Asante Postmaster General kwa kunilipia fidia

DPN

Member
Sep 28, 2020
29
66
Nawasalimu Wana-JF wote; heri ya mwaka mpya 2021.

Mnamo tarehe 07/12/2020 niliandika malalamiko yangu hapa JF kuhusu mzigo wangu kupotelea Posta tangu tarehe 13/3/2020; ambapo hatua za kufuatilia mzigo huo hazikuzaa matunda, mpaka nikafikia hatua ya kuandika malalamiko hayo JF kwenye link hiyo hapo chini.

Namshukuru Postmaster General pamoja na timu yake yote kuanzia Posta Magu, Mwanza, Dar-es-Salaam, Songea na Mbinga; leo tarehe 04/1/2021 saa 10:30 jioni nimepokea kutoka kwa Postmaster Magu, fidia ya mzigo wangu uliopotea; asanteni sana.

Asanteni pia Wana-JF wote mliochangia andiko langu hapo chini; naamini kwamba michango yenu yote iliwasukuma na kuwahamasisha niliokuwa nikiwalalamikia waone haja ya kuondoa kadhia hiyo ambayo ilikuwa ni fedheha kwa shirika.

Naamini uongozi na watumishi wote wa Posta Tanzania watachukua tahadhari zaidi na wataimarisha mifumo ya usalama katika usafirishaji wa mizigo ya wateja, ili kadhia na fedheha za aina hii zisiwepo, hivyo kutujengea imani sisi wateja wao.

Asanteni sana; alamsiki.

 
Wajirekebishe sasa. Hivi hao waliozembea mpk mzigo kupotea wanawajibishwaje mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: DPN
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom