Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Najitokeza asubuhi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wabunge wote wa CCM(wakiwemo pia Mawaziri,Manaibu Mawaziri,Spika,Naibu Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali).Mnafanya kazi ya 'kutukuka'.
Mnauonesha umma wa Tanzania jinsi ulivyofanya makosa kuwachagua kwa wingi wenu katika uchaguzi Mkuu wa 2010 na kupelekea wengine kuteuliwa au kuchaguliwa katika vyeo mlivyonavyo. Mnafanya kazi ya kudharau,kukejeli,kuzomea na kuharibu hoja yoyote ya Mbunge yeyote wa upinzani kwa maslahi hasa ya chama kuliko hata ya watanzania. Mnastahili sifa!
Mpo mnaoongoza kuomba miongozo ya kukandamiza hoja au kauli za wapinzani-hasa Mheshimiwa William Lukuvi,kwa kulinda Serikali na chama. Mnatekeleza kimatendo tulichowachagulia kwacho:ni kuhakikisha kuwa wapinzani hawafurukuti na CCM inatamba iwezavyo Bungeni huku TBC1 na/au Stae TV ikiwaonesha moja kwa moja. Raha ilioje!
Kuongea kwenu ni rahisi sana.Kila mnachosema hasa kinachosambaratisha hoja ya wapinzani hupigiwa meza na makofi mengi kwa kushangilia 'pointi' mnazozungumza. Chama kwanza,wananchi baadaye!
Ipo siku baadhi yenu au wote mtakuwa watazamaji wa Bunge kama sisi-tena si mbali ni 2015. Mtaona jinsi Bunge linavyopaswa kuwa. Msisahau kujikumbusha 'clips' zenu hizi ili mlinganishe na hilo Bunge jipya. Msisahau!
Hivi ni kweli kuwa tumewachagua nyinyi Wabunge kwa mamia kwenda Bungeni kufanya hivi? Mwigulu Nchemba alipoichana hadharani Bajeti Mbadala ya Upinzani iliyowasilishwa na Zitto Z. Kabwe,nyinyi mlishangilia sana. Juzi,Tundu A.M.Lissu aliipinga hoja binafsi ya Hamis Kigwangalla,tena kwa maneno matupu,ikawa nongwa.
Kigwangalla akatafutiwa nafasi ya kujibu mapigo. Muda wake wa kujibu hoja za Wabunge juu ya hoja yake akautumia kumshambulia moja kwa moja Tundu Lissu huku akisindikizwa na makofi na vigeregere.
Ipo siku mtajua kuwa hakuna katika nchi hii mwenye Jimbo wala cheo cha kudumu-si mbali,ni 2015. Mtajua kuwa hata asiye na pesa aweza kuwa Mbunge na kuboresha zaidi hoja zake kuliko nyinyi wenye pesa mnavyofanya. Mtajua kuwa sasa watanzania wanafuatilia kwa makini Wabunge wao na hoja zao. Mtafikia kuzilaumu luninga zinazowaonesha 'live' sasa. Siku inakuja!
Itafikia wakati,tena ni 2015, ambapo watanzania hawatajali fedha,vitisho,uzoefu,propaganda wala nini sijui ila uongozi imara kwa maendeleo ya Taifa hili. Hawatachagua tena wapiga makofi ila wajenga hoja.
Mna heri Wabunge wa CCM kwa kuturahisishia kazi ya kuchagua vyema 2015!