Asili ya neno "IFAKARA"

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,520
2,000
IFAKARA ni makao makuu ya Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro,
Tanzania na kitovu cha eneo lenye mashamba makubwa ya miwa . Kuna kituo muhimu cha TAZARA.
Mji uko katika bonde la mto Kilombero takriban kilomita 420 kusini-magharibi mwa Dar es Salaam.

Ifakara ni mji mkubwa kuliko yote ya wilaya ya Kilombero, wenye makabila makuu mawili maarufu kama
Wapogoro na Wandamba, wenye mfanano wa kuelewana katika baadhi ya matamshi ya lugha zao.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 55,956 walioishi humo.

Taasisi muhimu mjini ni Taasisi ya Afya Ifakara (Ifakara Health Institute) inayofanya uchunguzi wa kisayansi wa magonjwa kama malaria na ukimwi .
Kanisa Katoliki linaendesha Hospitali ya St Francis inayotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya pamoja na chuo cha wauguzi.
Tangu tarehe 14 Januari 2012 mji ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Ifakara.

ASALI YA NENO IFAKARA.

Jina Ifakara lilitokana na neno ufwakara lenye maana amekwishakufa. Neno hilo tena lilitokana na nyoka mkubwa ambaye alikuwa tishio kubwa kwa wakazi wa mji huo: watu mbalimbali waliuawa na mifugo pia kuuawa.
Jitihada nyingi zilifanyika kumuangamiza nyoka huyo na mwishowe walifanikiwa kumuua, ndipo neno ufwakara lilipovuma kwamba amekwishakufa. Wageni wengi kutoka sehemu tofautitofauti walishindwa kutamka vizuri jina hilo na kutamka Ifakara, mpaka leo Ifakara ndilo jina kuu la mji huo ndani ya wilaya ya Kilombero.Kama kuna mwingine anayeijua historia ya mji wa Ifakara atujuze zaidi.
 
lazalaza

JF-Expert Member
Dec 15, 2012
3,003
2,000
Asante sana mkuu huku ni kwetu maeneo ya V/60 minarani pale, nimefurahi sana kuona kanisa kubwa wenyewe tulikuwa tunaliita, maana zamani kanisa lilikuwa hilo st Frances, kkkt pale kwa namanji, alafu likafuata lile la walokole kule Kongo karibu na sheik nyambuka.

Nilisoma kidogo madukani miaka 80, Ifoza yetu
 
Mkwaju Ngedere

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
1,050
2,000
Nimeona jina LA NAMANJI, kuna ndugu anaitwa KASSIM NAMANJI, nilifanya nae kazi RAILWAYS GARAGE MBEYA,kama yupo tuwasiliane 0682 000511, 0712 000511
 
Oxx

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
729
1,000
Safi kwa kutujulisha... Historia hii..
Picha za kitambo kidogo Ila Ufwakara mjini sasa Hiv in Full Lami.
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
8,749
2,000
IFAKARA ni makao makuu ya Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro,
Tanzania na kitovu cha eneo lenye
mashamba makubwa ya miwa . Kuna kituo muhimu cha TAZARA.
Mji uko katika bonde la mto Kilombero takriban kilomita 420 kusini-magharibi mwa Dar es Salaam.

Ifakara ni mji mkubwa kuliko yote ya
wilaya ya Kilombero, wenye makabila makuu mawili maarufu kama
Wapogoro na Wandamba, wenye mfanano wa kuelewana katika baadhi ya matamshi ya lugha zao.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 55,956 walioishi humo.

Taasisi muhimu mjini ni Taasisi ya Afya Ifakara (Ifakara Health Institute) inayofanya uchunguzi wa kisayansi wa
magonjwa kama malaria na ukimwi .
Kanisa Katoliki linaendesha Hospitali ya St Francis inayotarajiwa kuwa
hospitali ya wilaya pamoja na chuo cha wauguzi.
Tangu tarehe 14 Januari 2012 mji ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Ifakara.

ASALI YA NENO IFAKARA.

Jina Ifakara lilitokana na neno ufwakara lenye maana amekwishakufa. Neno hilo tena lilitokana na nyoka mkubwa ambaye alikuwa tishio kubwa kwa wakazi wa mji huo: watu mbalimbali waliuawa na mifugo pia kuuawa.
Jitihada nyingi zilifanyika kumuangamiza nyoka huyo na mwishowe walifanikiwa kumuua, ndipo neno ufwakara lilipovuma kwamba amekwishakufa. Wageni wengi kutoka sehemu tofautitofauti walishindwa kutamka vizuri jina hilo na kutamka Ifakara, mpaka leo Ifakara ndilo jina kuu la mji huo ndani ya wilaya ya Kilombero.

Kama kuna mwingine anayeijua historia ya mji wa Ifakara atujuze zaidi.
Weka picha
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,473
2,000
Huu mji si ndo ulikuwa na AKA yake IFOZA?
Nalo maana yake nini?
Thanks for sharing that comrade.
 
displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,737
2,000
IFAKARA ni makao makuu ya Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro,
Tanzania na kitovu cha eneo lenye
mashamba makubwa ya miwa . Kuna kituo muhimu cha TAZARA.
Mji uko katika bonde la mto Kilombero takriban kilomita 420 kusini-magharibi mwa Dar es Salaam.

Ifakara ni mji mkubwa kuliko yote ya
wilaya ya Kilombero, wenye makabila makuu mawili maarufu kama
Wapogoro na Wandamba, wenye mfanano wa kuelewana katika baadhi ya matamshi ya lugha zao.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 55,956 walioishi humo.

Taasisi muhimu mjini ni Taasisi ya Afya Ifakara (Ifakara Health Institute) inayofanya uchunguzi wa kisayansi wa
magonjwa kama malaria na ukimwi .
Kanisa Katoliki linaendesha Hospitali ya St Francis inayotarajiwa kuwa
hospitali ya wilaya pamoja na chuo cha wauguzi.
Tangu tarehe 14 Januari 2012 mji ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Ifakara.

ASALI YA NENO IFAKARA.

Jina Ifakara lilitokana na neno ufwakara lenye maana amekwishakufa. Neno hilo tena lilitokana na nyoka mkubwa ambaye alikuwa tishio kubwa kwa wakazi wa mji huo: watu mbalimbali waliuawa na mifugo pia kuuawa.
Jitihada nyingi zilifanyika kumuangamiza nyoka huyo na mwishowe walifanikiwa kumuua, ndipo neno ufwakara lilipovuma kwamba amekwishakufa. Wageni wengi kutoka sehemu tofautitofauti walishindwa kutamka vizuri jina hilo na kutamka Ifakara, mpaka leo Ifakara ndilo jina kuu la mji huo ndani ya wilaya ya Kilombero.

Kama kuna mwingine anayeijua historia ya mji wa Ifakara atujuze zaidi.
Na jua ukijani haushagi huko,
Tausi Likokola ndio alipotokea huko,
Mchungaji Lwakatare ndio kwao huko,
Kwilo Boys ndio kwao huko,

Machache hayo
 
Tareeq

JF-Expert Member
May 3, 2010
772
500
Ngoja nikuulize je mila zao zikoje nasikia wanaoana kindugu ndugu na je wanaume wanatunza mikono ya sweta au na wadada wanakeketwa au wako fresh
 
lazalaza

JF-Expert Member
Dec 15, 2012
3,003
2,000
Ifakara means kafua kala ( kulikuwa na simba alikuwa anasumbua, wenyeji wakasema kafuakala). Kwa kiswahili keshakufa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom