Asante Mungu, deni la HESLB limekwisha

Asante Mungu, deni la HESLB limekwisha

Katika vitu namshukuru Mungu siku zote, ni kusoma bila hii mikopo.. Ila hongera sana mkuu kwa kumaliza deni lako.
 
Elimu muhimu sana hii mkuu, japo sina deni nao ila hiki kitu sikua nafahamu, wadaiwa wanaomaliza ni vyema wakajua hii kitu.
Nenda pale bodi wape index number yako ya form four watakuangalizia. Wakikuta limeisha watakupa hiyo clearance, wakikuta bado itakulazimu urudi umtaiti mwajiri wako kwamba marejesho alikua anapeleka au laa?

Kwa kuanzia anza na huo utaratibu utapata tu clearance letter.
 
Mm nimeanza kurejesha makato ya mkopo wangu wa HESLEB oktoba mwaka 2018.
Na mshahara ghafi unasoma 716k sijui ni lini hili deni nalimaliza ni shidaaa kwa kweli
 
Victor Wilbard Mlaki Deni lako Bado ukimaliza Hilo kuna Deni la Value Rention Fee na riba vitaanza kukatwa ukimaliza Deni lililo kwenye salary slip.
U mean ...Kama kwenye salary slip deni limekwisha badae watakuja Tena kulirejesha ? Ufafanuzi please!
 
Mm nimeanza kurejesha makato ya mkopo wangu wa HESLEB oktoba mwaka 2018.
Na mshahara ghafi unasoma 716k sijui ni lini hili deni nalimaliza ni shidaaa kwa kweli
Tutamaliza mapema tu kwa 15%
Sisi tulioanza na 8% unakatwa 41200/= @ mwezi kulipa milioni 20 aisee tulikuwa tunaiona miaka kama 15 mbele yetu ila kwako ni 5-7 inatosha
 
Ushauri Kama una mtoto ebu jaribu kumuandalia mazingira ya ada ya elimu ya juu hapo baadae kwa kuweka akiba asilimia 15 Kama ilivyokua unakatwa na heslb hivyo iwe Kama mwendelezo wa makato
We jamaa umetoa bonge la ushauri ngoja ni i screenshot Kabisaa be blessed man
 
U mean ...Kama kwenye salary slip deni limekwisha badae watakuja Tena kulirejesha ? Ufafanuzi please!
Yaani iko hivi Deni lililo kwenye salary slip ndo deni halisi ulilokopeshwa ila hilo deni lina penati na value retention fee inayozaa kila mwezi hivyo makato ya kwenye salary slip yakiisha baadae watakuja kuweka hayo mengine ya penati na value retention fee.
 
U mean ...Kama kwenye salary slip deni limekwisha badae watakuja Tena kulirejesha ? Ufafanuzi please!
Sidhani kwa marekebisho waliyoyafanya heslb
Nakumbuka niliwahi kwenda ofisini kwao nikawaomba statement ya tangu nianze kuchangia mwaka 2012 mpaka nilipokwenda yaani mwaka jana 2019.
Nilichokiona makato yanaendana jumla kuu ambayo inahisisha value retention fee,penalty(10%)na mkopo wenyewe.
Hakuna huo utaratibu wa kulipa mkopo kwanza kisha baadae makato mengine.
Swali hili nijihoji na nikapewa majibu kuwa hakuna makato mara mbili.Ila ni vyema kama una mashaka ukienda kuomba statement yako.
May take.
Nilipokwenda kwa sababu kuna miezi Heslb walikuwa wakitukata hela kama kawaida ila walikuwa hawabadilishi outstanding loan" deni l linabaki vilevile bila kupunguza ingawa wanakata".Suala hilo walilirekebisha na walikiri kuwepo kwa hitilafu hiyo.
Tupende kufuatilia.
 
Yaani iko hivi Deni lililo kwenye salary slip ndo deni halisi ulilokopeshwa ila hilo deni lina penati na value retention fee inayozaa kila mwezi hivyo makato ya kwenye salary slip yakiisha baadae watakuja kuweka hayo mengine ya penati na value retention fee.
Mkuu kuna cumulative value retention na inawekwa katika kasima yake
 
Yaani iko hivi Deni lililo kwenye salary slip ndo deni halisi ulilokopeshwa ila hilo deni lina penati na value retention fee inayozaa kila mwezi hivyo makato ya kwenye salary slip yakiisha baadae watakuja kuweka hayo mengine ya penati na value retention fee.

Ni bora uende physically ukapate status yako HESLB, mara nyingi huwa likiisha kwenye salary slip na ukakaa kimya unaweza kuja kuletewa deni jipya muda umeenda sana na limekuwa kubwa.
Mi nawashauri ambao bado wanalipa deni kwenda ofisi za HESLB kila mwanzo wa mwaka ili kupata status mpya na kuipeleka kwa mwajiri ili afanye update ya deni lako kwenye LAWSON. Hii inakusaidia kujua mwenendo wa deni lako.
 
Back
Top Bottom