Serikali Ifanye Usanifu wa Mabonde ya Umwagiliaji Ifakara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE ABUBAKAR ASENGA ATAKA SERIKALI IFANYE USANIFU MABONDE YA UMWAGILIAJI YA IFAKARA

Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mkoani Morogoro, Abubakar Asenga katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni tarehe 13 Juni, 2023 ameiomba Serikali kuyaangalia Mabonde ya Umwagiliaji Ifakara

"Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa umwagiliaji wa Kisawasawa wa Kilombero"? - Mhe. Abubakar Asenga, Mbunge wa Jimbo la Kilombero

"Skimu ya umwagiliaji ya Kisawasawa ipo katika Kata ya Kisawasawa Tarafa ya Mang'ula Wilaya ya Kilombero. Skimu ipo umbali wa kilomita 43 kutoka Mji wa Ifakara kupitia barabara ya Ifakara-Mikumi." - Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde

"Skimu ya Kisawasawa ina eneo la umwagiliaji lenye ukubwa wa Hekari 500. Mwaka wa fedha 2023-2024 Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya umwagiliaji imetenga fedha kwa ajili ya kufanya mapitio ya ufanisi ili kupata gharama halisi za utekelezaji miundombinu ya umwagiliaji" - Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde

"Mkurugenzi wa umwagiliaji aliahidi kwenda yeye mwenyewe, Naibu Waziri wa Kilimo atamuelekeza lini ili aende kutembelea mradi wa Kisawasawa? - Mhe. Abubakar Asenga, Mbunge wa Jimbo la Kilombero

"Kijiji cha Lungongore Kata ya Ifakara wana eneo linalofaa kwa umwagiliaji hasa wakati wa kiangazi, Naibu Waziri uko tayari kumuagiza Mkurugenzi kwenda na Lungongore kama Kisawasawa?" - Mhe. Abubakar Asenga, Mbunge wa Jimbo la Kilombero

"Nitamuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji kufika Kilombero mapema kadiri iwezekanavyo. Tulisaini mkataba wa kuwaajiri kwaajili ya kuyafikia mabonde yote nchini ikiwemo bonde la Ifakara Idete. Tayari tunayo Kampuni ambao wako asilimia 13 ya kufanya usanifu wa umwagiliaji katika bonde la Ifakara" - Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde.

IMG_0763.jpg
xfcg.jpg
 
Back
Top Bottom