Asante Ndimara Tegambwage umenena vyema

Asante Ndimara Tegambwage umenena vyema

twijuke

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
547
Reaction score
252
HATUA ya kufutiwa uanachama huwa haieleweki vizuri kwa watu wengi. Kuna mambo mengi ya kufanya pale unapofutiwa uanachama.

Unaweza kukaa kimya. Ukakubali kuondoka katika chama na hata ukaanzisha chama chako au kujiunga na chama kingine.

Unaweza kukaa kimya na ukaendelea kufanya mambo ambayo yanaweza hata kukisaidia chama ambamo umetimuliwa na hata vyama vingine. Ukapata umaarufu kufikia hatua ya waliokufuta uanachama kuanza kukuchumbia.

Unaweza kusahau shughuli zote za vyama vya siasa. Ukang'ang'ania eneo ulilosomea, ulilopenda, unalofahamu fika; na kujisimika kikamilifu. Hapa waweza kutumia uzoefu wako katika shughuli za siasa, kujenga mtazamo mpya juu ya mwenendo wa mambo katika jamii. Kama ni mwalimu, mchumi, mwanasheria, mwandishi wa habari, mfanyabiashara, mchuuzi/mjasiriamali au hata mkulima au mfugaji, waweza kutumia kile ulichochuma katika mienendo ya siasa, kutolea mifano ya kuleta mabadiliko katika jamii.

Unaweza kwenda mahakamani – ukashitaki waliokuvua uanachama; na unaweza kushinda. Tatizo la kushinda mahakamani, katika siasa, ni kama kushindwa. Hii ni tofauti na kudai fedha. Unaweza kushinda na kujifariji kuwa umeonyesha jinsi ya kujipigania; lakini huwezi kushinda mahakamani na kurudi kufanya kazi za siasa na wale waliokuvua uanachama.

Unaweza kujiuzulu uanachama kabla hawajakufukuza; na bila kelele wala mikwaruzo. Hili nalo lina heshima yake hasa unapokuwa umeamua kuachana na malumbano na kukashifiana. Hatua hii inafanana kimya kinene na inaendana na eneo Na. 2 hapo juu, ambako unabaki katika jamii na sura yako ileile lakini ukiwa ‘ubongo rejea' kwa kila anayehitaji msaada wako.

Unaweza kuamua kujiua kisiasa, kijamii na kitaaluma; na wakati mwingine kiuchumi – kwa kujiingiza katika minyukano ya gharama kubwa – na wale unaowaita ‘wabaya' wako. Muda wako, fikra zako, rasilimali zako, hadhi na sura yako vinaweza kuteketea kwa mafao haba au bila mafao yoyote.

Unaweza kujiunga na wapinzani wakubwa wa chama chako ambamo umevuliwa uanachama. Ukatumika kwelikweli kukisema vibaya chama chako cha zamani. Ukapewa ujira mkubwa, ukabebwa juujuu na hata kuteuliwa kuwa mtu mkubwa katika siasa nchini mwako. Ukajiliwaza kwamba ‘afadhali nimewakomoa!'

Baada ya muda mfupi ukajizika mwenyewe. Mifano ya aina hii ni mingi Tanzania, hasa kwa wale waliochomoka/chomolewa kutoka upinzani na kuingia CCM wakitamba kuwa wana ‘siri' za upinzani wakati ni ama ulafi au njaa yao binafsi.

Uwanja ni mpana kwa wanasiasa wa kweli na wababaishaji; na kila uamuzi unaochukuliwa; kila mkondo unaochaguliwa una athari zake – mbaya au nzuri. Bali hakuna ramli. Ni kukaa na kufikiri, hasa kwa wale walioamua kwa dhati kwamba wanataka kutumikia siasa. Bali kwa wale ambao hawakujua tofauti kati ya siasa za vyama na uana-harakati, watateseka sana kabla hawajapata MSHAURI.

Katika mazingira ambamo siasa zinagusa maisha ya kila mtu kupitia mifumo – sera, sheria, kanuni, uamuzi mbalimbali – uwakilishi baraza la madiwani au bungeni, au uteuzi ikulu au kwingine kwenye madaraka; si njia pekee ya kufanya siasa. Hata wanaokana siasa ndio wanafanya siasa pevu ya kukana siasa bila mafanikio.

Makala hii imeandaliwa na Ndimara Tegambwage, ipo kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Jan 2014.
 
Ninachojaribu kutafakari juu ya Mahakama zetu ni pale zinapotoa hukumu za kuwabakisha wanachama kwenye vyama ili 'wasiathirike'.
Mwanachama wa chama cha siasa kama mtu binafsi anayo haki ya 'kulindwa na Mahakama' but on the other way round iko hivi: Je vyama kama Taasisi nazo si zina haki ya kulindwa na Mahakama kwa mujibu wa Katiba zao na Katiba ya nchi kwa ujumla!?
Kwa maana hiyo, kweli inawezekana siku moja ikatokea Mahakama 'ikatoa hukumu' ya kumlazimisha mwanachama aliyeamua kuondoka/kukihama chama asiondoke ili isisababishe damage kwa chama na shughuli zake? (fikiria mara mbili kama hujanielewa tafadhali).

Yuko sahihi kabisa. Ni kama maisha ya ndoa, mume anatoa talaka kwa mke kwa tuhuma kuwa mke huyo ni kahaba( na anatoa ushahidi) na mchawi nao ushahidi unatolewa. Kisha mke anaenda kanisani/ mahakamani kupinga ndoa kuvunjika na huko hukumu inatoka kuwa ndoa hiyo haiwezi kuvunjika kwa vile ilifungwa kanisani na ndoa ya kikristo haivunjiki hadi kifo hivyo jamaa amchukue tuu mkewe na waendelee kuishi.
Lakini jee kuna ndoa tena hapo?
 
Good analysis, Zitto unakazi ya kututhibitishia Kuwa wewe siyo mbinafsi kama tunavyo kutazama sasa huku nje.
 
huyu ni msukule wa mbowe unategemea angeandika tofauti na alichokiandika?ningeshangaa.
 
HATUA ya kufutiwa uanachama huwa haieleweki vizuri kwa watu wengi. Kuna mambo mengi ya kufanya pale unapofutiwa uanachama.

Unaweza kukaa kimya. Ukakubali kuondoka katika chama na hata ukaanzisha chama chako au kujiunga na chama kingine.
Unaweza kukaa kimya na ukaendelea kufanya mambo ambayo yanaweza hata kukisaidia chama ambamo umetimuliwa na hata vyama vingine. Ukapata umaarufu kufikia hatua ya waliokufuta uanachama kuanza kukuchumbia.
Unaweza kusahau shughuli zote za vyama vya siasa. Ukang'ang'ania eneo ulilosomea, ulilopenda, unalofahamu fika; na kujisimika kikamilifu. Hapa waweza kutumia uzoefu wako katika shughuli za siasa, kujenga mtazamo mpya juu ya mwenendo wa mambo katika jamii. Kama ni mwalimu, mchumi, mwanasheria, mwandishi wa habari, mfanyabiashara, mchuuzi/mjasiriamali au hata mkulima au mfugaji, waweza kutumia kile ulichochuma katika mienendo ya siasa, kutolea mifano ya kuleta mabadiliko katika jamii
Unaweza kwenda mahakamani – ukashitaki waliokuvua uanachama; na unaweza kushinda. Tatizo la kushinda mahakamani, katika siasa, ni kama kushindwa. Hii ni tofauti na kudai fedha. Unaweza kushinda na kujifariji kuwa umeonyesha jinsi ya kujipigania; lakini huwezi kushinda mahakamani na kurudi kufanya kazi za siasa na wale waliokuvua uanachama.
Unaweza kujiuzulu uanachama kabla hawajakufukuza; na bila kelele wala mikwaruzo. Hili nalo lina heshima yake hasa unapokuwa umeamua kuachana na malumbano na kukashifiana. Hatua hii inafanana kimya kinene na inaendana na eneo Na. 2 hapo juu, ambako unabaki katika jamii na sura yako ileile lakini ukiwa ‘ubongo rejea' kwa kila anayehitaji msaada wako.
Unaweza kuamua kujiua kisiasa, kijamii na kitaaluma; na wakati mwingine kiuchumi – kwa kujiingiza katika minyukano ya gharama kubwa – na wale unaowaita ‘wabaya' wako. Muda wako, fikra zako, rasilimali zako, hadhi na sura yako vinaweza kuteketea kwa mafao haba au bila mafao yoyote.
Unaweza kujiunga na wapinzani wakubwa wa chama chako ambamo umevuliwa uanachama. Ukatumika kwelikweli kukisema vibaya chama chako cha zamani. Ukapewa ujira mkubwa, ukabebwa juujuu na hata kuteuliwa kuwa mtu mkubwa katika siasa nchini mwako. Ukajiliwaza kwamba ‘afadhali nimewakomoa!'

Baada ya muda mfupi ukajizika mwenyewe. Mifano ya aina hii ni mingi Tanzania, hasa kwa wale waliochomoka/chomolewa kutoka upinzani na kuingia CCM wakitamba kuwa wana ‘siri' za upinzani wakati ni ama ulafi au njaa yao binafsi.
Uwanja ni mpana kwa wanasiasa wa kweli na wababaishaji; na kila uamuzi unaochukuliwa; kila mkondo unaochaguliwa una athari zake – mbaya au nzuri. Bali hakuna ramli. Ni kukaa na kufikiri, hasa kwa wale walioamua kwa dhati kwamba wanataka kutumikia siasa. Bali kwa wale ambao hawakujua tofauti kati ya siasa za vyama na uana-harakati, watateseka sana kabla hawajapata MSHAURI.
Katika mazingira ambamo siasa zinagusa maisha ya kila mtu kupitia mifumo – sera, sheria, kanuni, uamuzi mbalimbali – uwakilishi baraza la madiwani au bungeni, au uteuzi ikulu au kwingine kwenye madaraka; si njia pekee ya kufanya siasa. Hata wanaokana siasa ndio wanafanya siasa pevu ya kukana siasa bila mafanikio.

Makala hii imeandaliwa na Ndimara Tegambwage, ipo kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Jan 2014.

CC: Pasco
 
Last edited by a moderator:
Yuko sahihi kabisa. Ni kama maisha ya ndoa, mume anatoa talaka kwa mke kwa tuhuma kuwa mke huyo ni kahaba( na anatoa ushahidi) na mchawi nao ushahidi unatolewa. Kisha mke anaenda kanisani/ mahakamani kupinga ndoa kuvunjika na huko hukumu inatoka kuwa ndoa hiyo haiwezi kuvunjika kwa vile ilifungwa kanisani na ndoa ya kikristo haivunjiki hadi kifo hivyo jamaa amchukue tuu mkewe na waendelee kuishi.
Lakini jee kuna ndoa tena hapo?
Asante kwa mfano mzuri na wa kueleweka. Na kwa vile lengo la chama ni wanachama kushirikiana ili kufikia malengo tarajiwa huku 'crushing' ya mawazo ikiwa within. Sasa nguvu ya Mahakama (sio sheria!!) inapokuwa kigezo cha uendeshwaji wa chama tafsiri yake inakuwaje!?
Kimsingi mimi na wewe najua hili sakata tumeshalielewa lakini tunaleta haya mawazo ili wengi miongoni mwetu waweze kuelewa.

huyu ni msukule wa mbowe unategemea angeandika tofauti na alichokiandika?ningeshangaa.

fanya uchanganuzi mwenyewe uone alichoandika kama hakina mantiki, ushabiki maandazi hauna maana katika kipindi hiki ambacho umeme umepanda maradufu na hali ya maisha inazidi kuwa mbaya kila ukicha...
 
Good analysis, Zitto unakazi ya kututhibitishia Kuwa wewe siyo mbinafsi kama tunavyo kutazama sasa huku nje.
Kazi nyingine ni tamko la Mzee Mkono (mpaka sasa hajakanusha).
ZZK alisema ana Freelander na Carina ambayo inakaaga Mwadiga.
TL akasema amehongwa NISSAN Patrol na Land Cruiser
Mzee Mkono akasema amemuuzia Patrol na 'anamkodisha' Landcruiser tangu mwaka 2009.

Nilichosikia baada ya haya maelezo ni kumuita mmoja wapo wa hawa 'kifaranga' lakini majibu halisi bado.

Tusubiri mengi, ila Zitto kama anajitakia marefu katika siasa atulie ajipange. Atapata umaarufu hata bila kutumika na kina Mwigulu na Nchimbi. Zitto wewe ni maarufu. Jipange upya. Bado umri unaruhusu. Angalia wapi umeteleza, bila kukubali kama umekosa utaendelea kujichanganya na mwisho utahumbuka. Tulizana.
 
Nilisema kuhusu Zitto kusahau kuhusu kuwa na uwezo wa kufanya kazi na viongozi alioshindana nao mahakamani.

Na siyo kushindana nao mahakamani tu, hata na kuwatuhumu kuwa mafisadi na wazinzi!

I think he (Zitto) knows he is a goner. But he just doesn't want to go down quietly without inflicting damage of his own to the party.

Otherwise why take the fight to court when the party (or at least its leaders and a good number of its members) have clearly made it clear that they don't want you?
 
Ninachojaribu kutafakari juu ya Mahakama zetu ni pale zinapotoa hukumu za kuwabakisha wanachama kwenye vyama ili 'wasiathirike'.
Mwanachama wa chama cha siasa kama mtu binafsi anayo haki ya 'kulindwa na Mahakama' but on the other way round iko hivi: Je vyama kama Taasisi nazo si zina haki ya kulindwa na Mahakama kwa mujibu wa Katiba zao na Katiba ya nchi kwa ujumla!?
Kwa maana hiyo, kweli inawezekana siku moja ikatokea Mahakama 'ikatoa hukumu' ya kumlazimisha mwanachama aliyeamua kuondoka/kukihama chama asiondoke ili isisababishe damage kwa chama na shughuli zake? (fikiria mara mbili kama hujanielewa tafadhali).

Mkuu omujubi kuna majaji na Mahakimu Hodari (hawa wanaitwa Bold Judges) na kuna waogo na wahafidhina hawa wanaitwa (Timorous soul Judges)....Sasa unapokwenda Mahakamani na kukutana na huyo wa kwanza atakueleza bayana kwamba uanachama wa chama cha siasa au kikundi kama (mbesii au vya kufa na kuzikana ni hiyari) lakini ukikutana na timorus soul ambao wengi wanakuwa pro government tarajia lolote ndo yaleyale maamuzi ya aibu kama suala la Mgombea Binafsi .

Kwa kukukumbusha Tu hata tume ya Dk.Nchimbi iliyochunguza na kuwasafisha Polisi kwamba hawahusiki na Kumuuwa Mwangosi iliongozwa na jaji (Ihema) lakini wakati huohuo Tume nyingine ya Haki za Binadamu katika suala hilohilo iliyoongozwa na Jaji Manento(hapa alikuwa Bold) ilikuja na taarifa iliyo watuhumu mojakwa moja Polisi na Kumgusa Kamuhanda kama muhusika Mkuu.

Kiuhalisia kujiunga na vyama vya siasa ni suala la hiyari kama ndoa huwezi kulazimishwa na Mahakama kuishi na mwenza wako wakati humuhitaji au tabia yake mbaya imekukifu .Mwisho wa yote katika suala hili itabainika tu kwamba Mh.Zitto baada ya kufuata usha uri mbovu alitimkia Mahakamani kabla ya wakati au kumaliza taratibu za ndani za chama chake.
 
HATUA ya kufutiwa uanachama huwa haieleweki vizuri kwa watu wengi. Kuna mambo mengi ya kufanya pale unapofutiwa uanachama.

Unaweza kukaa kimya. Ukakubali kuondoka katika chama na hata ukaanzisha chama chako au kujiunga na chama kingine.

Unaweza kukaa kimya na ukaendelea kufanya mambo ambayo yanaweza hata kukisaidia chama ambamo umetimuliwa na hata vyama vingine. Ukapata umaarufu kufikia hatua ya waliokufuta uanachama kuanza kukuchumbia.

Unaweza kusahau shughuli zote za vyama vya siasa. Ukang’ang’ania eneo ulilosomea, ulilopenda, unalofahamu fika; na kujisimika kikamilifu. Hapa waweza kutumia uzoefu wako katika shughuli za siasa, kujenga mtazamo mpya juu ya mwenendo wa mambo katika jamii. Kama ni mwalimu, mchumi, mwanasheria, mwandishi wa habari, mfanyabiashara, mchuuzi/mjasiriamali au hata mkulima au mfugaji, waweza kutumia kile ulichochuma katika mienendo ya siasa, kutolea mifano ya kuleta mabadiliko katika jamii.

Unaweza kwenda mahakamani – ukashitaki waliokuvua uanachama; na unaweza kushinda. Tatizo la kushinda mahakamani, katika siasa, ni kama kushindwa. Hii ni tofauti na kudai fedha. Unaweza kushinda na kujifariji kuwa umeonyesha jinsi ya kujipigania; lakini huwezi kushinda mahakamani na kurudi kufanya kazi za siasa na wale waliokuvua uanachama.

Unaweza kujiuzulu uanachama kabla hawajakufukuza; na bila kelele wala mikwaruzo. Hili nalo lina heshima yake hasa unapokuwa umeamua kuachana na malumbano na kukashifiana. Hatua hii inafanana kimya kinene na inaendana na eneo Na. 2 hapo juu, ambako unabaki katika jamii na sura yako ileile lakini ukiwa ‘ubongo rejea’ kwa kila anayehitaji msaada wako.

Unaweza kuamua kujiua kisiasa, kijamii na kitaaluma; na wakati mwingine kiuchumi – kwa kujiingiza katika minyukano ya gharama kubwa – na wale unaowaita ‘wabaya’ wako. Muda wako, fikra zako, rasilimali zako, hadhi na sura yako vinaweza kuteketea kwa mafao haba au bila mafao yoyote.

Unaweza kujiunga na wapinzani wakubwa wa chama chako ambamo umevuliwa uanachama. Ukatumika kwelikweli kukisema vibaya chama chako cha zamani. Ukapewa ujira mkubwa, ukabebwa juujuu na hata kuteuliwa kuwa mtu mkubwa katika siasa nchini mwako. Ukajiliwaza kwamba ‘afadhali nimewakomoa!’

Baada ya muda mfupi ukajizika mwenyewe. Mifano ya aina hii ni mingi Tanzania, hasa kwa wale waliochomoka/chomolewa kutoka upinzani na kuingia CCM wakitamba kuwa wana ‘siri’ za upinzani wakati ni ama ulafi au njaa yao binafsi.

Uwanja ni mpana kwa wanasiasa wa kweli na wababaishaji; na kila uamuzi unaochukuliwa; kila mkondo unaochaguliwa una athari zake – mbaya au nzuri. Bali hakuna ramli. Ni kukaa na kufikiri, hasa kwa wale walioamua kwa dhati kwamba wanataka kutumikia siasa. Bali kwa wale ambao hawakujua tofauti kati ya siasa za vyama na uana-harakati, watateseka sana kabla hawajapata MSHAURI.

Katika mazingira ambamo siasa zinagusa maisha ya kila mtu kupitia mifumo – sera, sheria, kanuni, uamuzi mbalimbali – uwakilishi baraza la madiwani au bungeni, au uteuzi ikulu au kwingine kwenye madaraka; si njia pekee ya kufanya siasa. Hata wanaokana siasa ndio wanafanya siasa pevu ya kukana siasa bila mafanikio.

Makala hii imeandaliwa na Ndimara Tegambwage, ipo kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Jan 2014.

From @GALinoma:
"Zitto ameijenga chadema na amewavutia wengi waingie chadema, ukiondoa Mbowe wengine wote pale juu wamemkuta Zitto na ni yeye aliyewachagiza wajiunge chadema leo wanajaribu kumtusi kivipi?Tunaofahamu siasa na wanasiasa hawa tuliona mbali tukaonya na kushauri suala hili litakigharimu chama, lakini ikadharaulika, wakabeza naona shughuli yake wanaipata sasa mpaka wanakimbia mahakamani. Zitto sio mwepesi kama baadhi ya watu wanavyojidanganya. Tulisema mtu huyu si wa kung'oa na kutupa kirahisi ni mzito kama jina lake na hii ni kutokana na mchango wa jasho lake alioutoa kuijenga CDM. Vijana walioanza siasa 2010 leo wamepandikizwa chuki na uongo kutwa nzima wanatukana hovyo mitandaoni. Wengine hatusemi lakini tumeona mengi na kuwaona wengi. Leo hii chama kinavurugwa inaumiza sana. Tatizo kuna watu wanajipa mamlaka ya kukiendesha chama ndio hao hao wavurugaji, watunga uongo, watunga fitna na uzandiki. Haya hayasaidii bali kuathiri ustawi wa chama. Mtu mbunge mzima unamobilize vijana waache kufanya kazi wakajazane mahakamani kuzomea. Huku ni kuwajaza ujinga. Naskitika vijana wamegeuzwa vipasa sauti vya wahafidhina, walilia posho na wafuja ruzuku. "
 
Kumbe boss wa mtunzi ni mbowe?hivi umaweza kumpondea boss wako?kuna usemi wa mjini boss hanuniwi
 
Back
Top Bottom