Asha Baraka ajitosa ubunge Kinondoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asha Baraka ajitosa ubunge Kinondoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,702
  Trophy Points: 280
  Asha Baraka ajitosa ubunge Kinondoni
  MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Asha Baraka, ameingia matatani kwa kudaiwa kuanza kufanya mikutano ya siri na wajumbe wa Tawi la Minazini, kwa lengo la kujitafutia uungwaji mkono wa kugombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni, katika uchaguzi mkuu ujao.

  Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumatano, zinadai kuwa mjumbe huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya ASET, ambao ni wamiliki wa bendi ya muziki ya Twanga Pepeta, amedhamiria kukutana na viongozi wa matawi yote na kutoa posho kwa baadhi yao ili kufanikisha azima yake.

  Katika kikao kilichoketi juzi, inadaiwa kwamba Asha alifanya mkutano na viongozi wa CCM Tawi la Mnazini, kwa lengo la kuwapongeza kwa ushindi uliopatikana katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni, sambamba na kujipigia debe la kuwania kiti hicho kinachoshikiliwa na Mbunge wa Jimbo hilo la Kinondoni, Idd Azzan.

  Tanzania Daima Jumatano iliwasiliana na mmoja wa wajumbe aliyekuwapo katika mkutano huo, ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema kuwa ni kweli alihudhuria kikao hicho na kupewa posho, lakini hakufahamu kama ilikuwa ni kwa ajili ya kikao au ilitolewa na mjumbe huyo.

  Hata hivyo, mjumbe huyo hakusita kubainisha kuwa hatua ya Asha kukutana na viongozi hao, inaonyesha wazi dhamira yake ya kuwania kiti hicho kinachotarajiwa kuwa na upinzani mkali ndani na nje ya CCM.

  “Mikutano hiyo ni endelevu kwa Asha Baraka katika matawi yote ya Kinondoni, amepanga kuonana na wajumbe katika kujadili mustakabali wa CCM kwa Jimbo la Kinondoni, katika kuweza kuchota wajumbe watakaofanikisha mpango wake,” alisema mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.

  Aidha, chanzo kingine kimeidokeza Tanzania Daima Jumatano kuwa Asha hajaanza hivi karibuni mikutano yake hiyo, bali mingine amekuwa akiifanya kinyemela.

  “Asha anatumia kila njia ya kuwafikia wajumbe kujiweka imara, ili atakapotamka hadharani nia yake hiyo awe na uungwaji mkono wa watu wengi zaidi,” kilisema chanzo cha habari.

  Akizungumzia suala la posho na vikao, Asha Baraka alikiri kukutana na wajumbe hao na kukanusha kwamba hafanyi kampeni ya kugombea ubunge mwakani, bali ni kukijenga chama na kupongezana kwa ushindi walioupata.

  Aidha, alisema kukutana kunasaidia kujua matatizo ya tawi hilo, kwa kuwa hakuwapo kwenye kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa.

  Hata hivyo alisema sababu ya kufanya mkutano katika tawi hilo ni kutokana na historia yake ya kukulia katika eneo hilo, sambamba na kuanza harakati za siasa akiwa Minazini, hivyo si rahisi kwake kusahau nyumbani.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  asili yao wapi huyu mwanamke?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,702
  Trophy Points: 280

  bonyokwa kule kimara mwisho
   
 4. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ni wa Kigoma huyu mama
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  eeh!
  KUMEKUCHA
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ishakuwa tatizo

  nilikuwa nashangaa bendi yake ilikuwa inakamua hata mwezi wa ramadhani ambao hata akina Kusaga na Freeman waliamua kunyuti

  duh!

  sasa kwa nini asigombee kwao Kigoma?
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,702
  Trophy Points: 280

  Give m a break GT
  UKIANZA KUCHUNGUZA KILA MTU TUTAKISAMBARATISHA CHAMA..CHETU CHA MAJAMBAZI...KEENJA WA UBUNGO NAE AKAGOMBEE WAPI...HAYA SHAMSA MANGUNGA NAE ANAKUJA UBUNGO NAE AKAGOMBEE WAPI...
   
 8. O

  Oshany Member

  #8
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtu kuonesha nia ya kugombea ubunge ni breaking news?
   
 9. E

  Edo JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  MNEC Nnape nayeye Ubungo au?
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Sasa anauwezo wa kwenda kujenga hoja bungeni? au ndo mambo ya kusafisha nyota, jina na maujiko ya kukaa kwenye viti vya kuzunguka? Hapa tuna kazi kubwa.
   
 11. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Namshauri amwachie Idd Azzan K'ndoni aende kumng'oa Rita Mlaki Kawe kwani dada huyu ni bomu kabisa. Hajafanya lolote tangu awe mbunge. Aliona mradi wa maji unasambazwa DSM nzima akajifanya kuwa kawe wamepata kwa juhudi zake. Aende atachukua kiulaiiiini.
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,702
  Trophy Points: 280
  weeee weeeee mwambie akome kabisa huku kawe tunampa mdee
   
 13. GP

  GP JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahahaaaaaa,
  mpwa naona SEMINA zinafanya kazi haswa kwenye signature!.

   
 14. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Asha Baraka ni huyu mwanadada katikati anayeongea na simu. Link hii
  [​IMG]
   
 15. D

  Dalilah Member

  #15
  Nov 26, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Mamaa wa kusugua kisigino, jamani huo ubunge ni mchezo tu?? Ataongea nini anachokijua cha busara, huyu Asha Baraka?? Kwao hathubutu maana wazee wa ujiji walimtolea radhi alipoenda na wanenguaji wa Twanga, wakamwaga mauno nusu uchi ilikuwa sooo la nguvu!! Aendelee tu na Mugongo Mugongo
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Chagueni wapinzani wawaletee maendeleo hawa mnao wakumbatia wanawaumiza tu.
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Soon utasikia mengi nae huyooooooooooo
   
 18. R

  Ronaldinho Member

  #18
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda ataanzisha chuo cha unenguaji,kwa kuwa ni CCM wadanganyika watampa kura tu bila kujali uwezo wake
   
 19. M

  Mundu JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Acheni agombee, mbona mzee wa TOT naye mbunge... Ubunge si ni kupokezana vijiti tu? kwani waliopo wamefanya nini, si afadhali Asha ana track record ya kusimamia bendi inayofanya kazi vizuri kwa zaidi ya muongo mmoja?

  nani kati yenu hajawahi kuimba hivi "twanga pepeta ninavyoipenda nitakunywa sumu juu yake..."
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  maana yke inaelekea wanaujua mchezo wanaocheza
   
Loading...