Asante Mungu, deni la HESLB limekwisha

Hiyo loan board imekuwa kama jini la kunyonya damu kwa vijana, yaani kijana ndo anaanza kazi anarundikiwa deni la milioni 20 hadi milioni 35, halafu mnawaita watoto wa wanyonge. Ideally hawatakiwi kurejesha zaidi ya milioni 5 hasa kwa vyuo vikuu vya umma kwa sababu serikali inawajibika kutoa elimu kwa vijana kwa kutoa pesa za kuendesha vyuo ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya wahadhiri, sasa hii milioni 20 inatoka wapi utafikiri mtu amechukua mkopo benki......
 
Wasiliana na zonal offices kwa sehem uliyopo wao watakupa clearance certificate. Mie nimemaliza mwez wa pili bad luck nilichelewa kutumiwa clearance certificate hivyo ofisini kwangu wakaendelea kunikata, nilikatwa mwez March na April so ni zamu yangu sasa nawadai bodi ya mikopo japo sina uhakika wa kupata pesa yangu.
Kuipata hela yako ongea na wahasibu wako ofisini. Kama ni waelewa watachukua mtu ambaye mnafanana mshahara watamkata yeye kwa miezi hiyo miwili, halafu watakupa hiyo hela yake then kule bodi watapeleka marejesho ya wafanyakazi wengine kwa ku'less amount yako for 2 subsequent months.

Kwa mantiki hiyo, ile yako iliozidi itakua reallocated kwa yule mnaefanana mishahara (Hapa Muhasibu kupitia mwajiri itabidi waandike hiyo barua ya reallocation of funds)

NB: Tofauti na hapo nyoka halambi unga kule HESLB.
 
Hongera kwa kumaliza deni. Kuhusu hiyo paragraph yako ya mwisho, Mungu anisaidie! Kamwe sitaenda kuchukua hiyo clearance form!

Hao Helsb ni VIBAKA! Kuna wakati niliwajaribu kwa email wanipatie taarifa za deni langu, waliniletea deni tofauti kabisa na lile la kwenye Salary Slip! Nikajiuliza hivi kuna Bodi za Mikopo mbili nchini?

Nashukuru Salary Slip ilisoma 0 miaka kadhaa iliyopita. Ila kusema niwafuate ili wanibambikie deni hewa, hilo wasahau. Hiyo clearance form wabaki nayo tu kama ukumbusho.
 
Makato ya mkopo ni sahihi kabisa, mtoto akatwe kwenye mshahara wake kwa kuwa alitumia mwenyewe hiyo pesa... waelezwe tu mapema kuwa ‘boom’ ni Salary Advance so waitumbue kwa kujua.

Mzazi kuendelea kusota na kujibana kwa ajili ya msomi, ili tu eti asije kukatwa mshahara ni kuteseka tu... itegemeane tu kipato cha mzazi.
Upo sahihi mkuu
 
Nenda pale bodi wape index number yako ya form four watakuangalizia. Wakikuta limeisha watakupa hiyo clearance, wakikuta bado itakulazimu urudi umtaiti mwajiri wako kwamba marejesho alikua anapeleka au laa?

Kwa kuanzia anza na huo utaratibu utapata tu clearance letter.
Je na wasio ba uwezo wa kufika huko HESLB wafanyeje?
Natamani kujua Outstanding Loan.
Hawa waajiri hawaaminiki!
 
Hiyo loan board imekuwa kama jini la kunyonya damu kwa vijana, yaani kijana ndo anaanza kazi anarundikiwa deni la milioni 20 hadi milioni 35, halafu mnawaita watoto wa wanyonge. Ideally hawatakiwi kurejesha zaidi ya milioni 5 hasa kwa vyuo vikuu vya umma kwa sababu serikali inawajibika kutoa elimu kwa vijana kwa kutoa pesa za kuendesha vyuo ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya wahadhiri, sasa hii milioni 20 inatoka wapi utafikiri mtu amechukua mkopo benki......
Yaani acha tu! Kuna watu karibia wanachanganyikiwa wakisikia Bodi. Mtu anadaiwa 60+m, na anakatwa 149,000 kwa mwezi.
Anayarajia kulipa deni kwa takribani miaka 33+ (kama makato hayatpongezeka sana).
Kadiri ya umri wake, atastaafu na labda mafao yamalizie deni.
 
Hili swala haliingii akilini, kuna kitu lazima kifanyike kuwaokoa hawa vijana na matatizo ya kisaikolojia..
 
Mimi nilianza kukatwa mwaka 2012
Mpaka leo ni miaka takribani minane (08) na nilikopeshwa kwa means test 80% ila nahisi mwezi huu wa tano nimemalizana nao.
 
Yaani acha tu! Kuna watu karibia wanachanganyikiwa wakisikia Bodi. Mtu anadaiwa 60+m, na anakatwa 149,000 kwa mwezi.
Anayarajia kulipa deni kwa takribani miaka 33+ (kama makato hayatpongezeka sana).
Kadiri ya umri wake, atastaafu na labda mafao yamalizie deni.
Madaktari na wafamasia wanakutana Sana na hii dhahama.
 
Je na wasio ba uwezo wa kufika huko HESLB wafanyeje?
Natamani kujua Outstanding Loan.
Hawa waajiri hawaaminiki!
Ingia website ya HESLB utapata contacts za zonal uliyopo
Zonal zimewekwa kimikoa
Japo ni wagumu sana kujibu email ila unacopy had mkurugenz wao tena kwa kuwasumbua ndio utajibiwa

N.a. mara nying statements wanazotuma zinakuwa hazioneshi michango yote,ni jukumu lako kuwasumbua had waone kero
 
Hakikisha unapata risiti zako zote za marejesho ya kila mwez kutoka kwa muajiri wako..hii itakusaidia in case baadhi ya marejesho yasipoonekana kwenye outstanding loan statements kutoka bodi ya mikopo
Je na wasio ba uwezo wa kufika huko HESLB wafanyeje?
Natamani kujua Outstanding Loan.
Hawa waajiri hawaaminiki!
 
Nashkuru sana ..jumatatu ntafanyia kazi hili
Kuipata hela yako ongea na wahasibu wako ofisini. Kama ni waelewa watachukua mtu ambaye mnafanana mshahara watamkata yeye kwa miezi hiyo miwili, halafu watakupa hiyo hela yake then kule bodi watapeleka marejesho ya wafanyakazi wengine kwa ku'less amount yako for 2 subsequent months.

Kwa mantiki hiyo, ile yako iliozidi itakua reallocated kwa yule mnaefanana mishahara (Hapa Muhasibu kupitia mwajiri itabidi waandike hiyo barua ya reallocation of funds)

NB: Tofauti na hapo nyoka halambi unga kule HESLB.
 
Je na wasio ba uwezo wa kufika huko HESLB wafanyeje?
Natamani kujua Outstanding Loan.
Hawa waajiri hawaaminiki!
Inategemeana upo wapi, hawa jamaa wana zone office zao ambazo ni Mwanza, Arusha, Mbeya,Dodoma na Dsm. Kama upo maeneo hayo au una mtu maeneo hayo mpatie index namba yako ya olevel, mwaka uliomaliza Chuo, na jina la chuo mtume aende aombe statement ya outstanding Loan watampatia. Yaani fanya kama unampa details zako zote akifika pale ionekane ni wewe.
 
Back
Top Bottom