Askari ajipiga risasi na kujiua

Askari ajipiga risasi na kujiua

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,918
Reaction score
38,244
ASKARI polisi mjini Kigoma, Koplo Selemani Mohamed Mbaga (39) maarufu kwa jina la Makamba amejiua kwa kujipiga risasi jana asubuhi nyumbani kwake, eneo la Bangwe mjini Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, George Mayunga aliwaambia waandishi wa habari mjini Kigoma kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa moja na robo asubuhi muda mfupi baada ya askari huyo pamoja na mwenzake kuchukua silaha tayari kwa kuingia kazini.

Kamanda Mayunga alisema kuwa askari huyo mwenye namba E 1827 alikuwa kwenye kikosi cha kupambana na ujambazi barabarani na kwamba siku ya tukio akiwa na askari mwenzake walikuwa wakiondoka kuelekea lindoni tayari kwa kutekeleza wajibu wao wa kazi.

Alisema kuwa baada ya kuchukua silaha na kuanza safari kidogo kuelekea lindoni alimwambia askari mwenzake kuwa kuna kitu amesahau nyumbani kwake maeneo ya Bangwe mjini Kigoma na ndipo wakarudi na alipoingia ndani kwake mara ukasikika mlio wa bunduki.

Aliongeza baada ya askari wenzake kusikia mlio huo wa bunduki waliingia ndani kwa askari huyo kujua kulikoni na ndipo walipomkuta tayari amejipiga risasi kifuani na kufa papo hapo.

Kamanda Mayunga alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana japo inaelezwa kuwa alikuwa na matatizo binafsi na kwamba afya yake ilikuwa ikiporomoka kila siku.

Mwili wa marehemu ambaye ameacha watoto wawili ulitarajiwa kusafirishwa jana kupelekwa nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro kwa maziko
 
tulishajua msiba wa taifa wengine, kumbo huyo. watu tena tuanze kuwapa rambi rambi akina burn
 
Hebu acha hizo bana. Hii inahusiana nini na siasa? Halafu kwa nini jina la "Makamba" umeliweka kwenye mabano kwenye kichwa cha habari kama sio uchokozi tu!!!
 
Duh! sasa watu mnafanya kufuru, Mod pse ondoa hilo jina hapo juu na weka jina halali
 
Back
Top Bottom