TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 24,956
- 25,053
Pongenzi hizi ninazitoa kwako Mweshimiwa rais pamoja na timu yako yote huko serikalini.
Pongenzi hizi ni kwa ajili ya namna ulivyoweza kushughulikia. suala la kurejesha uaminifu kwenye Bandari zetu. Majirani zetu wa Rwanda, DRC ,na Zambia, wanafurahia uaminifu na uwajibikaji mzuri kwenye bandari zetu. Kwa watu wa magari wanasema siku hizi wakiagiza magari na kuyapitisha kwenye bandari zetu yanawafikia yakiwa vile vile kama walivyoyaagiza. Hakuna tena wizi wa redio, betri, Kapeti na vitu vingine.
Pia wanasema pia hawacheleweshwi tena kwenye kuchukua magari yao, ndani ya masaa si zaidi ya 36, tayari wanakuwa wameishapewa magari yao.
Baada ya kupata udhibitisho huu wa. uaminifu na utendaji mzuri Badarini nikaona nipitishie Pongenzi zangu hizi hapa jukwaani, ili watanzania wajue jinsi Majirani zetu wanavyovutiwa na utendaji wetu siku hizi. Utendaji mzuri wa Rais wetu na sifa anazopata ni zetu sote Watanzania. Hivyo tuna haki ya kufurahia sifa hizo.
Mungu endelea kuibariki Tanzania. Amen.