Asante Mungu, deni la HESLB limekwisha

Asante Mungu, deni la HESLB limekwisha

Wakuu hopefully mko salama

Haikuwa kazi rahisi, Ila atimaye my salary slip haisomi tena makato ya higher education student loan board (HESLB).

Baada ya msoto wa makato kwa muda wa miaka 5 ndani ya nyavu za Bodi ya mikopo, hatimaye deni hilo limekwisha na hati ya mshahara ya mwezi wa tano ime-decrare the deduction is off.

Japo nilitambua umhimu wa malipo hayo, Ila kiukweli, makato hayo yalikuwa mzigo mkubwa na mara nyinyi yalininyima usingizi.

Natambua nimetimiza wajibu wangu wa kulipa mkopo ulionisaidia kupata elimu ya juu. Nitumie wasaha huu pia kuwashukuru wananchi wa Tanzania kupitia serikali ya Tanzania, kwa kunipa fursa ya kujielimisha kwa level of my first degree kupitia kodi za watanzania.

Niombe serikali iendelee kutoa fursa hii kwa vijana wa kitanzania ili wafikie ndoto zao za kujielimisha. Hata ivyo, kwa wazazi wenye uwezo usiruhusu mwanao kumbebesha mzigo huu wa deni la elimu ya juu. Hakika unachosha na kuvujisha jasho kwa kijana ambaye ndo kwanza anaanza maisha.

Mwisho kwa wale ambao mmeshamaliza deni la HESLB naomba kujua taratibu ya kupata loan clearance certificate, coz Kuna rafiki yangu mmoja amenishitua kuwa unawaza ku clear deni kwenye salary slip Ila ukienda bodi ya mkopo unaweza kuta bado unadaiwa, hii imekaaje wakuu?
Hongera mkuu naona nami niko mbioni ntafuatilia majibu ya clearence certificate
 
ila itakuwa vyema na ukitupa feedback kidogo ili uwape picha na wengineo mfano ulikuwa unadaiwa jumla ya deni la sh ngapi?, ulikaa miaka mingapi baada ya kugraduate ndio ukapata ajira, vipi penati je?, kwa mwezi walikuwa wanakata kama sh ngapi? vitu kama hivyo
 
Hongera kwa kumaliza deni. Kuhusu hiyo paragraph yako ya mwisho, Mungu anisaidie! Kamwe sitaenda kuchukua hiyo clearance form!

Hao Helsb ni VIBAKA! Kuna wakati niliwajaribu kwa email wanipatie taarifa za deni langu, waliniletea deni tofauti kabisa na lile la kwenye Salary Slip! Nikajiuliza hivi kuna Bodi za Mikopo mbili nchini?

Nashukuru Salary Slip ilisoma 0 miaka kadhaa iliyopita. Ila kusema niwafuate ili wanibambikie deni hewa, hilo wasahau. Hiyo clearance form wabaki nayo tu kama ukumbusho.
Was thinking the same thing, but what if they will reclaim back the loan and cause unnecessarily disturbance later ? I think I have to face them and get the clearance certificate immediately.
 
Was thinking the same thing, but what if they will reclaim back the loan and cause unnecessarily disturbance later ? I think I have to face them and get the clearance certificate immediately.

Mimi nina salary slip zote! Kuanzia siku deni linaanza, mpaka lilipoisha. Sasa siku watakayokuja na hilo deni la kunibambikia, tutaenda kushindana mahakamani.

Wataniambia wamelitoa wapi na ni kwa nini halikuonekana kuanzia mwanzo kwenye salary slip zangu.

All in all, iwapo Mungu atanijalia uzima nimeapa watoto wangu sitakubali nao waingie kwenye huu mtego. Bora niwasomeshe mwenyewe mwanzo mwisho!
 
Yaani mi mwezi wa kumaliza hilo deni nakwenda kufungua akaunti wakate kiasi hicho kwa ajili ya dogo janja hapo baadae mana nishazoea kuishi kwa 85%
 
Wasiliana na zonal offices kwa sehem uliyopo wao watakupa clearance certificate. Mie nimemaliza mwez wa pili bad luck nilichelewa kutumiwa clearance certificate hivyo ofisini kwangu wakaendelea kunikata, nilikatwa mwez March na April so ni zamu yangu sasa nawadai bodi ya mikopo japo sina uhakika wa kupata pesa yangu.
Wasiliana na zonal offices kwa sehem
uliyopo wao watakupa clearance certificate. Mie nimemaliza mwez wa pili bad luck nilichelewa kutumiwa clearance certificate hivyo ofisini kwangu wakaendelea kunikata, nilikatwa mwez March na April so ni zamu yangu sasa nawadai bodi ya mikopo japo sina uhakika wa kupata pesa yangu.

Pesa yako utapata mkuu, wewe andika barua ya kuelezea issue yako na vielelezo utakavyotakiwa kuambatanisha.Mimi nilirudishiwa makato yaliyokuwa yamezidi japo utasubiri 3-6 months.
 
Mimi nilianza kukatwa mwaka 2012
Mpaka leo ni miaka takribani minane (08) na nilikopeshwa kwa means test 80% ila nahisi mwezi huu wa tano nimemalizana nao.
Victor Wilbard Mlaki Deni lako Bado ukimaliza Hilo kuna Deni la Value Rention Fee na riba vitaanza kukatwa ukimaliza Deni lililo kwenye salary slip.
 
Hii ni kozi gani
Yaani acha tu! Kuna watu karibia wanachanganyikiwa wakisikia Bodi. Mtu anadaiwa 60+m, na anakatwa 149,000 kwa mwezi.
Anayarajia kulipa deni kwa takribani miaka 33+ (kama makato hayatpongezeka sana).
Kadiri ya umri wake, atastaafu na labda mafao yamalizie deni.
 
Serkali ifanye ingeondoa riba ya deni ili watu wakianza kulipa usiwe shida
 
Victor Wilbard Mlaki Deni lako Bado ukimaliza Hilo kuna Deni la Value Rention Fee na riba vitaanza kukatwa ukimaliza Deni lililo kwenye salary slip.
Nilishaomba statement nikaona mtiririko wote wa deni langu ambapo niliona kiasi cha mkopo,kiasi cha penalty (10%), kiasi cha value retention fee na jumla kuu.
 
Ulikuwa unakatwa kiasi gani kila mwezi?
Mimi naamini kama Serikali hii isingekuwa na majizi na mafisadi bado elimu ya juu ingeweza kutolewa BURE kwa kila Mtanzania anayefanikiwa kufika huko.
Maccm hayawezi kukubali hilo
 
Niombe serikali iendelee kutoa fursa hii kwa vijana wa kitanzania ili wafikie ndoto zao za kujielimisha. Hata ivyo, kwa wazazi wenye uwezo usiruhusu mwanao kumbebesha mzigo huu wa deni la elimu ya juu. Hakika unachosha na kuvujisha jasho kwa kijana ambaye ndo kwanza anaanza maisha.
Ni kweli kabisa. HESLB ni mzigo mkubwa sana. Kama unaweza kuukwepa, ukwepe kabisa
 
Back
Top Bottom