Asante sana Ngeleja

Asante sana Ngeleja

Utendaji Wa Ngeleja ktk wizara ngumu ya nishati na madini ndiyo unanifanya nimuone huyu mtu anaweza. Oohoo mwizi leta ushahidi hapa sio porojo .
 
Mtoa mada unajikakamua kuandika hata vyakuandika huvipati' hata kama ngeleja mjomba usikubali kujizalilisha kuandika upuuzi' tafuta hela kwa njia nyingine
 
shida ya vijana Wa Leo ni kuongozwa na hisia tu. jenga hoja zenye maana tujue kwann asiwe ngeleja na awe huyo unaempenda. Watu wanaweka facts za utendaji Wa ngeleja na nyinyi wekeni za hao mnao waamini basi tupime.
 
NGELEJA ndiye kiongozi atakayeweza kututoa tanzania kutoka sehem moja had nyngn...legacy alizoacha katika wzara ya nishati na madini...ndiyo sababu inayonfanya mm niamn kua anaweza na anastahili.....Twende na Ngeleja 2015
 
Ngoja nikuuulize wewe mpambe wa Escrow, kama Ngeleja ni jembe kwani aliachishwa nafasi hizo za uwaziri? kuna wengine wamekuwa wakibadilishwa nafasi za uwaziri na sii kufukuzwa, kwanini Ngeleja amefukuzwa moja kwa moja? ni mdhahifu, ni mwizi, na hata udhibitisho mwingine ni kwamba kwenye ripoti ya escrow, ni mtuhumiwa. Kamwe huyo Ngeleja sidhani kama atafaa hata kuwa mbunge.
 
Najua haumjui Ngeleja that's y..pata kumjua kidogo

WASIFU WA MHESHIMIWA WILLIUM MGANGA NGELEJA (THE CURRICULUM VITAE)

Particulars/ Husishi/Moja moja
Jina: WILLIUM
Jina la kati: MGANGA
Jina la mwisho/ukoo: NGELEJA
Tarehe kuzaliwa: 05/10/1967
Wasifu wa ndoa: AMEOA
Anuani: SLP 2000 DAR ES SALAAM
Simu ya kazi: 0754710070

Taaluma yake
2001-2002: CERTIFICATE YA SHERIA YA MAWASILIANO YA MITANDAO YA SIMU WITWATERSRAND UNIVERSITY SOUTH AFRICA
1996-1999: MASTERS IN LAW (LLM)UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
1991-1994: LLB UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
1987-1989: A-LEVEL IHUNGO HIGH SCHOOL
1983-1986: O-LEVEL MPWAPWA SECONDARY SCHOOL
1976-1982: PRIMARY EDUCATION(ELIMU YA MSINGI) BITOTO PRIMARY SCHOOL

Historia ya kazi
2005-2015: MBUNGE BUNGE LA TANZANIA (JIMBO LA SENGEREMA)
1/12/2007-08/02/2008: NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI
Feb 2008-May 2012: WAZIRI NISHATI NA MADINI
2000-2005: MWANASHERIA MKUU VODACOM TANZANIA
1995-2000: MWANASHERIA MKUU PRICE WATERHOUSE COOPERS COMPANY
1994-1995: OFISI YA MWANASHERIA MKUU KWA AJILI YA MAFUNZO YA SHERIA YA NCHI NA UTUMIZI SAMBAMBA NA USIMAMIZI WAKE

Wasifu kisiasa ndani ya chama (CCM)
1980-1981: MWENYEKITI WA VIJANA SHULE YA MSINGI BITOTO
2012-2017: MJUMBE HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

Na huo ndioo wasifu wa mheshimiwa Ngeleja...

ndugu utakuwa umekosea kidogo katika anuani; badala ya Anuani: SLP 2000 DAR ES SALAAM
nadhani ni Anuani: SLP 2000 SENGEREMA au sio?
 
Hayo ni majukumu ya serikali kuhakikisha kila mtanzania anapata hiyo huduma,na ndiomaana wanakusanya kodi kwa hiyo huhitaji kushukuru katika hilo...
 
Kiukweli hata mi namkubali huyu dogo Ngeleja. Jamaa ana uwezo wa kazi balaa,we fikiria lile liwizara ambalo ni kama wizara mbili kamili alikuwa analiendesha na Naibu Moja tu,pia Katibu Mkuu alikuwa 1 tu. Tangu alipotoka ilibidi Muhongo akabidhiwe Naibu Mawaziri wawili, Katibu Mkuu naye akaongezewa Naibu Katibu Mkuu.

Ngeleja alikabidhiwa wizara Feb 2008,ingawa Kabla ya hapo alikuwa Naibu kuanzia January 2007.

Kumbukeni Ngeleja alikabidhiwa wizara ikiwa katika hali mbaya sana. Kwenye sekta ya nishati,Tanesco ndo ilikuwa imetoka kuondolewa kwenye orodha ya mashirika yaliyokuwa yamekusudiwa kubinafsishwa tangu mwaka 1997. Hii maana yake ni kwamba tangu Mwaka 1997 Serikali au sekta binafsi hazikufanya uwekezaji wowote wa maana. Miundombinu ya Tanesco iliishazidiwa sana ndiyo maana mgawo wa umeme ulikuwa hauepukiki kila maji yalipopungua kwenye dams au mitambo ilipoharibika hata Kosovo tu.

So Ngeleja alipoingia ndo kaanza kurekebisha mambo ikiwa ni pamoja sera,Sheria,miongozo na kuibua na kuanza kutekeleza miradi mbalimbali Kama mlivyoiainisha humu.

Kwa hivyo kiukweli kwa kigezo cha legacy hakuna anayeweza kulingana Na Ngeleja Kati ya wanaotajwa kugombea urais awe from CCM au UKAWA,anayebisha alete hapa sifa Na utetezi wa hao wengine.

Sisi kama wachambuzi tusiendekeze mapenzi binafsi kwenye issue ya urais. Moja ya sifa kwa nafasi ya urais ni legacy,cyo porojo tu eti za maono ya mbele, hiyo halitoshi,lazima kila mgombea atudhihirishie legacy yake so far.

Wote tunakumbuka wakati anaondolewa uwaziri Mei 2012, Ngeleja aliishafanikisha kudhibiti mgawo wa umeme tangu Nov 2011 kupitia ule Mpango Maalum wa Dharura wa kudhibiti mgawo wa umeme ulioidhinishwa na Bunge mwezi Agosti,2011 kwenye bajeti ya Mwaka 2011/12. So mgawo wa umeme ulikuwa umedhibitiwa miezi 7 Kabla Ngeleja hajaondolewa. Mpango huo ulioanzishwa Na Ngeleja bado unaendelea hadi Leo.

Pia ni muhimu kujikumbusha kwamba tangu Ngeleja aondoke Serikali imekuwa ruzuku kwa Tanesco kissing cha shilingi 2.4bn a day kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa mafuta ya mitambo ya kikoi. Ruzuku hii ndo iliyochangia national budget deficit for the last 2 yrs!

Lakini pia wakati Ngeleja anaondolewa hasara kwa Tanesco ilikuwa just shs 43bn,leo ni zaidi ya shilingi bn 467.

Nakadhalika n.k
 
Halafu kuna watu wanadanganyana humu kwamba eti escrow imemmaliza kisiasa,siyo kweli. Fuatilieni mtajua kwamba kwenye uchaguzi huu katika jimbo lake la Sengerema,Ngeleja kashinda kwa 82% vitongoji, wakati kwa vijiji kapata 85%. By any standard huu ni ushindi wa kishindo kwa siasa za sasa na hasa ukizingatia mahasimu wake wanavyopambana kumchafua.

Issue ya escrow tuiachieni kwa vyombo husika. Escrow ingekuwa issue kwa voters Kafulila,Sugu,Mbowe,Wenje au Kiwia wa Ilemela wasingeshindwa!

Ushindi wa Ngeleja katikati ya tuhuma ni kielelezo tosh a kwamba jamaa anakubalika. Kwa wagombea wa kanda ya ziwa hakuna anayemfikia,labda ibis hi tu!
 
Nnatabiri CCM ikimpitisha Ngeleja atapata ushindi wa kishindo ka walivyoshinda akina Zuma,Uhuru Kenyatta au hata Mzee wetu Ali H Mwinyi,katikati ya tuhuma na firms za kisiasa.

Kumbukeni Kanda ya ziwa tu yenyewe ambayo ndiyo ngome ya Ngeleja ndiyo kanda wezeshaji kwa kila mgombea urais nchi hii awe Anatoka CCM au UKAWA.
 
Huyu Ngeleja ni mzuri sana, yaani kama tukiendeleza chuki na siasa chafu,tutakuja kupoteza jembe hili,asante sana watu wa njombe na mbinga kwa kumuona kamanda wetu huyu, yuko vzur kabisa mi nimempitisha ndani ya nafsi yangu

Kupoteza jembe ndio nini. Kwani unadhani wote tunataka kulima?! Ngeleja mzuri kwako lakini siyo eti awesome rais wa Tanganyika, no way.
 
Ngoja nikuuulize wewe mpambe wa Escrow, kama Ngeleja ni jembe kwani aliachishwa nafasi hizo za uwaziri? kuna wengine wamekuwa wakibadilishwa nafasi za uwaziri na sii kufukuzwa, kwanini Ngeleja amefukuzwa moja kwa moja? ni mdhahifu, ni mwizi, na hata udhibitisho mwingine ni kwamba kwenye ripoti ya escrow, ni mtuhumiwa. Kamwe huyo Ngeleja sidhani kama atafaa hata kuwa mbunge.

Ubunge nachukua mimi...
 
hiki ni kituko inaonesha jinsi gani baadhi ya watz wasivyo jua nini maana ya serikali
 
Vijana wengi hapa wanaongozwa na mihemuko ya kisiasa kwa sababu tu wameshikwa upande fulani... Lakini tukiongelea facts ndo kama hizo alizoelezea Mgope na eengine kuhusu huyu kijana Ngeleja. Kama si ushabiki basi kila mtu anapopinga legacy ya Ngeleja basi na atuambie hapa yeye mtu anayemkubali ili tumjadili hapa hapa...
 
huna haja ya kuletewa mtu wa kumjadili kwa sababu wakati utajieleza wenyewe. Unavyowafikiria vijana kuwa ni wa mihemuko umekosea sana na utaendelea kukaa gizani. natafakari sana jinsi gani uliwachukulia watanzania mpaka ukaamua kumpendekeza Ngeleja. Au anatokea jimboni kwako? kama ni hivyo na akakudanganyia chipsi, pole na tafadhali fikiri kama kijana mtanzania mwenye uzalendo halisi wa nchi yako. kama hukwendaga JKT kidogo tafadhali nenda upate uzalendo na hakika viiizi izi hivi vya rasilimali ya nchi yetu havitasikika tena vikipendekezwa kuiongoza nchi hii. Mtu yeyote unayempendekeza mpendekeze wewe kama wewe na ujitahidi kwamba ukimleta kwa watanzania utakubalika kwa hoja nzito na nzuri.
 
Back
Top Bottom