Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Marahabaaaa!
 
Shikamoo kaka Shimba(goti hadi ardhini huku na kichwa nimeinamisha)
Marahabaaaaaaa !!!

Yaani hapa nilipo nipo nimekunja na nne kabisa nashika shika midevu yangu. Na kwa vile ushaniambia kuwa mi si furushi basi najiona kama dunia yote ni yangu. Kabarikiwe sana ewe binti mwema
 
Ndio maana mtoto hawezi kumsalimia mtoto mwenzake "Shikamoo" au watu wenye umri unaolingana hawasalimiani shikamoo.....
SALAMU YA SHIKAMOO NI KWA AJILI YA KUMSALIMIA MTU ALIYEKUZIDI UMRI TUU.............
Kwahiyo Shikamoo kwa siku hizi ina maana gani? kama ina maana ya salamu mbona salamu nyingine za kibantu zina maana nzuri yenye uhalisia wa wakati.
 
Kwahiyo Shikamoo kwa siku hizi ina maana gani? kama ina maana ya salamu mbona salamu nyingine za kibantu zina maana nzuri yenye uhalisia wa wakati.
Mkuu, kiuhalisia SHIKAMOO si salamu. Huko Lamu ambako ndo chimbuko la lugha hii ya Kiswahili, hawasalimiani kwa kutumia neno hilo.
 
hivi na MARAHABA maana yake ni nini? nimesikia mengi kuhusu shikamoo
 
Mkuu, kiuhalisia SHIKAMOO si salamu. Huko Lamu ambako ndo chimbuko la lugha hii ya Kiswahili, hawasalimiani kwa kutumia neno hilo.
Sidhani sasa ivi kila anae amkia anamaana ya kwamba niko chini ya miguu yako
 
Hii yote inatokana na kutokujua Maana yake na Nidhamu ya Uwoga.
 
Sidhani sasa ivi kila anae amkia anamaana ya kwamba niko chini ya miguu yako
Sahihi ila kiasili ni kuwa watoto huwaamuru wakubwa washike miguu yao. Neno hili nasikia ni la Kireno na lilitumika enzi hizo za utumwa kwa mtumwa akimkosea bwana wake basi kusamehewa aliamuliwa amshike kiganja cha mguu bwana mkubwa.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…