Asanteni sana Wabunge wa CCM!

Asanteni sana Wabunge wa CCM!

Wamevimbiwa posho hao 2015 inakuja watakiona cha moto

kaka waache waendelee na upuuzi wao,Hawafanyi hivyo kwa kupenda bali Mungu ameamua kuwafunua mbele ya watanzania.Kwa sasa wako uchi wa mnyama.
 
kila jambo lina Mwisho! Job Ndugai ubabe unaofanya una mwisho na utasimama mbele za haki kujibu ulivyolitendea taifa hili kwa kukandamiza wabunge waliokuwa na mapenzi ya dhati kwa nchi yao,na wewe ukitaka kujionyesha kuwa unaweza kufanya lolote ulitakalo jitukuze tu sasa bwana mkubwa.
 
Ccm wanajivunia rushwa ya chumvi, kanga na vikofia vya kijani wakati wa uchaguzi!! Si ajabu kwamba watanzania wakairudisha madarakani tena ccm pamoja na uozo wote huo!!! Bado tuna safari ndefu!!!!!!

Mkuu Watanzania ni Mimi wewe na wao sasa mimi na wewe kama tumeliona hili tuanze kupigania hawa hawatushindi na mwaka huo kwa uwezo wa mungu watatuua maana na walivyowepesi wa kuiba kula na makada wao ma RC na MDC ambao wanajua fika piga geuza CDM ikichukua nchi hawana chao. Ndugu zangu watanzania shime alaykum tupigane tuwatoe watu wanaotuhadaa wenyewe wanadhani kupiga kelele Bungeni wanapata massive support la hasha wanazidi kujenga chuki ka Watz. Wasitegemee jimbo la Ubungo na Mengine ya DCM kama watayapata tena. Wajiandae kuwa watizamaji
 
kaka waache waendelee na upuuzi wao,Hawafanyi hivyo kwa kupenda bali Mungu ameamua kuwafunua mbele ya watanzania.Kwa sasa wako uchi wa mnyama.

Uzuri wanatengeneza njia ya kumng'oa mkoloni mweusi bila ya wao kujua watakapo kuja kushtuka tayari wamesha tupwa nje
 
Mwalimu angekuwepo asingekubali upuuzi huu, ila kwa kuwa hayupo ni sawa na watoto yatima katika nchi yao - nani wa kukemea - watu wanaongoza kikao cha bunge kama kikao cha harusi -- shame. Mbunge wa CCM anaweza kusema lolote na asichukuliwe hatua, wa upinzani ataambiwa athibitishe na hata akifanya hivyo uthibitisho unawekwa kapunu -- Lema alisema waziri mkuu ni muongo mbona utetezi wa kauli yake umefichwa. Mtatungaje sheria bila kutenda haki? ndiko tunakoipeleka Tanzania yetu.
 
Hila, ghiliba, kiburi, ulimbukeni vinavyooneshwa na LUkuvi, Ndugai, Bi Kiroboto Original VINAKERA na Watanzania tumeona tumesikia... Ngoma inogile wananchi tumeamka sasa NA vita hivi tumevigeuza kuwa personnal..
 
binafsi jana nilifurahi sana,sana.Yule jamaa ana upara kama uwanja wa mkutano wa wachawi hamna kitu kichwani.Yuko kama jina lake,Jobu yaani Kibarua.Ni kibarua wa magamba
 
Ni kweli,hakukuwa na haja ya kuondoa hoja ya mbunge kama kweli wanajiamini kwamba wanafanya kazi as per ilani ya CCM,nilidhani hapa ndo walipotakiwa kueleza bayana jinsi wanavyosaidia kuondoa tatizo la maji Dar ambalo limekuwa sugu for almost 51 years,sasa kuiondoa inamaana wajanja wameshapiga hela hapo,du R.I.P TZ under CCM
 
Tumewakosea nini ccm,hamna hata huruma!
 
Mwanazuoni mmoja katika maendeleo ya kimataifa (international development) ameandika kitabu kinaitwa: Kicking Off The Ladder (kwa tafsiri isiyo rasmi... Kupiga Teke Ngazi). Kitabu hicho kinaeleza namna nchi za Magharibi zinavyotumia kila aina ya mbinu kupitia 'misaada' kuhakikisha kuwa nchi maskini haziendelei.

Mnyukano unaondelea sasa bungeni unaakisi maudhui ya kitabu hiki kwa muktadha wa Tanzania ya sasa. Wabunge wengi wa sisiemu na viongozi wa serikali baada ya 'kufanikiwa kupanda' wanachofanya sasa ni 'kupiga teke ngazi' ili wengine wasipande. Kibaya zaidi kwao hapo 'juu' walipo panawaka moto na huku chini hawawezi kurudi maana 'ngazi' waliyotumia kupandia walishaipiga teke.

Ukiona au kusikia mbunge, waziri au kiongozi wa chama tawala anazomewa au kupopolewa mawe na wananchi ujue watu wamemchoka na hawataki kumwona tena huku chini. Ukiona au kusikia mbunge anachomewa nyumba na hao hao waliompigia kura na kushangilia ushindi wake wa kishindo, kimbunga au upepo wa kisulili, ujue hapo juu alipo panaungua na sasa hana namna ya kushuka chini tena. Ukiona au kusikia naibu waziri anaenda mahali kwa kujificha tena kwa kuvalishwa magwanda, ujue sasa huyo sio kiongozi au mtawala wa watu tena, anatamani kushuka chini lakini ashukeje maana alishiriki kupiga teke ngazi aliyotumia kupanda.

Ushauri wangu bure kwa wabunge na viongozi wa sisiemu, rudisheni 'ngazi' mliyotumia kupandia, mshuke taratibu nasi tutawasamehe makosa yenu na kuwapokea uraiani kama wananchi maana kazi ya kuongoza nchi imewashinda. Kuendelea kung'ang'ania hapo juu ni gharama zaidi maana mnazidi kujenga hasira na chuki dhidi yenu mlio kundi dogo sana na mamilioni ya watanzania waliowafikisha hapo. Asomaye na afahamu!
 
Nimekuelewa sana mkuu, na naamini kwa hili lililotokea bungeni jana wana Dar es Salaam watakuwa wakosefu wa kwenda ahera kama watawachagua tena hawa vichwa maji.:A S angry::confused2:

Wazungu wanasema hivyo VIOJA wanavyofanya CCM kwa Watanzania IS A BLESSING IN DISGUISE.
Sisi waswahili tunasema kwamba SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA. Hata uwaambie vipi CCM ni sikio la KUFA.

Nitashangaa sana kama CCM itapata MBUNGE hata MOJA Dar es Salaam kutokana na kuzima hii KERO kubwa ya Maji tunayoipata sisi wakaazi wa Dar es salaam. Au Kama CCM itapa MBUNGE hata moja Mtwara kutoka na kutaka kupoka raslimali ya gesi ya Mtwara bila kuwanufaisha wana WanaMtwara.

But gosh, give me a break, Tanzanians have very short memory and CCM knows this very well. 2015 WanaDar es Salaam na Mtwara watakuwa wamesahau haya madhila yote ya CCM, hasa watakapopewa vitenge, kofia, T-shirts, chumvi, sabuni na kusindikizwa na ahadi hewa.

Ukombozi wa kweli wa nchi uko kwenye ELIMU, bila elimu ya URAIA we are doomed. Wana Dar es Salaam ndiyo tunawaangusha Watanzania. Soma historia za nchi mbalimbali chachu za mabadiliko kiini chake huwa ni CAPITAL CITY. Lakini Dar es Salaam Capital City ya Bongo ambapo >90% wako informed na UBAYA WA CCM, sisi ndiyo kwanza tunachagua WABUNGE wa CCM na kumumpatia kura za kishindo mgombea urais wa CCM. Believe me kama Capital City ya Tanzania ingekuwa aidha Mbeya, Arusha au Mwanza, there is no question about that CCM 2015 ingezikwa tena BAHARINI kama Osama Bin Laiden!
 
Najitokeza asubuhi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wabunge wote wa CCM(wakiwemo pia Mawaziri,Manaibu Mawaziri,Spika,Naibu Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali).Mnafanya kazi ya 'kutukuka'.

Mnauonesha umma wa Tanzania jinsi ulivyofanya makosa kuwachagua kwa wingi wenu katika uchaguzi Mkuu wa 2010 na kupelekea wengine kuteuliwa au kuchaguliwa katika vyeo mlivyonavyo. Mnafanya kazi ya kudharau,kukejeli,kuzomea na kuharibu hoja yoyote ya Mbunge yeyote wa upinzani kwa maslahi hasa ya chama kuliko hata ya watanzania. Mnastahili sifa!

Mpo mnaoongoza kuomba miongozo ya kukandamiza hoja au kauli za wapinzani-hasa Mheshimiwa William Lukuvi,kwa kulinda Serikali na chama. Mnatekeleza kimatendo tulichowachagulia kwacho:ni kuhakikisha kuwa wapinzani hawafurukuti na CCM inatamba iwezavyo Bungeni huku TBC1 na/au Stae TV ikiwaonesha moja kwa moja. Raha ilioje!

Kuongea kwenu ni rahisi sana.Kila mnachosema hasa kinachosambaratisha hoja ya wapinzani hupigiwa meza na makofi mengi kwa kushangilia 'pointi' mnazozungumza. Chama kwanza,wananchi baadaye!

Ipo siku baadhi yenu au wote mtakuwa watazamaji wa Bunge kama sisi-tena si mbali ni 2015. Mtaona jinsi Bunge linavyopaswa kuwa. Msisahau kujikumbusha 'clips' zenu hizi ili mlinganishe na hilo Bunge jipya. Msisahau!

Hivi ni kweli kuwa tumewachagua nyinyi Wabunge kwa mamia kwenda Bungeni kufanya hivi? Mwigulu Nchemba alipoichana hadharani Bajeti Mbadala ya Upinzani iliyowasilishwa na Zitto Z. Kabwe,nyinyi mlishangilia sana. Juzi,Tundu A.M.Lissu aliipinga hoja binafsi ya Hamis Kigwangalla,tena kwa maneno matupu,ikawa nongwa.

Kigwangalla akatafutiwa nafasi ya kujibu mapigo. Muda wake wa kujibu hoja za Wabunge juu ya hoja yake akautumia kumshambulia moja kwa moja Tundu Lissu huku akisindikizwa na makofi na vigeregere.

Ipo siku mtajua kuwa hakuna katika nchi hii mwenye Jimbo wala cheo cha kudumu-si mbali,ni 2015. Mtajua kuwa hata asiye na pesa aweza kuwa Mbunge na kuboresha zaidi hoja zake kuliko nyinyi wenye pesa mnavyofanya. Mtajua kuwa sasa watanzania wanafuatilia kwa makini Wabunge wao na hoja zao. Mtafikia kuzilaumu luninga zinazowaonesha 'live' sasa. Siku inakuja!

Itafikia wakati,tena ni 2015, ambapo watanzania hawatajali fedha,vitisho,uzoefu,propaganda wala nini sijui ila uongozi imara kwa maendeleo ya Taifa hili. Hawatachagua tena wapiga makofi ila wajenga hoja.

Mna heri Wabunge wa CCM kwa kuturahisishia kazi ya kuchagua vyema 2015!

Roho inapotaka kuacha mwili huwa na tabia kama hizi..... Sasa hivi CCM ipo katika mporomoko ndio maana kelele ni nyingi kupita maelezo. CCM imeshakuwa kama chama cha upinzani wakati bado imeshika rungu la dola.... CCM jipangane aina ya mazishi mnayotaka na sio kupiga kelele kama watoto wa shule wasio na mwongozo.

Najitokeza asubuhi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wabunge wote wa CCM(wakiwemo pia Mawaziri,Manaibu Mawaziri,Spika,Naibu Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali).Mnafanya kazi ya 'kutukuka'.

Mnauonesha umma wa Tanzania jinsi ulivyofanya makosa kuwachagua kwa wingi wenu katika uchaguzi Mkuu wa 2010 na kupelekea wengine kuteuliwa au kuchaguliwa katika vyeo mlivyonavyo. Mnafanya kazi ya kudharau,kukejeli,kuzomea na kuharibu hoja yoyote ya Mbunge yeyote wa upinzani kwa maslahi hasa ya chama kuliko hata ya watanzania. Mnastahili sifa!

Mpo mnaoongoza kuomba miongozo ya kukandamiza hoja au kauli za wapinzani-hasa Mheshimiwa William Lukuvi,kwa kulinda Serikali na chama. Mnatekeleza kimatendo tulichowachagulia kwacho:ni kuhakikisha kuwa wapinzani hawafurukuti na CCM inatamba iwezavyo Bungeni huku TBC1 na/au Stae TV ikiwaonesha moja kwa moja. Raha ilioje!

Kuongea kwenu ni rahisi sana.Kila mnachosema hasa kinachosambaratisha hoja ya wapinzani hupigiwa meza na makofi mengi kwa kushangilia 'pointi' mnazozungumza. Chama kwanza,wananchi baadaye!

Ipo siku baadhi yenu au wote mtakuwa watazamaji wa Bunge kama sisi-tena si mbali ni 2015. Mtaona jinsi Bunge linavyopaswa kuwa. Msisahau kujikumbusha 'clips' zenu hizi ili mlinganishe na hilo Bunge jipya. Msisahau!

Hivi ni kweli kuwa tumewachagua nyinyi Wabunge kwa mamia kwenda Bungeni kufanya hivi? Mwigulu Nchemba alipoichana hadharani Bajeti Mbadala ya Upinzani iliyowasilishwa na Zitto Z. Kabwe,nyinyi mlishangilia sana. Juzi,Tundu A.M.Lissu aliipinga hoja binafsi ya Hamis Kigwangalla,tena kwa maneno matupu,ikawa nongwa.

Kigwangalla akatafutiwa nafasi ya kujibu mapigo. Muda wake wa kujibu hoja za Wabunge juu ya hoja yake akautumia kumshambulia moja kwa moja Tundu Lissu huku akisindikizwa na makofi na vigeregere.

Ipo siku mtajua kuwa hakuna katika nchi hii mwenye Jimbo wala cheo cha kudumu-si mbali,ni 2015. Mtajua kuwa hata asiye na pesa aweza kuwa Mbunge na kuboresha zaidi hoja zake kuliko nyinyi wenye pesa mnavyofanya. Mtajua kuwa sasa watanzania wanafuatilia kwa makini Wabunge wao na hoja zao. Mtafikia kuzilaumu luninga zinazowaonesha 'live' sasa. Siku inakuja!

Itafikia wakati,tena ni 2015, ambapo watanzania hawatajali fedha,vitisho,uzoefu,propaganda wala nini sijui ila uongozi imara kwa maendeleo ya Taifa hili. Hawatachagua tena wapiga makofi ila wajenga hoja.

Mna heri Wabunge wa CCM kwa kuturahisishia kazi ya kuchagua vyema 2015!

amani iwe nao katika kutekeleza huo uovu wao.
 
......Natamani sana uchaguzi mkuu ufanyike Kesho... tuone yatakayotokea.. viongozi walioko madarakani wanafanya jinsi wapendavyo, maana wao wameshiba, hawana shida yoyote katika kusomesha watoto wao matibabu na maisha kwa ujumla...lakini mtanzania wa kawaida bado anateseka na kula mlo mmoja wa shida kwa siku...TENA MTANZANIA ANAKULA KULA USHIBE SIO LISHE KAMILI.... maisha yanazidi kuwa magumu, huduma za kijamii za kila siku zinatishia maisha ya mtanzania wa kawaida.... watu wanakuosa maji .. mijini maji yakitoka leo mpaka wiki mbili au tatu kama Dar.. wananunua maji ya kunywa ndoo 500/= na zaidi... nyama inaliwa kwa machale machale .. samaki ndo usiseme kabisa... dagaa ni anasa.. maharage ndo balaaa...mchele, unga, sukari bei zake hazieleweki eleweki... wao wako kwenye viyoyozi kuanzia magari yao, maofisi yao mpaka majumbani mwao... wanatia aibu wanafananishwa na wwatu wanaokula bila kunawa...... EEEeeeeeeeeeeeeee Mwenyezi MUNGU .... Tusaidie
 
Back
Top Bottom