Habari ya Jumatatu wana ndugu wote.
Niaze na kumshukuru mungu kwa afya njema alio nijalia neema hii. Pia nimshukuru M/Mungu kwa kunipa mke bora na sio bora mke.
Kiukweli wanawake wanamapungu mengi lakini sio wote. Wapo ambao wanajitambua na kujielewa kama ambavyo wanaume walivyo. Kuishi na mwanamke kunahitaji HEKIMA, BUSARA, NA USTAMILIVU. Ukiwa hivyo utaishi nae kwa wema na amani upendo utaongezeka. Kiukweli mke wangu ni miongoni mwa wanawake wenye upeo na busara kubwa, kiasi ambapo najivunia kua nae. Amekua na mchango mkubwa ktk maisha yetu.
Kiukweli sijawahi kugombana naye wala kumuhisi chochote, amekuwa ni mtu makini, anayetumia busara kubwa katika maamuzi yake. Amekua mcheshi mno , mwenye tabasam kila nikimuona nahisi furaha sana. Pia nami najisifia kwa kuweza kumuendo mke wangu, na kumfanya awe bora.
Tatizo la sisi wa baba tunapo kuwa katika maisha ya ndoa hua tunatumia mfumo dume, mfumo kandamizi, mabavu. Hali hii inafanya wamama kujiona vijakazi mwishowe nao hufanya watakavyo kwa kukosa busara, hekima kwa wanaume wao.
M/Mungu alituagiza tuishi nao kwa akili, alikuwa anajua wao ni watu wa kuelekezwa bila ukali, watu wa kuwapa nafasi nao watoe maoni yao. Na hata ukiwapinga basi tumia akili kumpinga na fosi, nguvu wara kejeri.
ASANTE MKE WANGU KWA KUNIPA WATOTO, ASANTE MKE WANGU KWA KUNIJENGEA HESHIMA.MUNGU IBARIKI NDOA YETU.
Sent using
Jamii Forums mobile app