Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,443
IFAKARA ni makao makuu ya Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro,
Tanzania na kitovu cha eneo lenye mashamba makubwa ya miwa . Kuna kituo muhimu cha TAZARA.
Mji uko katika bonde la mto Kilombero takriban kilomita 420 kusini-magharibi mwa Dar es Salaam.
Ifakara ni mji mkubwa kuliko yote ya wilaya ya Kilombero, wenye makabila makuu mawili maarufu kama
Wapogoro na Wandamba, wenye mfanano wa kuelewana katika baadhi ya matamshi ya lugha zao.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 55,956 walioishi humo.
Taasisi muhimu mjini ni Taasisi ya Afya Ifakara (Ifakara Health Institute) inayofanya uchunguzi wa kisayansi wa magonjwa kama malaria na ukimwi .
Kanisa Katoliki linaendesha Hospitali ya St Francis inayotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya pamoja na chuo cha wauguzi.
Tangu tarehe 14 Januari 2012 mji ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Ifakara.
ASALI YA NENO IFAKARA.
Jina Ifakara lilitokana na neno ufwakara lenye maana amekwishakufa. Neno hilo tena lilitokana na nyoka mkubwa ambaye alikuwa tishio kubwa kwa wakazi wa mji huo: watu mbalimbali waliuawa na mifugo pia kuuawa.
Jitihada nyingi zilifanyika kumuangamiza nyoka huyo na mwishowe walifanikiwa kumuua, ndipo neno ufwakara lilipovuma kwamba amekwishakufa. Wageni wengi kutoka sehemu tofautitofauti walishindwa kutamka vizuri jina hilo na kutamka Ifakara, mpaka leo Ifakara ndilo jina kuu la mji huo ndani ya wilaya ya Kilombero.
Kama kuna mwingine anayeijua historia ya mji wa Ifakara atujuze zaidi.