Awali ya yote ningependa kwa kuwauliza waandishi wa habari, HIVI MNAGOMBEA NINI?! Nimeona kichwa cha habari kwenye gazeti la TAIFA LETU, kwamba BALELE (au Balile?) APAKATWA NA MAFISADI!!!!! Wala sikuvutiwa na kichwa hicho hadi kunifanya ninunue gazeti hilo!!! Sana sana ni kichwa cha habari kilichonichefua na ndio maana nimekata shauri la kuandika na kuwaauliza waandishi wa habari, mnagombea nini?! Ni kweli sijasoma, lakini ni nani asiyejuwa kwamba katika matumizi yetu ya lugha, MTU KUPAKATWA, maana yake ni KUINGILIWA KIMWILI?! Huyu Balele ni mwanamke au mwanaume?! Lakini, ilimradi c rahisi kukuta wanawake wakijiingiza kwenye ujinga kama huu( wa malumbano), basi bila shaka huyu Balele atakuwa mwanaume!!! Kama hivyo ndivyo, ina maana mwandishi amemaanisha kwamba BALELE AMELAWITIWA??!! Hakika, tu wepesi wa kulalamika lakini wakati mwingine waandishi mnastahili kabisa kufungiwa!!! Siamini endapo mwandishi anayejali maadili ya kazi yake anaweza kuweka tittle kama hiyo!!! Na ningekuwa mmiliki wa gazeti hilo, ningemtimuwa kazi mhariri bila maelezo unless kama na yeye (mmiliki) anavutiwa na uvunjifu huu maadili!!!