Celine Joseph
Member
- Dec 12, 2014
- 6
- 6
NJOMBE, MBINGA ASANTE NGELEJA KWA KUTUTOA GIZANI
Juzi wakati wawakilishi wa gazeti letu walipotembelea maeneo ya Njombe na Mbinga wakihoji kuhusu namna umeme ulivyovifikia vijiji vingi katika maeneo hayo walikutana na maneno mengi sana lakini mengi yalikuwa na maneno ya shukrani kwa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini mh.Willium Mganga Ngeleja, watu hawa walio wengi kwa idadi walisikika wakisema maneno " ASANTE NGELEJA KWA KUTUJALI, ISINGEKUWA WEWE LEO TUNGEKUWA GIZANI" kauli hii ilinishangaza sana na ilinibidi kuwahoji kwanini hasa wanamtaja Ngeleja kama wakushukuriwa na si Mh.Rais au hata Waziri wa Nishati na Madini wa sasa.
Wakazi hawa wa Njombe na Mbinga walisema kama sio Ngeleja na ubunifu wake leo hii tungekuwa gizani, wakaendelea yaani kama sio umeme wa wakala wa umeme vijijini REA, kitu ambacho Ngeleja alikianzisha kama mkombozi wa sisi watu tuishio vijijini leo tungekuwa gizani na hata nyuma kimaendeleo. " Tunamshukuru sana Ngeleja kwa kuianzisha REA na kuhakikisha sisi huku kijijini tunapata umeme kwa ajili ya maendeleo zaidi".
Wananchi hawa wa Mbinga na Njombe waliendelea kusema kuwa viongozi wengi wamekuwa na upendeleo kwa maeneo wanapotoka hasa wanapopata nyadhifa kubwa kama aliyokuwa nayo Ngeleja lakini kwa huyu baba wa watu Ngeleja ni tofauti kabisa yaani ameacha huko kwao usukumani akatukumbuka wahehe na wabena na sisi wangoni pamoja na Wamatengo na hata ndugu zetu kule Nyasa, huyu ni mtu wa watu anajali sana watu na ana huruma sana kwani anatambua utu wa watu ni kiongozi mzuri sana hana upendeleo yaani huyu ni tofauti kabisa.
Wakazi hawa wa Mbinga na Njombe waliendelea kulalmika na kuonesha kusononeka sana kwani wanadai hawakufurahishwa na kitendo cha maneno watu waliyokuwa wanamrushia na kumpakazia enzi za uongozi wake mpaka kumpelekea kujiuzulu mwaka 2012 mwezi May, wanadai kujiuzulu kwa Ngeleja kulikwamisha mambo mengi sana ikiwemo mipango mingi iliyokuwa mezani kwa ajili ya kuhakikisha vijiji vingi nchini vinapata umeme na kuvihakikishia maendeleo katika nyanja tofauti tofauti.
Wanaendelea kusema kuwa sisi umeme tuliletewa na tuliunganisha kwa bei rahisi sana yaan elfu 27 tuu, zamani ilikuwa mpaka laki saba lakini yule Msukuma wa watu akapambana mpaka ikashuka kiasi hicho eti bado watu wanasema hajui kuongoza sijui wanataka wafanyiwe nini ili waone mtu anafanya kazi, wanadai kama sio Ngeleja maisha yao kule vijijini yangekuwa ya giza sana na kusingekuwa na maendeleo kamwe.
Wanadai kuwa si huyu huyu Ngeleja aliepambana kuhakikisha swala la mgawo wa umeme nchini linapungua, au watu wamesahau kuwa Ngeleja ndiye aliyebuni mradi wa kuiunganisha mikoa yote ya Tanzania kwenye grid ya taifa kupitia miradi ya North-West Grid (kutokea Shinyanga,Geita,Kigoma,Katavi, Rukwa hadi Mbeya), Makambako-Songea na ule wa kuimarisha huduma ya umeme kupitia North-East Grid (kutokea Dares salaam hadi Kilimanjaro). lakini bado watu wanasema sio kiongozi mzuri walitaka awabebe mgongoni.. Kijana wa watu anafanya kazi kubwa sana na alitusaidia na daima tutashirikiana nae na kumkumbuka kwa safari yoyote atakayoianzisha.
Niliendelea kuwahoji na niliwadokeza kuwa kuna tetesi kuwa Ngeleja atagombea uraisi mwakani yaan hapa mpaka vilugha vyao vilizungumzwa waliaikika wahehe wakisema " Uwii, Inguluvi imlete munu huyu, tuisakumunu huyu ache kwa wewe" wakimaanisha "Mungu amlete mtu huyu,tunamuhitaji kwa ukombozi wetu" maneno haya yaliambatana na furaha kubwa iloyonishtua sana kwani sikitegemea wangelipokea swala hilo kwa furaha na shangwe kubwa wanasema watampitisha kwa hali na mali ili aendelee kuwatetea wao na watanzania kwa ujumla.
Walisema kwa walio tangaza nia mpaka sasa hakuna anayefaa kuwa raisi labda kama Ngeleja akigombea kama ndugu mwandishi ulivyotudokeza hapo, walilaumu kuwa mbona kama anataka kugombea uraisi yupo kimya mpaka sasa ? Mimi nilikosa cha kuwajibu na niliwaambia sijui anatafakari nini lakini nadhani kugombea uraisi ni moja ya fikra kubwa alizo nazo, waliomba kutembelewa na Mh. Ngeleja na mimi bila hajizi kwa sababu ya kazi yangu ya uandishi namba za viongozi huwa ninazo niliitafuta ilipokuwa namba ya Ngeleja na nilimpigia nikamwambia kuhusu kuwatembelea watu wa Njombe na Mbinga na yeye aliitika na kuwaahidi kuwa atapanga siku akawatembelee wazungumze vizuri na kujua wanaendeleaje, watu hawa walifarijika sana na kuendelea kuwa na imani kubwa na mh.Ngeleja na wamesema wanamuandalia zawadi kubwa mnoo kama shukrani...
Tunashukuru ndg mwandishi kwa kututembelea na Mungu akubariki sana popote ulipo, Mungu ibariki Njombe na Mbinga, Mungu ibariki Tanzania.A