Asante Ndimara Tegambwage umenena vyema

Asante Ndimara Tegambwage umenena vyema

Mbowe tumepigwa naye mabomu, Mbowe tumesota nae rumande, Mbowe tumepoteza muda wetu sote kwa kazi za chama, Mbowe tumeingia gharama zetu binafsi kwa ajili ya chama. Mwacheni Mbowe wetu jamani!
ukiwa ni muhalifu kama yeye, na uhalifu wenu mnafanya pamoja! ni wazi madhara ya uhalifu lazima mpate wote. ajabu! unakna fahari kuwekwa rumande? au ulipata mwenza ukiwa huko?
hongera
 
Naendelea kusisitiza ni muhuni kwa maana mwanasiasa huyu mzoefu wa haya mambo ya kufukuzana ingekuwa ni busara zaidi kipindi mgogoro huu unaanza angemuita Kijana ZZK na kujaribu kumshauri naamini ZZK ni kijana msikivu sana lakini sio hii alofanya kushauri baada ya moto kuwa mkali zaidi mambo ya "angelijua"yashapitwa na wakati,alichofanya ni kujikosha kwa akina Mbowe na Slaa ndo maana ushauri wake kautoa kwenye gazeti la Tanzania Daima,kuwa mjanja mkuu fungua macho...huu mgogoro watu washaufanya mtaji.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums

Hapa sielewi yani alosema hapo si kweli?

Na kama ni kweli hakutakiwa kusema kisa hakumshauri?

Na pia unauhakika kwamba hajamshauri? Na mbona kwa huu uzi kasema mengi ambayo zitto anawezafanyia kazi?

Lakini tabia ya zitto ya ovaconfidence si waijua mkuu wangu.

Sawa inaweza akawamuhuni kama unavosema ww je umepima na kugundua kwamba hizo hoja zake zina uhuni?
 
Mkuu naamini tutakuwa hatujaelewana ila tunaweza kukubaliana kutokuelewana katika hili tegambwage,zaidi ya hayo kheri ya mwaka mpya japo umechakaa kidogo..

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Kazi nyingine ni tamko la Mzee Mkono (mpaka sasa hajakanusha).
ZZK alisema ana Freelander na Carina ambayo inakaaga Mwadiga.
TL akasema amehongwa NISSAN Patrol na Land Cruiser
Mzee Mkono akasema amemuuzia Patrol na 'anamkodisha' Landcruiser tangu mwaka 2009.

Nilichosikia baada ya haya maelezo ni kumuita mmoja wapo wa hawa 'kifaranga' lakini majibu halisi bado.

Tatizo wengi huwa hatuelewi au kujielewa. kunapokuwa na pande mbili zinazopingana binadamu huwa kisaikolojia lazima awe upande mmoja. Washabiki wa michezo wanalijua sana hili maana hata ungekuta timu mbili zinacheza na haumujui hata mmoja wa wachezaji haitakuchukua muda utakuwa ushapata timu ya kusapoti na pinzani.
Hiki ndo kinachotokea na huwa mtu anapenda kuamini upande aliolazimishwa na nafsi kuwa sahihi au ndo wenye haki au unastahili kushinda. Hii hali huwa ni ngumu kuibadilisha kwa kipindi hicho mpaka yaje yatokee mengine ambayo yatailazimisha nafsi kujua kuwa ulichokiamini mwanzoni siyo sahihi au upande fulani ulikuwa unaonewa.
Kuamini kuwa ZZk ni msaliti au si msaliti wengi wetu tunasukumwa na nafsi na kusoma mabandiko humu jf au popote pale.
Bali kuna watu wanaojua ukweli ila kwa sababu za maslahi hupotosha ukweli na kusema ZZk ni msaliti au si msaliti (kulingana na yeye anafaidika na upande upi) na hawa ni wataalamu wa kuandika na kushawishi na huwa wameegamia upande mmoja.
Kwa hali ya kawaida usitegemee Tanzania Daima litaweka bandiko lako kama upo upande wa kumkashifu Mbowe & Co.
Suala la ZZk kujibu kila tuhuma au kutoa ufafanuzi haiwezekani na ni sawa na Mbowe & Co. ila kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa nafsi yako imekutuma vp, asipojibu ZZk unahoji, lakini Mbowe & Co hautahoji na wala tuhuma zake hautaziona.

Salaam.
 
Hata kama zitto angekuwa kakitumikia chama kwa jasho la damu,haiwezi kumpa uhalali wa kuhujumu chama,kuvunja kanuni na misingi ya chama kwa kuanzisha makundi tena kwa kushirikiana na watu walio nje au waliofukuzwa cdm then akaachwa,Tunasema haiwezekani na haitawezekana! hata SHETANI alikuwa ndiye MALAIKA MKUU tena mwenye uwezo mkubwa lakn alivyoasi alifukuzwa mara moja,sembuse ZZK tu!!?
 
Mahakama siyo Chombo cha uadui, ni Chombo cha kudai haki
Ni matumaini yangu Viongozi wa Chadema watakuwa Wakomavu kisiasa na hivyo kuendlkea kufanya kazi na Zitto iwapo atashinda rufani yake katika baraza kuu

Na pia ni matumaini yangu Zitto atafanya kazi na viongozi wa Chadema bila kinyongo iwapo atashinda rufani yake katika baraza kuu.
Chadema itabidi iunde tume ya maridhiano na kusameheana ili "yaliyopita si ndwele tugange yajayo".

Pamoja na Uchambuzi mzuri wa Ndimara Tegambwage, ILA AMESAHAU OPTION MOJA AMBAYO NI "KUSAMEHEANA" KWA PANDE ZOTE MBILI BAADA YA SINTOFAHAMU NA KUKURUKAKARA ZOTE KUTOKEA.

MIMI NINASEMA INAWEZEKANA KWA PANDE ZOTE MBILI KUSAMEHEANA, KAMA MANDELA ALIWASAMEHE MAKABURU, ZITTO ATASHINDWAJE KUWASAMEHE WANAOMPIKIA JUNGU?

AU MBOWE ATASHINDWAJE KUMSAMEHE ZITTO KWA YALE ALIYOMKWAZA NAYO?.

Hoja ya Zitto kutokutakiwa Chadema ni hoja ya Kijinga, Kama Chadema ni kambi ya Mbowe basi Kweli hatakiwi, Lakini kama Chadema ni Ya WanaChadema kutoka nchi nzima basi Zitto anatikiwa, na Baraza Kuu ndiyo Chombo kitakachohitimisha hili
 
Ninachojaribu kutafakari juu ya Mahakama zetu ni pale zinapotoa hukumu za kuwabakisha wanachama kwenye vyama ili 'wasiathirike'.
Mwanachama wa chama cha siasa kama mtu binafsi anayo haki ya 'kulindwa na Mahakama' but on the other way round iko hivi: Je vyama kama Taasisi nazo si zina haki ya kulindwa na Mahakama kwa mujibu wa Katiba zao na Katiba ya nchi kwa ujumla!?
Kwa maana hiyo, kweli inawezekana siku moja ikatokea Mahakama 'ikatoa hukumu' ya kumlazimisha mwanachama aliyeamua kuondoka/kukihama chama asiondoke ili isisababishe damage kwa chama na shughuli zake? (fikiria mara mbili kama hujanielewa tafadhali).

Omujubi we kavue samaki kyoma hapa sio mahala pako..

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Zitto tells Mbowe and co "IF YOU ARE A BULL BUCKER, I AM A DUPPY CONQUEROR"

"You ago tired to see me face
Me say you can't get me out of the race
Oh Men you said i'm in your place
And then you draw bad card
I make you draw bad card
Propaganda spreading over my name
Say if you wanna bring another life to shame
I want to disturb my neighbor as i'm feeling so alright
In a rub dub style, rub dub style
"
 
Kwa jinsi nilivyoelewa makala yake. Conclusion inakuja kwamba no matter how, but ukishapata misukosuko ya kisiasa, inayopelekea kutoka kwenye chama, basi ndio hakuna namna ya kurejea vizuri kama ilivyokuwa kabla zaidi ya jahazi kuwa limezama forever.

But Kama hivi ndivyo Hasa anavyomaanisha. Mm nagomaga mwanawane.
 
From @GALinoma:
"Zitto ameijenga chadema na amewavutia wengi waingie chadema, ukiondoa Mbowe wengine wote pale juu wamemkuta Zitto na ni yeye aliyewachagiza wajiunge chadema leo wanajaribu kumtusi kivipi?Tunaofahamu siasa na wanasiasa hawa tuliona mbali tukaonya na kushauri suala hili litakigharimu chama, lakini ikadharaulika, wakabeza naona shughuli yake wanaipata sasa mpaka wanakimbia mahakamani. Zitto sio mwepesi kama baadhi ya watu wanavyojidanganya. Tulisema mtu huyu si wa kung'oa na kutupa kirahisi ni mzito kama jina lake na hii ni kutokana na mchango wa jasho lake alioutoa kuijenga CDM. Vijana walioanza siasa 2010 leo wamepandikizwa chuki na uongo kutwa nzima wanatukana hovyo mitandaoni. Wengine hatusemi lakini tumeona mengi na kuwaona wengi. Leo hii chama kinavurugwa inaumiza sana. Tatizo kuna watu wanajipa mamlaka ya kukiendesha chama ndio hao hao wavurugaji, watunga uongo, watunga fitna na uzandiki. Haya hayasaidii bali kuathiri ustawi wa chama. Mtu mbunge mzima unamobilize vijana waache kufanya kazi wakajazane mahakamani kuzomea. Huku ni kuwajaza ujinga. Naskitika vijana wamegeuzwa vipasa sauti vya wahafidhina, walilia posho na wafuja ruzuku. "

Zitto kaijenga vip Chadema?? unaijua chadema na ilipotoka?? alikuwa na resource zipi za kujenga chadema?? be clear Chadema imemjenga Zitto na si vinginevyo.. Unataka kuniambia Zitto kaijenga Chadema kuliko Slaa na wakina Ndessamburo??

Zitto alikuwa kijana mdogo, aliyelelewa na chama na kufanya kazi za chama ili kupata chochote, hakuna jingine zaidi ya hilo na ndo mana kabla ya Ubunge hukuwai msikia! Hakuna maarufu kuliko taasisi iliyokukuza, amepotoka na atajuta..

Hivi unajua hata huo ubunge na fedha za kampeni alipozipata?? Ajifunze shukrani na kuheshimu waliomuinua, njaa na tabu sana na ikizidi na hatari zaidi..
 
From @GALinoma:
"Zitto ameijenga chadema na amewavutia wengi waingie chadema, ukiondoa Mbowe wengine wote pale juu wamemkuta Zitto na ni yeye aliyewachagiza wajiunge chadema leo wanajaribu kumtusi kivipi?Tunaofahamu siasa na wanasiasa hawa tuliona mbali tukaonya na kushauri suala hili litakigharimu chama, lakini ikadharaulika, wakabeza naona shughuli yake wanaipata sasa mpaka wanakimbia mahakamani. Zitto sio mwepesi kama baadhi ya watu wanavyojidanganya. Tulisema mtu huyu si wa kung'oa na kutupa kirahisi ni mzito kama jina lake na hii ni kutokana na mchango wa jasho lake alioutoa kuijenga CDM. Vijana walioanza siasa 2010 leo wamepandikizwa chuki na uongo kutwa nzima wanatukana hovyo mitandaoni. Wengine hatusemi lakini tumeona mengi na kuwaona wengi. Leo hii chama kinavurugwa inaumiza sana. Tatizo kuna watu wanajipa mamlaka ya kukiendesha chama ndio hao hao wavurugaji, watunga uongo, watunga fitna na uzandiki. Haya hayasaidii bali kuathiri ustawi wa chama. Mtu mbunge mzima unamobilize vijana waache kufanya kazi wakajazane mahakamani kuzomea. Huku ni kuwajaza ujinga. Naskitika vijana wamegeuzwa vipasa sauti vya wahafidhina, walilia posho na wafuja ruzuku. "

ZZK kawaleta uvccm mahakamani, waratibu wa vijana hao wa ZZK ni CCM; Zungumzia na hili.
 
huwa simtofautishi na muhogo mchungu. ful usanii
 
From @GALinoma:
"Zitto ameijenga chadema na amewavutia wengi waingie chadema, ukiondoa Mbowe wengine wote pale juu wamemkuta Zitto na ni yeye aliyewachagiza wajiunge chadema leo wanajaribu kumtusi kivipi?Tunaofahamu siasa na wanasiasa hawa tuliona mbali tukaonya na kushauri suala hili litakigharimu chama, lakini ikadharaulika, wakabeza naona shughuli yake wanaipata sasa mpaka wanakimbia mahakamani. Zitto sio mwepesi kama baadhi ya watu wanavyojidanganya. Tulisema mtu huyu si wa kung'oa na kutupa kirahisi ni mzito kama jina lake na hii ni kutokana na mchango wa jasho lake alioutoa kuijenga CDM. Vijana walioanza siasa 2010 leo wamepandikizwa chuki na uongo kutwa nzima wanatukana hovyo mitandaoni. Wengine hatusemi lakini tumeona mengi na kuwaona wengi. Leo hii chama kinavurugwa inaumiza sana. Tatizo kuna watu wanajipa mamlaka ya kukiendesha chama ndio hao hao wavurugaji, watunga uongo, watunga fitna na uzandiki. Haya hayasaidii bali kuathiri ustawi wa chama. Mtu mbunge mzima unamobilize vijana waache kufanya kazi wakajazane mahakamani kuzomea. Huku ni kuwajaza ujinga. Naskitika vijana wamegeuzwa vipasa sauti vya wahafidhina, walilia posho na wafuja ruzuku. "

Na mzee Mtei aseme nini sasa kama zzk amekuwa na mchango mkubwa? Watu waliingia kwa hiari yao kwa kufuata sera za chama na sio sera za ZZK bhana, acha uongo hapa. Alafu pia unaongelea upande mmoja tu, wale wahuni wanaoenda kumsupport ZZK kule mahakamani nao wameambiwa na CDM?
I hate ignorant sana.
 
Huyu alihusika sana kuiua NCCR Mageuzi! hivi yuko chama gani kwa sasa?
Hivi kwanini unaacha hoja na kutaka tujadili mtu? Badala ya kusoma hoja na kujikita huko wewe unaangalia mtoa hoja. Fallacy!
 
From @GALinoma:
"Zitto ameijenga chadema na amewavutia wengi waingie chadema, ukiondoa Mbowe wengine wote pale juu wamemkuta Zitto na ni yeye aliyewachagiza wajiunge chadema leo wanajaribu kumtusi kivipi?Tunaofahamu siasa na wanasiasa hawa tuliona mbali tukaonya na kushauri suala hili litakigharimu chama, lakini ikadharaulika, wakabeza naona shughuli yake wanaipata sasa mpaka wanakimbia mahakamani. Zitto sio mwepesi kama baadhi ya watu wanavyojidanganya. Tulisema mtu huyu si wa kung'oa na kutupa kirahisi ni mzito kama jina lake na hii ni kutokana na mchango wa jasho lake alioutoa kuijenga CDM. Vijana walioanza siasa 2010 leo wamepandikizwa chuki na uongo kutwa nzima wanatukana hovyo mitandaoni. Wengine hatusemi lakini tumeona mengi na kuwaona wengi. Leo hii chama kinavurugwa inaumiza sana. Tatizo kuna watu wanajipa mamlaka ya kukiendesha chama ndio hao hao wavurugaji, watunga uongo, watunga fitna na uzandiki. Haya hayasaidii bali kuathiri ustawi wa chama. Mtu mbunge mzima unamobilize vijana waache kufanya kazi wakajazane mahakamani kuzomea. Huku ni kuwajaza ujinga. Naskitika vijana wamegeuzwa vipasa sauti vya wahafidhina, walilia posho na wafuja ruzuku. "

Labda kama ulikataka kusema DARUSO, Zitto chadema ni kifaranga wa juzi watu tuko CDM kitambo hawezi kujiita mwenyeji kwa njia yoyote ile.
 
Kuna uzi humi JF unasema Mchawi wa Chadema ni Chadema wenyewe na uongozi wake. Dr. W P Slaa akaupa LIKE kuuubwa sana. Akili kumkichwa wandugu.
 
Back
Top Bottom