Asilimia kubwa ndugu huvunja ndoa za ndugu zao

Kabla ya kuoa au kuolewa jitahidi utengeneze mazingira ya nyumbani, hii itapunguza utegemezi.
 
Ila pond hata huyo mchepuko nae anastahili adhabu huoni km ndiye anafanya huyo jamaa akudharau?
 
Mimi juzi tu nimemkataza mpwa wangu kuja kukaa kwangu.

Ni hivi, huyu mpwa wangu nilimleta mjini, nikasimamia show akapata msingi wa kukaa mjini. Mimi baadae nikachomoka nimefikia ughaibuni ila mke wangu mmoja yupo mkoani. Sasa mpwa anataka kuhama Dar kurudi mkoani baada ya miaka kama 7 hivi toka nimuache Dar, anaomba nimpe hifadhi kwangu.

Yaani afikie kwa mke wangu anapojipanga, hii siyo mara ya kwanza yeye kujaribu kurudi mkoani, 2019 aliniomba hifadhi hivi hivi nikamruhusu, cha kushangaza alifika kwangu na watoto wawili, kwanza hakuniambia amepata mtoto wingine mdogo. Wa kwanza nilijua anaye ila pia hakuniambia anakuja naye kwangu.

Sasa baada ya muda akaamua kuondoka kurudi Dar, leo anaomba kurudi kwangu. Inamaana nitakuwa na wajibu wa kumlisha na watoto wake wawili, najua tu atakapofika tu wataanza mambo yao ya wanawake watagombana na mke wangu bure, mke wangu na mtoto wangu nawahudumia kwa bajeti nayoiweza mimi, nikimruhusu aje na watoto wake wawili ntakuwa na bajeti ya watu watano na karaha juu.

Nimeamua kuwa mbaya. Sitaki ujinga wa ndugu. Isitoshe nyumbani kwao siyo mbali na ninapoishi sema kwa kuwa amechezea maisha kama mwanamke anaona aibu kwenda kukaa nyumbani kwao.

Nimemuambia kwangu hakuna nafasi ajipange atafute namna ya kuanza maisha. Nimefanya hivyo kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima katika familia yangu na pia kumpa changamoto ajisimamie, siyo kila siku aje kuomba msaada atazoea.

Akakae kwao
Kukaa na watu ni kazi mno
 
Naongelea uhuru wa wanandoa wanapokuja watu hamtakuwa huru hata kulaliana sebuleni mnakaa mnajichunga kila muda wakati mpo kwenu
Nakuelewa Sana, tatizo Ni Kwamba wakati wa uchumba huwa tunajifanya kuwapenda sana hao ndg na hata kuishi nao hatuonagi tatizo
 
Wakati wa uchumba mbona mnajifanya kuwapenda sana ndg wa mume? Hizo kanuni za kutobanwa mziainishe kabla ya kuolewa, acheni roho mbaya, maisha ya kiafrika ndo hayo, Kwanza ndg wa mume unakuwa na hakika hawezi kukuibia mume kwa asilimia nyingi
Ndugu wa mume hawhaaat???? teh utashangaa sana kujua wanaokuita wifi ndio wanaotombbbana na mmeo haya mambo haya yacheki tu kwa mbali
 
Kuoa .ni kuongeza familia .unakuwa na famila ya upande wa mume na mke .hivyo basi kuishi kiujamaa ni bora zaidi kuliko kuishi watu wwngi.mimi binafsi napenda ndugu waje kwangu wakae angalau mwezi nafurahi.! Utakuta mtu kalelewa n shangazi au bibi ila yeye akioa anachukia kuja kwa ndugu huo ni ubinafsi. Kama suala ni chokochoko zinazuilika.
 
Kuoa .ni kuongeza familia .unakuwa na famila ya upande wa mume na mke .hivyo basi kuishi kiujamaa ni bora zaidi kuliko kuishi watu wwngi.mimi binafsi napenda ndugu waje kwangu wakae angalau mwezi nafurahi.! Utakuta mtu kalelewa n shangazi au bibi ila yeye akioa anachukia kuja kwa ndugu huo ni ubinafsi. Kama suala ni chokochoko zinazuilika.
Ni kweli lakin wawape hata muda basi hata mwaka au miaka miwili
Mmeoana hata mwezi haujaosha wageni
 
Kuvunjika ndoa ? Sababu ni Kukosa Uvumilivu na Diplomasia....

Ndugu, Wanonko, Wafitini walikuwepo tangu enzi na enzi...., Ndugu kuja kuishi / kuamia kabisa ilikuwepo zamani kuliko hata sasa, mtu sasa hivi anajenga nyumba ndogo ya kwake na familia yake..., zamani lazima nyumba iwe na guest rooms, sasa hivi mtu akitembea / anafikia hata hotelini; zamani ufikie hotelini wakati ndugu yako yupo eneo hilo anaweza kusema umemdharau..., So what has changed ?

Uvumilivu / Diplomasia na kuweza kuishi kwa ku-adapt
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom