wake kwani kune tetesi toka kwa wakwe wanawasiliana amemuondoa Hofu, habari nyingine zinasema kuwa yupo Iringa.
Hawa wezi na Polisi ni kitu kimoja mtathibitisha km mlishaiona picha ya yule askari aliyemlipua mwandishi wa habari huko Iringa alivyolindwa
 
Back
Top Bottom