Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 954
- 510
Kwa hakika tumepita kwenye misukosuko mingi,kuanzia kutekwa kwa ulimboka,mauaji padre mushi,kumwagiwa tindikali sheikh Soroga kuuawa kwa mwandishi mwangosi Iringa,tukio la bomu arusha,nk.Sasa hivi amani imetawala na victor ameonekana ndiye mhusika mkuu anayepaswa kulisaidia jeshi la polisi kwa tukio la arusha.Tunataka nawengine waliohusika kwenye matukio mengine nao wakamatwe
Imekuwa kawaida kila tukio linapotokea polisi haileti majibu fasaha ya watu waliohusika na hayo matukio na hivyo kuruhusu akili za binadamu kuanza kutuhumiana na kujenga chuki.Tunaomba polisi ifanye kazi yake ipasavyo ili tuwajue wahusika wakuu wa matukio yote yaliyotokea.
Tunahitaji amani yetu iendelee kutamalaki.Watanzania tupaswa kumshukuru mungu kwa Tunu ya amani,polisi na vyombo vya usalama wafanye kazi yao barabara ili wachawi wanaotaka kuivuruga amani ya hii nchi wajulikane.
Mambo yanayotokea nchini kwetu,tunapaswa kuyatafakari kwa umakini,vinginevyo tutawahukumu watu kwa makosa wasiyofanya mwisho wa siku laana itaturudia wenyewe.Binaadamu wanaakili sana,ni waledi wa kutengeneza visa kwa ajili ya kufanikisha malengo waliyopanga.Mwenyezi mungu wahukumu wote wenye michezo michafu na kuhatarisha amani ya nchi yetu.