Ashakum c matuc-mwandishi alawitiwa?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ashakum c matuc-mwandishi alawitiwa?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Oct 2, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote ningependa kwa kuwauliza waandishi wa habari, HIVI MNAGOMBEA NINI?! Nimeona kichwa cha habari kwenye gazeti la TAIFA LETU, kwamba BALELE (au Balile?) APAKATWA NA MAFISADI!!!!! Wala sikuvutiwa na kichwa hicho hadi kunifanya ninunue gazeti hilo!!! Sana sana ni kichwa cha habari kilichonichefua na ndio maana nimekata shauri la kuandika na kuwaauliza waandishi wa habari, mnagombea nini?! Ni kweli sijasoma, lakini ni nani asiyejuwa kwamba katika matumizi yetu ya lugha, MTU KUPAKATWA, maana yake ni KUINGILIWA KIMWILI?! Huyu Balele ni mwanamke au mwanaume?! Lakini, ilimradi c rahisi kukuta wanawake wakijiingiza kwenye ujinga kama huu( wa malumbano), basi bila shaka huyu Balele atakuwa mwanaume!!! Kama hivyo ndivyo, ina maana mwandishi amemaanisha kwamba BALELE AMELAWITIWA??!! Hakika, tu wepesi wa kulalamika lakini wakati mwingine waandishi mnastahili kabisa kufungiwa!!! Siamini endapo mwandishi anayejali maadili ya kazi yake anaweza kuweka tittle kama hiyo!!! Na ningekuwa mmiliki wa gazeti hilo, ningemtimuwa kazi mhariri bila maelezo unless kama na yeye (mmiliki) anavutiwa na uvunjifu huu maadili!!!
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  daaaah kwetu kule LAMU mtu akisema kapakatwa basi ndo hivo sheikh
   
 3. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  lol!! nac kwe2 ndio maana ya kupakatwa!!!!
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  lakini na wewe naona kama umekosea hiyo maana ya kupakatwa ..ina maana mama anapompakata mtoto ni kwamba amemuingilia kimwili au na mie sijui kiswahili
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Udhaifu wa lugha yetu ya Kiswahili....Masanilo alionekana amepakatia laptop yake kwenye mapaja....sidhani kama maana yake nailawiti! .....
   
 6. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 784
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 80
  Sina kamusi ya kiswahili hapa nilipo, ila naamini neno moja la kiswahili laweza kuwa na maana zaidi ya moja, huoni kwamba kuwa kutoa maana yako ya 'kulawitiwa' utakuwa labda hujamaanisha maana halisi ya mwandishi?. Mwandishi katumia sentesi tata ndiyo, lakini mzee mtoto anapopakatwa kwa mfano huwa analawitiwa?
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...sasa sisi tutajuaje kama ulikuwa unataka kuinywesha maziwa au laa?!
   
 8. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa wewe bwana umeamua kuleta matusi ukumbini. Sielewi imekuwaje hata mhariri wa JF kakuruhusu utuletee uchafu huo. Unakitukana Kiswahili chetu. Hata kama nami sijasoma, wewe ndio kabisa umeamua kujichora. Kiswahili kina maana nyingi najua. Unadhani ni mwandishi gani anaweza kuandika kwa kumaanisha wewe unavyotaka kutulazimisha tuelewe?

  Jamani, hebu tuheshimu kijiwe, kuna watu aina nying wanasoma hapa, hata wengi tu wna hadhi kama ya babu, baba, mama, bibi. Sasa utoto na ujinga wa kuvuta bangi hapa sio mahali pake. Mimi naamini wewe sio mjinga, kumradhi, mjinga kwa tafsiri sanifu ni yule asiyeelewa juu ya kile kinachoongelewa. Akielekezwa hubadilika kiungwana. Mpumbavu ni yule anayejua hatari ya kile afanyacho lakini anakifanya makusudi tu ili kutaka atakacho akifanikishe. Hata umwelimishe mwaka mzima kitu hicho hicho hatataka kamwe kujionyesha ameelewa na kubadilika, mpaka anachotaka kieleweke.

  Sijui nikuweke kundi gani. Fundi mitambo, hebu angalieni taratibu za kutozirusha habari kama hizi. Mtu asitukanwe kupitia chombo hiki. Huyu mwandishi kaamua kumtukana anayetajwa. Yawezekana JF ikashikishwa adabu kwa kuruhusu matusi ya moja kwa moja kama haya kwa mtu. Hutashitakiwa kwa kukaa kimya kama umekosa cha kuandika.

  Ukiwa na jazba usiandike. Uliza majirani kabla hujaleta ukumbini matusi yako. Kama mwandishi wa gazeti ulisemalo angemaanisha mambo yako hilo gazeti lingekuwa mshikemshike hivi sasa. Usimpotoshee mada, anza mpya ya kwako. Tafadhali JF ufunge mjadala wa habari hii kuepusha madhara zaidi.

  Leka.
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahaha hahahaha Lugha yetu inaudhaifu kufikisha ujumbe....mfano, Masanilo anatembea na First lady...inaweza leta tafsiri mingi sana. SteveD ni mzee wa kula kisamvu.....hapo mzee inaweza leta maana lukuki ....hahahahaah hasa jamaa wa Mwambao wakihusishwa....
   
 10. M

  Mbelakisa Member

  #10
  Oct 2, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ni mpotoshoshaji tena usiyefaa kuigwa. sina hakika kama wewe unajua kiswahihili kama ulivyotoa fasili yako. kwani kupakatwa ni kiswahili cha kawaida mno.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama huna cha kuleta hapa ni bora ukakaa kimya badala ya kupoteza watu...wanakodolea macho thread wee...kumbe upupu mtupu!
  Shiiit!
  Kuna jamaa mmoja humu JF ana akili sana, aliwaomba moderators waweke kitufe cha kumkandia mtu akileta pumba hapa, yaani kitufe cha opposite of THANKS... Sasa sijui akina robbot wamelichukuliaje ombi hilo, au wamelitupa kapuni, lakini kimsingi ni muhimu sana kikawepo!
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa mimi kama umesahau! Kuna jamaa hapa watakuwa na vitufe vya pumba visivyo na idadi! Jamii ina watu wa aina mbali mbali basi tuwavumilie tu....
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  mkuu hiyo idea ya kuanzisha kitufe cha kuponda imesimama sana, kama vipi pitisha petition umesahau mfumo wa tz lazima mgome ndio msikilizwe?
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  By the way ...sitakiwi kukumbuka specifically kuwa ni nani, ila nakupa big-up mkuu Masa, na ndo maana nikekupa THANKS musee!

  Ila wewe unanibania mbaya mkuu, hata thanks ya kuvunga kavu mkuu?
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mukuu PJ

  Nimeisha kutunuku Thanks hapo, sasa mzee wasiliana na Demelo kamchango kidogo JF isifungwe....si unajua mkono mtupu haulambwi? Hicho kitufe MODS wakikianzisha nadhani NasDaz atapata vyakutosha.!
   
 16. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Au tutajuaje kama unaangalia clips za Ujengelele, huku ukiimba ule wimbo wa "biashara ya kuoa sasa hivi sina?"
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  The lunacy of this thread lies in the notion that the poster felt dignified enough not to pick a copy of this rubbish and pollute his mind, but ironically enough he felt justified to unleash this same nauseating vomit into our faces.

  The irony of this thread is that the potrayed dignity and self-righteousness of the poster is exposed as sheer hypocrisy and unguided principle lacking pretense.

  If this garbage is so nauseating, as you imply, then why promote it with free advertisement here?
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  shem lol! waipakata laptop? kwa ndugu yetu Nazdaz yeye kafasiri tofauti sana.....hili ndio tatizo la kutokujua kiswahili watu kama Nazdaz kila neno wana fasiri tusi!
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wewe nawe.....hata mwenyewe hujui ulichokiandika
   
 20. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wewe kama yai halipandi kaa kimya kabla sijakuitia NN.

  Mkiambiwa muwe mnachungulia Daily Noize mara moja moja mnaona hatari.

  Mie ndiye ukweli, kuna wadau hawajui kiswahili hapa wanataka summary ya issues basi nikiandika kiswahili wanaomba nidonoe kwa Dickens diction.

  Siyo hatari wala nini, it's not like I'm being elitist by trying to force you to compare the symphonies of Vivaldi and those of Tchaikovsky with relation to the fluctuations of the chauvinistic libido.

  It is just basic English, go grab a book or something and get over it, simpleton.

  What would JF be without the whole range of this spectrum continuum?. But then again I would rather do without some aspects of the lower end of that spectrum.
   
Loading...