Asili ya dunia ni dhambi na dhambi si hatia

Asili ya dunia ni dhambi na dhambi si hatia

Southern Highland nakujibu kwamba sihalalishi dhambi bali dhambi tiyari ilishaalalishwa na dunia tuiishi kabla hata sijazaliwa, naona umeigusia serikali ambayo ipo kwa kuwa dhambi ipo

mfano dhambi haipo na watu hawavunji sheria unahisi muhimili wa mahakama(legislature) utakuwepo? Na vipi kuhusu kila mtu akiwa mnyoofu na tamaa(dhambi) haipo juu ya umiliki wa vitu wala mamlaka kuna haja ya kuwa na serikali au dini?

Vipi kuhusu biashara bila kumwongezea cha juu mteja(uhesabiwa kama dhambi kuchukua zaidi ya halali yako na kumpamba akuchangie hata kama bidhaa unayompa si bora unavyoinadi na hata baadhi ya imani zinataka mabenki yasitoze riba,watu wasinywe pombe au kumiliki bar n.k) unahisi faida ingepatikana vipi?
 
Ila jaman aliebuni silaha (BUNDUKI) sijui apiwezaje!! Uoiangalia inavyofany kazi na nguvu yake DAAH!!!
 
'Kufa kufaana' tupo duniani 'kuchumia tumbo' na hakuna dhambi nikitenda dhambi kwa sababu ipo hili niitende niishi, Niende moja kwa moja kwenye hoja:-

Lengo la kutengeneza silaha nikuua watu, nia nikupata pesa unapoziuza, hapo unazalisha ajira na mapato ya serikali ambayo baadaye yanakwenda kulipa wafanyakazi ambao baadaye watakwenda kununua bidhaa nakuwachangia wafanyabiashara nakutoa sadaka kanisani ambazo baadaye uboresha miundombinu na maisha ya watumishi wa kanisa kuendelea kukemea uovu.

Magonjwa yanapotengenezwa kupitia vyakula,madawa,mitindo ya kimaisha, maabara na baadaye kuenezwa kimakusudi kwa kujua, je wanaofanya hivyo huwa wanakuwa wamekosea au wako sawa?

Achana na kifungo cha utu na huruma(ubinadamu) ebu fikiria kwa umakini, mfano Ukimwi, Kansa, kisukari na magonjwa mengine yanayotesa wanadamu leo hii yapate dawa nakutokomezwa kabisa, je wahisi ni faida kwa dunia au hasara?

Je, ni ajira ngapi zitapotea, biashara za madawa itakuwaje, vipi mapato, wangapi watapoteza taaluma zao,n.k

Je, ikiwa watu wataachwa waongezeke pasipo kuuliwa/kupunguzwa kwa njia mbalimbali wahisi dunia itakuwa mahala salama pa kuishi ukizingatia rasilimali tuliyonayo(scarcity) na uwiano wa matumizi/uhitaji wake, je itabaki kwenye balance nzuri?

Kumbe shida yako ndo kuponea kwangu bila wewe kupata shida mi nikaja kukutatulia/kuneemeka na kutokuwepo kwako hatujaishi bado, hivyo nikikupa nabarikiwa ila nikikukwapulia unanilaani(dhambi) nikiwapelekea familia ile riziki niliyokwapua wakala wasife njaa(baraka) hivyo bila kutenda dhambi maisha duniani yasingewezekana

Kwa maana kupitia dhambi jema huja kusawazisha ubaya baadaye dhambi uchukua nafasi yake kumaintain equilibrium na ni endless process hivyo nathibitisha kwamba dhambi siyo hatia bali ipo hili tuiishi.
Dhambi ni hatia, isipokuwa asili ya dhambi yenyewe ndiyo siyo hatia. Binadamu yeyote anazaliwa akiwa na asili ya dhambi, ambayo hiyo pekee siyo hatia kwake ila ni kwamba asili hiyo ndiyo huwa inamuweka katika uwezekano mkubwa wa kuingia kwenye hatia kirahisi sana na muda wowote ule!
 
Hakika...
Wachache wenye taarifa za muhimu ndiyo hutawala wengi waliyokua gizani...

Cc: mahondaw
 
Dhambi ni hatia, isipokuwa asili ya dhambi yenyewe ndiyo siyo hatia. Binadamu yeyote anazaliwa akiwa na asili ya dhambi, ambayo hiyo pekee siyo hatia kwake ila ni kwamba asili hiyo ndiyo huwa inamuweka katika uwezekano mkubwa wa kuingia kwenye hatia kirahisi sana na muda wowote ule!

Kwahyo unathibitisha kuwa asili ya binadamu ni dhambi(anazaliwa akiwa nayo) ila akiishi uhalisia
wake huo ni hatia?
Kumbuka umesema dhambi ni hatia na binadamu anazaliwa akiwa tiyari na asili ya dhambi, sasa kama asili yake ndiyo hiyo kivipi utegemee aishi kivingine? hivyo bado msimamo wangu ni kuwa dhambi si hatia bali ipo tuiishi.
Labda unipe sababu yenye mashiko kwanini mwanadamu awe na hatia kwa kutenda kile ambacho ni asili yake.
 
'Kufa kufaana' tupo duniani 'kuchumia tumbo' na hakuna dhambi nikitenda dhambi kwa sababu ipo hili niitende niishi, Niende moja kwa moja kwenye hoja:-

Lengo la kutengeneza silaha nikuua watu, nia nikupata pesa unapoziuza, hapo unazalisha ajira na mapato ya serikali ambayo baadaye yanakwenda kulipa wafanyakazi ambao baadaye watakwenda kununua bidhaa nakuwachangia wafanyabiashara nakutoa sadaka kanisani ambazo baadaye uboresha miundombinu na maisha ya watumishi wa kanisa kuendelea kukemea uovu.

Magonjwa yanapotengenezwa kupitia vyakula,madawa,mitindo ya kimaisha, maabara na baadaye kuenezwa kimakusudi kwa kujua, je wanaofanya hivyo huwa wanakuwa wamekosea au wako sawa?

Achana na kifungo cha utu na huruma(ubinadamu) ebu fikiria kwa umakini, mfano Ukimwi, Kansa, kisukari na magonjwa mengine yanayotesa wanadamu leo hii yapate dawa nakutokomezwa kabisa, je wahisi ni faida kwa dunia au hasara?

Je, ni ajira ngapi zitapotea, biashara za madawa itakuwaje, vipi mapato, wangapi watapoteza taaluma zao,n.k

Je, ikiwa watu wataachwa waongezeke pasipo kuuliwa/kupunguzwa kwa njia mbalimbali wahisi dunia itakuwa mahala salama pa kuishi ukizingatia rasilimali tuliyonayo(scarcity) na uwiano wa matumizi/uhitaji wake, je itabaki kwenye balance nzuri?

Kumbe shida yako ndo kuponea kwangu bila wewe kupata shida mi nikaja kukutatulia/kuneemeka na kutokuwepo kwako hatujaishi bado, hivyo nikikupa nabarikiwa ila nikikukwapulia unanilaani(dhambi) nikiwapelekea familia ile riziki niliyokwapua wakala wasife njaa(baraka) hivyo bila kutenda dhambi maisha duniani yasingewezekana

Kwa maana kupitia dhambi jema huja kusawazisha ubaya baadaye dhambi uchukua nafasi yake kumaintain equilibrium na ni endless process hivyo nathibitisha kwamba dhambi siyo hatia bali ipo hili tuiishi.
Najua wewe uwa unafanya meditation, umefikiri mbali sana na umeuona uhalisia. Kiukweli dunia ndo iko hivyo na itaendelea kua hivyo, watu watakubishia kutokana na mapokeo ya dini Ila wakiamua kua neutral watakuelewa vizuri. AHSANTE
 
Kwanini umeangalia upande wa faida pekee?
Kwa haraka haraka waweza dhani nimebezi katika kuongelea faida pekee ila ukirudia kusoma bandiko langu utanielewa, upande wa wachangiaji wameniuliza wakiegemea upande mmoja wa hasara za dhambi ndiyo maana majibu yangu yamekuwa upande wa faida kuprove kuwa kile kionekanacho kama hasara ni faida ya upande mwingine yaani ukipoteza mwingine anaokota na kinyume chake.

Je, wadhani kwa kuwa dhambi inapelekea simanzi,majonzi,manung'uniko,unyanyasaji,majuto,dhuluma,wizi,mauaji,ukatili,usaliti,upweke,ushirikina nakadhalika yapaswa kuwa hatia?

Je, kuna jema pasipo ubaya, na pasipo ubaya jema linamaana gani? Endapo ukifukuzwa kazi leo hii kwa mtizamo wa juu juu wa jumla ni kuwa umepoteza (ni kweli kwako ni hasara na mateso makubwa kwa wategemezi wako), ila mahali ulikotoka wanakuwa wameangukia faida/neutral tu na sio hasara. Ebu tulinyumbue kuthibitisha kwa pande zote mbili tuone kama lina ukweli ndani yake:-

Hasara kwako binafsi; itakuathiri kisaikolojia, kukosa matumaini,kushuka kiheshima nakudhalilika, kukosa mahitaji muhimu, kukosa mwelekeo kimaisha,kuchanganyikiwa,kujiua n.k

Faida kwako binafsi; itaimarisha zaidi ukaribu na imani yako, utagundua uwezo wako wa kufanya kazi nyingine nje ya ile ya mwanzo,itakurejeshea heshima kama mpambanaji, utawashangaza waliokutendea ubaya kwa mafanikio yako,utapata uzoefu juu ya kuvunjika moyo, utawavutia na wengine kuthubutu n.k
Hasara kule ulikotoka(kazini); nafasi ulioiacha itatumika gharama mpya kuijaza,msaada/uwepo wako utakosekana,pengine ulikuwa na uwezo mkubwa/utaalamu hivyo kumpata mwingine kama wewe itawachukua muda na biashara itayumba,pengine umeondoka na wateja wako au ubunifu nakadhalika.

Je faida ulikotoka ikoje: wameajiri upya kwa kiwango cha mshahara mdogo kuliko waliokuwa wakikulipa,wamepata jembe jipya lichapa kazi,wamefanikiwa kulinda nidhamu au maadili ya kazi, wamefanya nepotism,wameweka mfukoni fungu la kuajiri na mafunzo n.k

Kwahiyo katika huu mfano utaona kuwa faida na hasara hazitupani, yaani dhambi na jema ni pande mbili za shilingi na haziachani inategemeana kwa wakati huo umechagua/umejikuta huko katika upande upi na ufanyeje upindue shilingi urudi kwenye upande mwingine, hivyo haitoshi kusema kuwa kuna upande ni hatia na mwingine hauna bali pande zote ni halali na utumika pamoja pasina hatia.
 
Kwahyo unathibitisha kuwa asili ya binadamu ni dhambi(anazaliwa akiwa nayo) ila akiishi uhalisia
wake huo ni hatia?
Kumbuka umesema dhambi ni hatia na binadamu anazaliwa akiwa tiyari na asili ya dhambi, sasa kama asili yake ndiyo hiyo kivipi utegemee aishi kivingine? hivyo bado msimamo wangu ni kuwa dhambi si hatia bali ipo tuiishi.
Labda unipe sababu yenye mashiko kwanini mwanadamu awe na hatia kwa kutenda kile ambacho ni asili yake.
Hapana hujanielewa. Tukisema kuwa mtu ana asili ya wizi, anaweza kuwa hata hajawahi kuiba hata mara moja, ila pengine labda wazazi wake wanaonyesha kuwa walikuwa hivyo. Tunaweza kusema kuwa "huyu mtu kuna siku atakuja kuiba, ana asili ya wizi". Kwa hiyo mtu aliye na asili ya dhambi, anaweza kuwa tayari ameshatenda dhambi, au hajawahi kutenda ila uwezekano mkubwa ni kuwa lazima tu atakuja kutenda dhambi kwenye muda fulani. Kuwa na asili ya dhambi siyo dhambi, isipokuwa ni mazingira kama ya kuwa na mimba ya dhambi yanayopelekea watu kuwa na uhakika kabisa kuwa lazima tu siku mioja utajifungua mtoto dhambi. Kwa hiyo mimba siyo mtoto, na mtu hawezi akawa ana vyote viwili, mimba ya mtoto A pamoja na mtoto A kwa wakati huo huo
Zaidi ni kuwa aliyesema kuwa dhambi ni hatia siyo wewe, ni Mungu. Hapa sasa labda umwondoe Mungu kwanza, yaani useme kwamba Mungu hayupo halafu ndiyo uhalalishe issue ya dhambi kutokuwa hatia, kwa sababu ulizaliwa ukiwa tayari una asili ya dhambi, haikuwa hiari yako. Ukimwondoa Mungu, dhambi inakuwa siyo hatia kwa sababu ni kitu ambacho automatically ulizaliwa nacho kikiwa ni sehemu yako, ila ukimwingiza Mungu unakuta kuwa yeye ndiye akliyesema kuwa dhambi ni hatia na anayo sababu ya msingi sana kussema hivyo ambayo hata wewe unaweza kukubaliana nayo pasipo ubishi wowote, assuming tu unaamini kwamba Mungu yupo, na possibly una evidence pia kadhaa za kuweza kuthibitisha uwepo wake.
Mungu yupo na kama huamini hilo, ni kwa vile tu hujawahi kuweka jitihada za kutosha kuweza kumtafuta. Na Dhambi ni hatia pia, inabidi ukubaliane vizuri sana na hilo
 
Mkuu nimekuelewa vizuri sasa hapo kwenye asili ya dhambi ulichokuwa umemaanisha kabla ila ulipogusia juu ya Mungu nikapata maswali mengine(siyo kwamba simwamini Mungu bali mi ni mdadisi tu)
Ikiwa katenda kosa bosi wako kazini na wewe wa chini yake ndo ukabebeshwa ule msalaba ukawajibishwa kwa kosa la mwingine uhitwa kutimiza wajibu,

je ina utofauti gani na kuzaliwa bila kosa nakubebeshwa msalaba wa makosa ya wengine hili uwajibike?

Je, unahisi ukirithishwa dhambi (kuzaliwa ukiwa na asili ya kukosea) ambayo si makosa/mapenzi yako, hiyo siyo dhambi kwa yule akuhukumuye kwa mapungufu ya wengine?
Nakama ndo hivyo kuna uhalali gani wakusema dhambi ni hatia ilihali kila upande watenda jambo lile lile, umesema kuwa muumba alikuwa na sababu za msingi kututia hatiani kwa dhambi zetu ila ujazitaja.
 
Kwa mtizamo wangu mimi, ule wa kibinadamu tu na si ule wa maandikoa matakatifu perce, "The Doctrine of Collective Responsibility" ndiyo inayofanya kazi hapa, kwamba Mungu alitoa maagizo kwa Adam na Hawa na uzao wao wote, kwamba kila watakalotenda litaathhiri uzao wao wote. Tuseme kwa mfano babu yako wewe alimwachia mali nying baba yako mzazi na kumwagiza azitunze na kuzirithisha vizazi na vizazi vitakavyofuata. Ikitokea kwa bahati mbaya baba akafuja mali hizo na maisha yakabadilika na kuwa ya umaskini, je wewe utasema kuwa hauishi maisha ya kifukara kwa sababu si wewe uliyefuja mali, wakatui upo chini ya mikono ya baba yako ambaye hana mali tena? Ukweli ni kuwa hata wewe pia utalaqzimika kuishi maisha hayo hayo ya ufukara uliosababishwa na kosa la baba yako mzazi wmpaka pale utakapopata uwezio wa kujikwamua kutoka kwenye kosa hiloi. Utaishi maisha ya ufukara kwa kipindi fulani ISIPOKUWA, utakuwa huna haki ya kuishi maisha hayo ya kifukara
.
Hivyo basi, wanadamu wote wana asili ya dhambi, lakini hawana HAKI ya kuendelea kuishi kwenye asili hiyo. Damu ya Yesu aliyefanyika kafara msalabani ilishaondoa HAKI ya wewe kuishi maisha ya asili ya dhambi, ila haijaiondoa ile asili yako ya dhambi. Ni kweli una asili ya dhambi lakini huna tena HAKI ya kuishi kwenye asili hiyo. Ya kuambiwa sasa chanhganya na za kwako
 
Watu hawawezi kumwelewa mleta mada, ila binafsi mtazamo wangu unafanana sana na mleta mada. Binafsi siamini uwepo wa dhambi, hakuna dhambi ila kuna hatia.

Kwa mfano mimi nikiua mtu, hiyo siyo dhambi...ila naweza kuwa na hatia au nisiwe na hatia pia kwa sababu hatia inategemea chanzo, mazingira yaliyosababisha mimi niue.
 
hivyo haitoshi kusema kuwa kuna upande ni hatia na mwingine hauna bali pande zote ni halali na utumika pamoja pasina hatia.
Hii haiapply kwa binadamu mwenye nafsi ya kibinadamu kwenye chochote kile kuhusu dhambi.
Hapo ndipo unapata tofauti ya mnyama na binadamu kiumbe mwenye ubongo wenye nguvu ya kufikiri,kuelewa na kutambua.

There's no way dhambi isiwe hatia kwa binadamu.

Mfano wewe unafika kwako unagundua baba yako amemuua mkeo na watoto wako.
Na babako amefanya hivyo akiwa hana tatizo lolote la akili ambapo tunahusisha ubongo.
Bali amefanya kwa imani za kishirikina.

Wewe hapo utachukua hatua gani?

Mifano uliyotoa haitoshi kujustify kwamba dhambi sio hatia.
 
Mtoa maada unaonekana ulijipanga, coz unajibu LA kila swali linaloulizwa na hoja zako zinamashiko, hongera katika hilo🙌🙌🙌
Dhambi haiepukiki ndo maana hata ktk Bible inasema tusiache kuomba na kufanya toba
Note; usifanye dhambi ya makusudi na yenye kumuumiza mwenzio🚶🚶🚶🚶
 
Ni kweli ulivyofundishwa na imani yako ya kikristo na si lazima niizungumzie biblia ndo bandiko langu liwe sahihi hata bila Biblia wala Quran dhambi ingekuwepo bado(akili ingeweza kung'amua jema au baya) kama unafikiria vizuri utagundua tiyari Mungu nishamzungumzia na shetani nishamzungumzia(kulingana na mtizamo wa imani yako), Hivyo kwakuwa umetaka niingie huko kabla ya kukujibu ntakuuliza maswali mawili mepesi(fikiri kwa makini kabla yakunijibu)

Ipi tofauti kuu kati ya Mungu na shetani?

Unahisi kosa la shetani pale bustani ya edeni lilikuwa ni nini hasa?
Mimi nadhani shetani hakuwa na kosa ..yeye alitumia vizuri nafasi alivyopata. Kosa alikuwa nalo yule mwanamke Eva kuruhusu kutumiwa na shetani.

Tofauti kati ya Mungu na Shetani ni "kanuni zilizopo kwenye ulimwengu usiyoonekana"

Mfano kila kwenye "imani" kila akifanyacho Mwenyezi Mungu, Shetani hukigeuza na kufanya yeye pia. Kama kutoa sadaka kama Kafara..Mungu alitoa kafara yani Yesu (hapo damu ilihusika) Hivyo shetani na yeye huwatuma wafuasi wake kutoa kafara...

Mungu au/na Shetani wote kufanya kazi kupitia mwanadamu..hakuna hata siku moja wanafanya kazi zao nje ya hapo.

Alishoshindwa shetani ni kumtengeneza mwanadamu kama Mungu alivyomtengeneza Yesu ili aje duniani kutolewa kama kafara ili watu wasamehewe makosa/madhambi kupitia iyo sadaka ya damu.

"Kiimani" shetani hawezi kuumba..na ndiyo anatumia binadamu (wachawi, waganga) kama Mungu anavyotumia pia binadamu (wachungaji, mitume, mashakhe)

Hizo ni formula za ulimwengu usiyoonekana.
 
Mi naona mtoa mada yuko sawa kihisia ila hayupo sawa kiimani😀😀

Unajua hisia ni mojawapo ya sheria za akili..akili haiwezi kuishi bila kuisi, kufikiri, kukosentreti..

Kiiman unaishi kulingana na mazingira, tamaduni, dini..ambazo hujenge na kuleta ustaarabu ma hofu flani mfano kuiba ni dhambi, lakini kwangu siyo dhambi ni kama opportunity tu umekutananayo ila ukishikwa ni sawa na opportunity imekutana na Risk na hivyo return yake ndo utajua.
 
Kwa mtizamo wangu mimi, ule wa kibinadamu tu na si ule wa maandikoa matakatifu perce, "The Doctrine of Collective Responsibility" ndiyo inayofanya kazi hapa, kwamba Mungu alitoa maagizo kwa Adam na Hawa na uzao wao wote, kwamba kila watakalotenda litaathhiri uzao wao wote. Tuseme kwa mfano babu yako wewe alimwachia mali nying baba yako mzazi na kumwagiza azitunze na kuzirithisha vizazi na vizazi vitakavyofuata. Ikitokea kwa bahati mbaya baba akafuja mali hizo na maisha yakabadilika na kuwa ya umaskini, je wewe utasema kuwa hauishi maisha ya kifukara kwa sababu si wewe uliyefuja mali, wakatui upo chini ya mikono ya baba yako ambaye hana mali tena? Ukweli ni kuwa hata wewe pia utalaqzimika kuishi maisha hayo hayo ya ufukara uliosababishwa na kosa la baba yako mzazi wmpaka pale utakapopata uwezio wa kujikwamua kutoka kwenye kosa hiloi. Utaishi maisha ya ufukara kwa kipindi fulani ISIPOKUWA, utakuwa huna haki ya kuishi maisha hayo ya kifukara
.
Hivyo basi, wanadamu wote wana asili ya dhambi, lakini hawana HAKI ya kuendelea kuishi kwenye asili hiyo. Damu ya Yesu aliyefanyika kafara msalabani ilishaondoa HAKI ya wewe kuishi maisha ya asili ya dhambi, ila haijaiondoa ile asili yako ya dhambi. Ni kweli una asili ya dhambi lakini huna tena HAKI ya kuishi kwenye asili hiyo. Ya kuambiwa sasa chanhganya na za kwako
Ikiwa aliyeiumba dhambi aliichukulia kama changamoto ambayo ni lazima iwepo hili maisha yawepo, je sisi ni nani hata tulipinge hilo kwa kuhalalisha kuwa twaweza kuiepuka dhambi kisa twaagizwa kufanya hivyo na mleta tatizo.

Labda nikukumbushe kuwa anguko la shetani kwenye dhambi si bahati mbaya bali ni mapenzi yake yeye aliyeumba ajuae viumbe vyake na hatima zao, yeye aliye mwanzo na ndiye mwisho mjuvi wakila kitu na mkamilifu peke yake.

Hivyo alivipa viumbe vyake maisha ya sura mbili yaani ndani mwao ni makazi ya vyote viwili yaani dhambi na mema huku akisisitiza mema kama mtihani/kipimo dhidi ya dhambi hili hali katika yeye vyote vilikuwamo yaani dhambi na mema, na yeye aliyetuumba kwa mfano wake pia aliruhusu dhambi au shetani aendelee kuwepo,

Mfano yeye mungu mwenye uweza,muumba,upendo na huruma isiyo na mipaka,mwingi wa rehema,msamaha na kudra ndiye huyo huyo mungu mwenye wivu, mwenye hasira iwakayo,mwenye kuadhibu kizazi kimoja mpk kingine kwa dhambi moja,mwenye roho mwovu yaani dhambi(soma kitabu cha samweli pindi ufalme wa sauli ulivyoanza kuondoka mikononi mwake kwenda kwa daudi/alivyompa roho ngumu farao n.k),mwenye kutolewa kafara za damu(uhai), kuongoza walio wake vitani kukatili vizazi na mali za maadui zao nakadhalika.
Mifano ni mingi sana ukiachilia mbali kuwajaribu yaani kutumia dhambi(shetani) kama kipimo kwa watu wake kuthibitisha imani zao juu yake,kwa lugha nyingine nikutumia vyote mema na mabaya kutawala/kutukuzwa/kuabudiwa/kutumikiwa/kujidhihirisha nakudumisha miliki imara daima.."tazama wasije wakala na matunda ya mti ule wa uzima wakaishi milele..." Kwanini akutaka viumbe vyake viishi milele achilia mbali kujitambua?
Je ikiwa dhambi ni jambo lililoundwa kwa makusudi yakumsaidia wema kujidhihirisha au mapenzi ya muumba kutimizwa kivipi ni hatia?
 
IJe ikiwa dhambi ni jambo lililoundwa kwa makusudi yakumsaidia wema kujidhihirisha au mapenzi ya muumba kutimizwa kivipi ni hatia?
Bandiko lako limenichanganya, sijakuelewa uko upande gani. maana point zilizo nyingi unakubaliana na mimi, lakini mwisho umemaliziza tena kwa swali ambalo limenichanganya. Kwa hiyo unaona kuwa dhmabi siyo hatia, si ndito? Okay, ni sawa dhambi siyo hatia, ila huwa inapelekea mtu awe hatiani. Ili kuhakikisha katika hili, nenda tu hata leo ukaibe Kariakoo
 
Back
Top Bottom