Habari za muda huu wadau?
Hongereni kwa mfungo na Allah ajaalie uwe ni wenye manufaa.
Miaka mitatu na na miezi mitatu iliyopita nilijaaliwa kufunga ndoa na mke wangu kipenzi, yeye hakuwa mwanamke wangu wa kwanza ila alikuwa mwanamke mwenye tabia njema kuliko wote ambao nimewahi kuwa nao maishani mwangu. Imani yake ya dini ni kubwa kuliko wote ambao nimewahi kuwa nao na vitu hivyo viwili ndio chachu ya mimi kuamua kumuoa yeye.
Kiasili mababu zake wanatokea Hadramaut-Yemen na walihamia Zenji kipindi kileeee cha ukoloni na Utumwa, wazazi wake yeye walizaliwa Zenji hivyo ni Wazanzibar kwa kuzaliwa. Ni mrembo haswa na rangi yake ya mtume sichoki kumtazama! Mke wangu tulijuana mwaka 2008 tukiwa Form Five (lakini hatukuanzisha mahusiano). Mungu kwa mipango yake baada ya kumaliza kidato cha sita tulifaulu na sote tukaelekea mwanza ambapo yeye alikuwa Bugando na mimi nikaelekea kwa baba mtakatifu Malimbe (SAUT). Baada ya kumaliza yeye akapata kazi mwanzo mwaka 2014 November na mimi nkapata kazi mwaka 2015 Feb (rasmi with contract).
Mimi ni mtoto wa kimaskini ila yeye kwao wamejaaliwa kiasi, alinipenda kwa umaskini wangu, akanithamini haswa! She wasan important pillar in believing into myself as always alikuwa akiniambia I will really reach far kimafanikio, nkimuuliza why? alikuwa anasema "I can just see it"
Alikuwa ndio nguzo ya ndoa yetu kufungwa maana ki-ukweli familia yake haikunikubali, (hawa wamanga wanatabu sana!!!) ila yeye alisisitiza kwamba ni lazima aolewe na mimi na namshukuru Mungu ndoa ilikuwa.
Alinipenda pale nlipokuwa sina kitu, nlipokuwa na kipato cha chini na mpaka sasa nina kipato cha kawaida. Mapenzi yake yanazidi kuongeza tu! Anampenda Mungu kuliko anavyonipenda mimi na hilo linanifanya nizidi kumpenda, mara kadhaa nshaamka usiku na kumkuta kwenye mswala anaswali, ukimuuliza kwanini hukuniamsha na mimi anasema nlikuwa nakuacha kidogo upumzike na ningekuamsha maana nataka niwe na wewe peponi!
Ni mwanamke tofauti na wanawake wengi sana hususan linapokuja suala la kumuogopa mungu wake, na hilo linanifanya niwe na amani ya hali ya juu. Mapambo ya kidunia hayamshtui moyo kabisa, anajua anachokifanya, hatumii make up kabisa, kwenye kabati lake anaweka nguo anazozitumia tu na asizozitumia anasema ni haki ya maskini, mara ya mwisho nimemshuhudia akigawa magauni mapya kabisa na kanga doti nyingi tu maana yeye hazitumii. Ana imani na yakini kwamba muda wowote atakufa na kurudi kwa mola wake na hilo linaikata kiu yake ya dunia.
Ni aina ya mwanamke ambae anakaa anakumbuka kisses tulizokuwa tuki-kiss kipindi cha uchumba wetu, na kuanza kulia na kulaumu kwamba kwanini tulimkosea mungu vile kwa kuikaribia zinaa?? Nitatoa ushuhuda hata mbele za Mungu kwamba sikuwahi kuzini nae kabla ya ndoa japo mimi nliwahi kuzini na wanawake wengine.
Leo kipenzi changu anaingia kwenye operation kujifungua mtoto wetu wa kwanza, am somehow excited and somehow worried. She is not worried at all na ananiambia hakuna kitakachotokea isipokuwa alichokiandiaka Mwenyezi Mungu na hilo ndio linamfanya asiwe na hofu. Nawaombeni dua na maombi yenu wadau. Nimlipe nini zaidi ya mapenzi ya dhati kwake?? Juu ya mengi ambayo tayari nimemfanyia kama shukrani kwa upendo wake, our trip to Singapore, Malaysia, Cambodia, Vietnam and Thailand later this year nadhani itakuwa miongoni mwa zawadi nzuri kwake
Ndani ya kipindi hiki cha Ramadhan amekataa kabisa kuacha kufunga na amefunga siku 16 zilizopita, amesoma jumla ya juzuu 21 mpaka jana usiku na anaskitika kwamba atakosa kumalizia juzuu 9 zilizobaki kwa kuwa atakuwa kwenye Nifas.
Nathibitisha kwamba hii ni bahati ya hali ya juu, na sijutii uamuzi wangu wa kuacha wale mademu wangu ambao wengine walikuwa na viuno vikubwa na macho mazuri na ambao baadhi waliolewa na sasa washaachika kwa tabia zao mbovu.
Kwa wasiojua: leo ni siku kubwa sana kwenye historia ya uislam maana leo ndio siku waislam walishinda vita vya Badr wakilishinda jeshi la Ma-Quraysh la zaidi ya watu 1000 huku wao wakiwa 313.
Leo ni siku kubwa kwa uislam na nadhani itakuwa siku kubwa kwangu pia.
Ahsante na mumkumbuke mke wangu kwenye maombi yenu maana anatuletea "Mtanzania" mpya leo.