Asanteni sana POLISI


VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,989
Points
2,000
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,989 2,000
Zamani kidogo(wakati ndio naanza kujua jema na baya),Wanasheria hususani Mawakili walisifika kwa sifa nyingi zisizovutia. Walionekana waongo,wezi,wauaji,watetezi wa wakosaji na kadhalika. Si kwamba sifa hizi ndizo zilizonivutia hadi nami kuwa Wakili...la hasha! Niliingia fani hii nikiamini kuwa watatokea watu watakaotupokea sifa hizo. Tumewapata.Ni Polisi wa Tanzania.

Polisi ni wauaji;polisi ni waongo(wakioongozwa na mwanafunzi wangu wa intelijensia Kova);polisi ni wezi;polisi ni watetezi wa wakosaji(hasa wenye mali na fedha). Angalau sasa Mawakili Wasomi tunapumua kidogo. Tunatafutiwa sifa mpya nyinginezo.Kwasasa tupo likizo ya dhihaka,kejeli na sifa mbaya.

Asanteni sana Polisi.Mmetusaidia sana.Msengwile!(tunawashukuru-kingoni)
 

Forum statistics

Threads 1,295,850
Members 498,410
Posts 31,225,356
Top