Asanteni wana JF, nilipita na kupatwa Sinza

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,125
8,627
Niliamua kukaa siku mbili bila kibali cha Makonda Dar es Salaam. Nilifanya vile kwani nilikokuwa nimezamia nilikutana na Wabongo kibao wengine wakaniomba nifikishe zawadi ana kwa ana kwa ndugu zao pia niliona bora nipite mitaa ya narung'ombe kwani ndiyo mitaa nilipoanza kiduka cha vifaa vya umeme mzigo wa kwanza nilichukulia mitaa hiyo. Siku ya kwanza ya mapumziko niliamua kuwatafuta marafiki zangu wa FB walioko Dar na nilikutana na wawili na nashukru walikuwa wadada wema na wanaojiheshimu. Baadae niliamua kukabidhi dhawadi nilizopewa huko ng'ambo ndipo kati ya hao watu aliniambia nimsubiri Sinza. Nilisubiri baadae niliamua kwenda kwenye ofisi za ACACIA kumuona ngosha mwezangu ambaye aliniomba nisikose kumuona kabla ya kwenda Usukumani. Nilionana nae ofisini kwake karibia na sheli ya mafuta iitwayo Victoria na baadae nikarudi Sinza na kumsubiri mwenyeji wangu nimkabidhi zawadi zake then nisonge Mwanza. Basi nikiwa hapo nikamuuliza dreva tax ni wapi tapata chakula kizuri hasa ugali, akaniambia ni hapo Sinza Makaburini sehemu inaitwa Fast Food. walikuja polisi watatu na kati ya hao mmoja nilimfahamu kwani alikuwa mpakani Mtukula na nilimfahamu kipindi naenda kufuata vipodozi Kampala ndipo nikawaambia waagize chakula nilipe!! Jamani bill ilipoletwa nilitamani kupitia mlango wa chooni. Niliuliza pembeni mbali na hao maafande ili wasisikie kulikoni hii bill imekuwa kubwa hivi wakati chakula nichakawaida tu(80,000/=)? Wakanijibu ni bei ya kuku mzima wa kienyeji na vingine!! Ukweli ni kwamba walileta kuku nusu na nikawauliza kama kuku ni yote leteni hapa firigisi mhudumu akasema firigisi huwa zinabaki machinjioni!! Kweli kupatwa si kwa jua tu hata kwa binadamu pia.
1474116407607.png
1474116581525.jpg
 
wa mikoani hamuwezi kuishi dar ona unalialia wakati hiyo hela ni ndogo sana
 
wa mikoani hamuwezi kuishi dar ona unalialia wakati hiyo hela ni ndogo sana
Ni kweli ndugu ila wangenipatia bei kabla ya kuniingiza chaka vile. Natokea mkoani japo nilipita nikitokea ng'ambo kidogo ya nchi brother
 
Watu wanne mlikuka mbona kama Fea tu ungeenda ile restaurant inayozunguka yenyewe AKEMI Gorden jubilee Tower nadhani ungetafutiwa watu wakudhamini...pale quality plaza tulikula African food ugali sembe na fish plus juice1 na soda tonic watu wanne ilitucost 89 wakenya walitamani kulia machozi... Na hapo walikimbia happy hours The chef pride ya 2,500 kisa watu wengi nikawarush huko walijuta
 
Watu wanne mlikuka mbona kama Fair ungeenda ile restaurant inayozunguka yenyewe AKEMI Gorden jubilee Tower nadhani ungetafutiwa watu wakudhamini...
Tatizo nilistukizwa kisaikolojia ndugu harafu firigisi hakuna
 
Break point ya kijitonyama wahudumu walikuwa wanawapiga sana wateja hasa wakiona mteja amezungukwa na wasichana
 
Pole sana Ng'wanapagi Dah umenikumbusha hapo fast food kitambo sana, niliwahi kukaa na shemeji yenu, nikaagiza kuku nusu ili tushee naye. dah jamaa kaleta amekatakata kabisa, sasa sisi wengine tumetoka bara nikamwambia shemeji yenu hebu ngoja nikuoneshe maajabu ya hapa, nikaanza kumuunga yule kuku nusu hahaha dah kipande flani hivi kikubwa kikakosekana, nikamwita mhudumu lete hiki cha hapa, ooh huyo kuku yuko hivo hivo, ebana nilizua balaa mpaka meneja akaja nikamwambia hii tabia naiona sana hapa, sio kwa kuwa nimekaa na mtoto mrembo hapa mkahisi ntauchuna, leteni kipande cha hapa, nikaona wateja wenzangu nao wanaangalia kuku zao. Daslam noma. Hujiulizi wapishi wengi mahotelini wananenepa tu?
 
Back
Top Bottom