Asili ya uchawi na kuabudu Maiti, Jua na Mwezi ni Babeli siku chache baada ya gharika ya Nuhu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Kuna mambo manne ambayo Yanapatikana duniani kote kwa asilimia kubwa kabla hata hatujaingiliana (globarization)

1:Watu kuabudu wafu katika desturi zao.

Desturi hii utaikuta utaikuta australia, japan, afrika yote, India,
America Yote, Ulaya, na kila mahala. Hii inaonyesha ufanano huu ambao hauwezi kutokea kwa kuibuka ''Evolve" ni ushahid tosha Kuna siku moja mahali flani watu wote walikuwa wanaishi sehemu moja.
Ibada hizi nyingi, zinapatikana siku hizi hadi katika baadhi ya imani za kikristo,baadhi ya waislam, wabudha.

2; Sikukuu za kumbukumbu za wafu.

Bibilia inasema Safina Ilituama juu ya mlima hararati tarehe ya kumi na saba ya mwezi wa kwanza.
Kwa Kalenda mpya ya kiebrania iliyoanza kuanzia walipotoka misri tarehe hiyo inaanguka mwanzoni mwa mwezi wa tisa.

Tarehe hii au karibu na hii inasherekewa
Peru,kwa wahindu,Mexico, Wakazi wa kaskazini wa visiwa vya pacific, wa australia wa asili, Waajemi na wamisri wa zamani waliisherekea, Mataifa ya kaskazini mwa ulaya, Warumi wa zamani na kwingineko. Baadhi ya wakristo wanasherehe zinazogongana na tarehe hiyohiyo katika kuadhimisha vifo vya watu wao wakidini.

3: uwepo kwa Stori za watu kuokolewa kupitia meli/mtumbwi na aina ya stori zinazoendana na ile ya Nuhu.
uwepo wa stori kuhusu kuwahi kutokea mafuriko na watu kuokolewa kwa njia ya kitu kama mtumbwi upo katika zaidi ya tamaduni 150 duniani kote.
Stori hizi zimekuwepo hata kabla mambo ya imani za kikristo na kiislam kuwepo. Hii ni ushahidi kwamba kuna siku moja watu walikuwa pamoja, wakatawanyika na hiki tunachokiona ni mwangwi wa kile ambacho waliwahi kukiamini wakati wako pamoja. Na mababu wa mababu wao ni wale waliotawanywa pale babeli kwenye mnara.

4: KUABUDU JUA
Ibada za Kuabudu jua,miezi, miandamo ya miezi, nyote na viumbe pia ilianzia huko huko babeli.
Iliaminika wakuu wao wakina Nimrod walikufa walipaa kwenda mwezini, juani na huko angani.
Ibada hii inasura ya kidunia na utaikuta kila kona ya Dunia mfano.
*Misri ya Zamani - Ra, Osiris etc
*Kaanani - Baal, Shamas, Adoni etc
*Syria - Tammuz, Elagabalas
*Umedi na uajemi - Ormuz na Mithra
Wahindi - Mitra
Wagiriki - Apollo, Adonis na Hercules

HISTORIA YA UCHAWI/IBADA YA WAFU/ NA TAMADUNI ZOTE ULIMWENGUNI ZINATURUDISHA PALEPALE BABELI.

Kwa Mujibu wa Vyanzo mbalimbali vya kihistoria,
Vinakubaliana na inachokisema Bibilia kuwa Ustaarabu wa mwanadamu ulianzia pale katika Bonde la SHINARI.

1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.

" Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko...9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote. ''
Mwanzo 11:2,3,9

Wababeli hawa waliambatana na Ibada ya wafu, ndugu zao waliokufa katika Ile Gharika. Lakini Pia waliianzisha sherehe hiyo ya wafu wao siku ambapo Safina Ilitua juu ya mlima hararati.
Hivyo baada ya Kutawanywa sio jambo la ajabu kukuta desturi hizo zikiendelea kila kona. Hapo ndio chanzo cha uchawi wote na tamaduni zote zakijadi duniani hadi huu Kwetu Tanzania.

Ustaarabu wa Dunia Ulianzia babeli kwa wakaldayo, Ukaenda Misri, wagiriki wakautoa misri na kuuingiza Ulaya. Warumi wakauchukua kutoka kwa Wagiriki. Na ustaarabu huo mwingii ukatapakaa tena dunia hii ya kisasa kutokea ulaya. Lakin kabla miaka mingi iliyopita Siku ambayo wanadamu walitawanywa na kuchafuliwa Lugha dunia nzima baada ya gharika walizisambaza katika asili na tamaduni zote duniani.

Miungu Ya Babeli ambayo ilikuwa na Utatu wao Mtakatifu yaani BABA,MAMA, na Mwana (Nimrod, semiramis na Tammuz) Imetapakaa dunia nzima kwa majina tofauti tofauti. Na miungu hii yote iliwahi kuwa watu halisi siku za nyuma kabla hawajafanywa miungu.
Mfano, Mwanahistoria Prutaech anasema makuhani wa kimisri waliwafundisha kuwa hao miungu yaani Osiris, Horus na Volcan walikuwa watu halisi huko nyuma.
Alexander The great aliwahi kumuandikia barua mama yake mzazi akimwambia miungu yao Saturn, Jupiter, Juno, wote walikuwa watu halisi kama alivyoambiwa na kuhani mkuu wa miungu ya kimisri Leo alipokuwa akifundishwa siri za miungu. Miungu hii inauwezo wa Kutokea watu na kuwapa maelekezo ya Kiungu.

Mwisho;
Hakuna jipya chini ya jua. Miungu na taratibu nyingi za kipagani dunia ya sasa bila kujali ni ya kisasa kiasi au imeingizwa kwenye dini kwa kificho kiasi gani chanzo chake ni Babeli, Zikaingia Misri, na Kuingizwa Ulaya na Wagiriki kisha kusambaa dunia yote ya kisasa. Ila dunia ya Kale ilisambaa kupitia Machafuko ya Lugha pale mnara.

Hii ndiyo sababu Kitabu cha UFunuo kwa mafumbo kinaifananisha hali ya dunia ya siku za mwisho na Babeli ile ya zamani na upagani wake.
Anawaita wanadamu Wote watoke katika mifumo ya kiibada inayoelekezwa kwa wafu, Jua, miezi, Ushetani na kila aina ya mfumo wa maisha usiompendeza.

Ufunuo 18:1Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
 
Nijuavyo mimi tunaishi kizazi cha nyoka.... Kizazi kile cha Sodoma na Gomora
mkuu Sodoma na Ghomorah nao walichokifanya uasisi wake ni hapohapo bonde la SHINARI/Babeli.

YEREMIA 23
13 Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli.
14 Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.

::::::::::::::::::::::
Ukiangalia pale Juu nimeeleza mungu Baali asili yake ni hukohuko BABELI.
Huyu aliabudiwa misri, syria, kaanani na sehemu kubwa katika middle east na dunia.
Wagiriki walimuita BELOS baadae Zeus. Ila chanzo chake ni Babylon.

Kwa kaanani alikuwa Mungu wa Uzazi. Katika sherehe yake, wanawake walivaa nguo za wanaume na wanaume za wanawake kukawa na Uzinzi, ushoga, Usagaji katikati ya sherehe mambo ambayo sodoma na gomora yalikuwa kawaida tu.

Ndio maana wana wa israel walipokaribia KAANANI Mungu aliwakataza wanawake kuvaa mavazi ya kiume na wanaume ya kike na Kushiriki sherehe na miungu hiyo ya kaanani alijua nini kingetokea.

Yote haya yatajirudia. huyo ni bahari ambaye alikuwa shetani huyohuyo na mawakala wake katika udanganyifu akiwaaminisha JUA, au Maiti zilizokufa kumbe ni majini na mapepo.

hivyo mkuu, Sodoma na Gomorah ni TAwi tu la Babeli kulekule. Tena kule sadaka katika sikuukuu zake Mabikra walizitoa bikra zao kwa huyo Mungu kwa kujichomekea kwenye alters ambazo zilikaa kama uume au kwa sasa tuziite Dildo.
 
Aisee mbona unabifanya nijione 0brain, yaani nilikuwa sijawahi kuwaza kama ni hivi, kuhusu babeli najiulizaga tu, ni nani aliyebaki na Lugha ya Adam
 
Mwazo wa uovu (Polytheism) ulianzia Ancient Babylon (Babeli) au kwa jina lingine Mesopotamia.....Nimrod - Semiramis - Tammuz.....Ambao pia Roman Catholic wanafuata mfumo huu wa kipagani wa Ibada...NI PM KAMA UNA SWALI AU UNAPENDA KUJIFUNZA ZAIDI
 
Back
Top Bottom