Usiposhukuru kwa kidogo basi hata ukipewa kikubwa huwezi kusema asante!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,530
Mchuzi wa umbwa hunywewa wa moto.. ! Leo nimedamkia huko JF kwenyewe sio hapa Jukwaani pamoja na boda wangu kuniingiza chaka.. Akidai kuna mdudu alimkanyaga na kutufanya tupotee njia lakini bado niliwahi kuliko wenyeji

Hivi ulishawahi kwenda kwa mtu na kukuta hata hajatoka kitandani? Unaweza kuishia kuona haya huku roho ikikusuta... Hata kama ahadi ni deni lakini sio kwa kuwahi huko

Anyway JF IMETUHESHIMISHA (Msemo wa Maxence Melo - Founder) Nami nasema asante sana!
Asante na shukrani zangu nyingi hazitakamilika bila kuwataja hawa
1. Founders wa JF
2. Uongozi na viongozi wote wa JF
3.Members Wote waliotupigia kura
4. Marafiki na maadui pia
Kwa wote niliowaja hapo kila mmoja kwa nafasi yake amefanya hili liwezekane

Kuna ambao sikuwataja hapa! Si kwamba nimepitiwa la hasha.. Bali wana nafasi zao maalum kabisa kwenye hii heshima. Nao ni Mungu Mwenyezi yote( mimi ni mwamini) na familia yangu ninayoipenda sana.. Kisha ndugu jamaa na marafiki
Kuna huyu member mkongwe Elli huyu ndiye alinifanya nkajoin JF.

Usiposhukuru kwa kidogo hata ukipewa kikubwa bado utaona umepunjwa.. Na pesa japo ndio kama msingi wa karibia kila kitu kwenye maisha lakini SI KILA KITU kwenye maisha

Nimefarijika, nimefurahi kupata tuzo husika toka kwenye majukwaa matatu.. HM, Photos na Intelligence.. Ushindi huu si wangu pekeyangu bali ni wana JF wote ambao tulikuwa pamoja kwenye majukwaa husika na mengineyo pia.. Mimi nimetumika kama mwakilishi tuu

Panapo uhai, afya, siha njema na uwezo kuna kitu nitarudi kukisema hapa tarehe 27 March 2024.. Yaani mwaka mmoja toka leo.. Zawadi nilizopata zitabaki kuwa kumbukumbu ya kuvutia na furaha kubwa kwangu

Kwa moyo mkuu na kwa unyenyekevu mkubwa nasema asanteni wote ambao kwa njia moja ama nyingine mmechangia ushindi huu

Mungu ibariki JF
 
Picha ya zawadi
Ukiona manyoya?
20230327_130338.jpg
20230327_170917_HDR.jpg
 
Back
Top Bottom