Askari aliyezuia wizi bandarini Dar atekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari aliyezuia wizi bandarini Dar atekwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Sep 11, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Fidelis Butahe na Jannifer Summi | 11 September 2012

  MMOJA wa askari wa bandari, Cornell Kufahaizuru aliyeshiriki operesheni ya kuzuia jaribio la wizi wa shaba na mafuta Bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, juzi ametekwa na watu wanaodaiwa ni wahusika wa jaribio hilo.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe zilieleza kuwa juhudi za kumtafuta zinafanywa na vyombo vya dola nchini.

  Licha ya Dk Mwakyembe,chanzo kingine cha habari cha kuaminika kutoka Kitengo cha Ulinzi na Usalama katika bandari hiyo, kimethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

  Waziri Mwakyembe alisema Kufahaizuru alitoweka siku moja baada ya kupambana na katika zoezi la wizi huo, hajulikani alipo.

  "Juhudi za kumtafuta huyo kijana na waliomteka zinaendelea, lakini mpaka sasa hajapatikana ingawa kuna taarifa zisizo rasmi zinazoeleza kuwa kuna maeneo huwa anaonekana," alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:

  "Uhalifu wa aina hii ni mpya kabisa, huu ni ukurasa mpya wa uhalifu nchini lazima tupambane nao, unaweza kuufananisha na zile filamu za nchini Nigeria."

  Awali, askari mmoja katika kitengo cha ulinzi bandarini hapo kwa sharti la kutotajwa, alidaiKufahaizuru alitekwa na watu wasiojulikana juzi.

  Alisema jana kuanzia saa 7:00 mchana walianza kupokea ujumbe mfupi wa maneno kutoka simu ya askari huyo, ukitoa masharti ya kuachiwa kwa wahusika wote waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la wizihuo.

  Chanzo hicho kinadai kuwa, watekaji hao wametoa saa 24 kutimizwa kwa sharti hilo na iwapo halitatekelezwa kwa wakati, wametishia kumuua askari huyo.

  Kuhusu hatua zilizochukuliwa mpaka sasa za kumwokoa askari huyo, chanzo kingine cha habari kutoka ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, kimedai kuwa wanafanya kila linalowezekana na wameshaanza rasmi msako mkubwa wa kuwasaka wale wote wanaohusika na utekekaji huo na wanatarajia kuwanasa muda wowote.

  Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Bandari, Mranda hakukanusha wala kukubali na kudai kuwa yuko safarini akirejea Dar es Salaam.

  Jumamosi iliyopita, watu 10 wakiwamo polisi wawili walikamatwa kwa tuhuma za kutaka kuiba shaba katika bandari hiyo.Shaba hiyo iliyokuwa katika kontena, inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh1 bilioni na ilikuwa iibwe saa 9:00 usiku wa kuamkia juzi.

  Tukio hilo linadaiwa lilikuwa likiratibiwa na polisi kadhaa wakiwamo wa Kikosi cha Mamlaka Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), walioingiza bandarini kichwa cha treni pamoja na watu wengine wanane kwa ajili ya kutekeleza wizi huo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi, askari wa bandari walipata taarifa za kuwapo kwa uhalifu huo na kwenda eneo hilo na walikuta watuhumiwa hao wakipakia shaba hiyo.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mfanyakazi anatekwa... Nchi ni ya Wezi...
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ama kweli serikali legelege ndiyo matunda yake hayo!

  Ngoja tuone mwisho wa filamu hii nzuri sana!
   
 4. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Hicho ni kipimo cha namna wezi na majambazi wanavyotamalaki hapa nchini chini ya uongozi dhaifu wa jk na ccm yake.mwakyembe naye akae sawa watamteka nyara hata yeye asipoangalia wampeleke kule pande.
   
 5. peri

  peri JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  yani watu wamekuwa na ujasiri wa ajabu katika kutuibia.
  Wanaona wizi ni haki yao na hili ni kutokana na kuwalea mafisadi, sasa kila mmoja nae anataka kuiba tena kwa lazima.
  Aibu iliyoje kwa taifa letu?
   
 6. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  This is not like a movie but its a movie!!! utafikiri mambo ya James Bond 007.
   
 7. commited

  commited JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Zomba umesikia mambo ya serikali ya jk, wapi ile maneno serikali inamkono mrefu??, watu wamekwiba mabilioni ya epa, meremeta, kiwira, uswis, rada, kesi za utata kama za babu seya,zombe, mauaji ya polisi kwa raia wake nyamongo, singida, morogoro, arusha, iringa, mwanza nk....maisha duni kwa kila mtanzania, ukosefu wa mikopo vyuo vikuuu takribani graduates 500,000 (2010-2011) hawana ajira... Wizi wa rasilimali kila sehemu... Na watu hao bado wapo serikalini na wengine ni mawaziri.... Hizi ni salamu zangu kwako zomba na mnaoishabikia nyinyiemu
   
 8. i

  iseesa JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Je Hao watekaji wana uhusiano na "CHIZI" wa Kamanda Kova aliyemteka Ulli? Natumaini Kova ataunda Tume itakayoongozwa na Ahmedi Msangi. KUMBUKA: Msangi alikuwa na kikosi chake (alipokuwa Moro) cha kushusha mizigo kwenye magari Makubwa kilichojulikana kama "SHUSHA SHUSHA"
   
 9. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mabwepande inanukia....
   
 10. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  De-legitimization of a state! Crime has infiltrated into the state organs and they are part of criminal rings. Mababe wa Kivita na interahamwe-like gangs wanazaliwa na mifumo kama hii.
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Mara vielelezo muhimu kuhusu waliosimamishwa kazi vimepotea, mara kampuni iliyosimamishwa zabuni yake inaenda mahakamani, mara wafanyakazi wa bandari wanataka kugoma...what the hell is going on? Hivi bandarini si kuna waajiriwa kama waajiriwa wengine? Mbona tunataka kuruhusu watu wachache wajifanye wao ndio wamiliki wa bandari? Kama wanafuja mali ya umma waende zao. Nahisi wanataka kuonyesha kwamba they are unshakable.
   
 12. N

  Nagoya Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani matapeli wa shaba nchi hii hawajulikani. Serikali acheni kutu chezea wahusika mnawajua hata viongozi waandamizi wa jeshi la police dili hili wanalijua. Hata baadhi ya cooper sheet zilizoibiwa kipindi cha nyuma zinajulikana zilipo.
   
 13. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Haishangazi kwa kuwa aliyetekwa ni mtetezi wa rasilimali ya Taifa na angekuwa fisadi au mwezi wa rasilimali za Taifa ningeishangaa nchi yangu.
   
 14. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,827
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Kitu kimoja watu wengi msichokijua...hao mnaoita Mapolisi ni MAJAMBAZI WAKUBWA....narudia hao ni MAJAMBAZI wakubwaaaaaa.....na kwasababu ya udhaifu wa hii serikali eti wao ndio mnaita walinzi wa usalama....
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  waeleze maana sijui hata wamelishwa nini hao watu.
   
 16. s

  sawabho JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Wezi wa kuku ndio wanaoshughulikiwa na wamejaa katika magereza, wezi wakubwa wanadirki kuteka mtu na kutokomea naye. Taarifa za Kiintelijensia haziwanasi hawa, Mkono wa Serikali unaendelea kwa baadhi ya wahalifu unakuwa mrefu, lakini baadhi unakuwa mfupi !!!
   
 17. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Dah Uzalendo Umemponza.ANGEUNGANA NAO KUSINGEKUWA NA TABU....
   
 18. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kauli moja tu hapa kua kwanza anafahamika na wezi na inawezekana baadhi ya police walitumika kumuuza mwenzao. Ila tusubiri coz hua wanapiga kelele hapa IGP hafai wanakaa kimya kama viziwi, haya ni madhara ya ushemeji katika vyeo.
   
 19. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Wajinga tu hawa wanahangaika na watu wasikuwa na makosa yoyote!! Kina Mwangosi, Chadema nk.....vitu vya maana kama hivi vina washinda!!
   
 20. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwa mtindo huu hatutafika mkuu. Katika harakati zozote lazima watu wataumia. Haki haichukuliwi kwenye sahani ya dhahabu.
   
Loading...