Uchaguzi 2020 Asante kwa kuja; Fikisha salamu zetu kwa Robert Amsterdam na wenzake

kajekudya

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
2,469
4,904
Zipo taarifa ambazo wewe mwenyewe umezithibitisha kuwa mara baada ya Uchaguzi utarudi Ubelgiji, huko ulipokuwa kwa takribani miaka mitatu na kurudi siku chache kabla ya zoezi la Uchaguzi mkuu kuanza. Ni jambo jema kuwa ulijua huwezi kutoboa na ukafanya maandalizi hayo mapema.

Sasa sisi Watanzania tunao utamaduni wetu, utamaduni adhimu sana, tunapopata mgeni basi wakati wa kurudi hupenda kumumtuma salaam ili kuwapelekea wale aliowaacha huko! Basi nasi Watanzania tunakutuma salaam hizi.

1. Mwambie Robert Tanzania ni nguli katika siasa, Mwambie hadi mda huu ina vikoloni vyake inavitawala. Mpe ukweli kuwa Rais wa Tanzania hupatikana Tanzania, pale Dodoma na si kwenye hoteli za nyota tano huko Brussels, New York, London au Paris. Mkumbukeshe kuwa Watanzania wana utamaduni tofauti kabisa na ule wa zile nchi zilivyotawaliwa na Ubelggiji na Ufaransa ambazo Marais wake bado wanaamriwa Brussels na Paris.

2. Mkumbushe Watanzania wanaamini bado katika Ujamaa, umoja na kujitegemea. Waambie wanajua kuwa Mabeberu hawajawahi kuwa watu wema kwao na wanacheza nao kwa tahadhari. Waambie Watanzania linapokuja swala la maslahi ta Nchi huwa kitu kimoja, huachagua Maslahi ya Nchi bila kujali gharama zake, Mwambie uzalendo bado umetamalaki!

3. Mwambie na hii kwa Kumnong'oneza, kuwa vyama vya upinzani kikiwemo hicho chako ni vimatawi vya Chama na shughuli zake zinaratibiwa na kitengo, ndio maana ni vya msimu vinapanda na kushuka. Mwambie hata Chairman wako na Mtendaji mkuu wako ni waajiriwa watiifu. Mwambie hata huyu Sheikh na huyu Askofu nao ni waajiiriwa watiifu ndio maana wamewekwa karibu yako kipindi hiki, hawa ndio watakaomaliza mchezo. Mwambie mfumo wa siasa na ulinzi wa Tanzania ni very complex. Mkumbushe sarakasi za Mbobezi, Mkumbushe pia kuhusu yule kipenyo aliyewahi kupenya hadi ngazi ya Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa

4. Waambie kuwa kwa mjibu wa utaratibu wa Uchaguzi Tanzania hakunaga Mpinzani wa kudumu, ila wapo wa Msimu, hivyo na wewe ulikuwa wa Msimu huu tu, Msimu ujao atatengenezwa Mpinzani mwingine, waambie wakutafutie kazi nyingine kabisa. Wakumbushe kuwa hata wewe ulitengenezwa ili kuhahakikisha Lowassa anasahaulika vichwani mwa Watanzania na kura zake millioni 6, kazi ambayo umeifanya kwa uaminifu na kwa uadilifu, Lowassa Sasa yupo CCM baada ya kupuuzwa, hiyo yote ilikuwa kazi yako. Hivyo waambie kuwa Mara baada ya Uchaguzi ataandaliwa Mpinzani mwingine ili kuhakikisha wewe unafifia.

Tafadhali Fikisha salamu zetu na Asante kwa kuja.
 
CCM turufu iliyobaki ni kujaribu kubia kura tu kwa kutumia Police na baadhi ya wafanyakazi wa Tume wasio waaminifu, ila this time mtadhibitiwa na mtaumbuliwa!! Kwa ushahidi mkubwa tumeona mkikataliwa kote muendako, mgombea wenu ni kama ana roho ya kukataliwa vile sijui kamkosea nini Muumba wake kumpa mzigo huo mzito mgogoni.

Lissu anakwenda kushinda mapema, ni 70% win. Ushindi mnene kabisa!! Mwambieni baba yenu aanze kuaga mapema sababu akigoma yatamkuta makubwa !!
 
Watanzania tujitokeze kwa wingi tukamuadhibu msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji kesho
NAKUBALIANA NA WEWE. HIMA WATANZANIA KESHO TUJITOKEZE KUWAADHIBU HAWA MABEBERU NA VIBARAKA WAO. TWENDE KUPIGA KURA MAPEMA TUU ILI IFIKAPO SAA 10 JIONI WAISOME NAMBA. YAAANI IIIIIIIIIIIIIIIII.... WANADHANI SISI NI WAJINGA SAAAAANA. ETI MIRADI YA UMEME, BARABARA, RELI, NK. SI KITU!!!!! WAMETUTUKANA. ZAWADI YAO NI KURA ZOTE KWA CCM.
 
Zimbabwe ilianza kwa mchezo Kama huu.mwisho wake Robert Mugabe alibakia na familia yake na kuichia nchi matatizo makubwa Sana.
Zimbabwe ni different story.
Wakulima wazungu wengi wao wenye asili ya Uingereza walinyanganywa mashamba yao bila fidia.

Serikali ya Mugabe ikayagawa mashamba kwa marafiki zake badala ya wananchi waliokuwa hawana ardhi.

Waliopewa mashamba waliuza vitendea kazi,hadi mbegu,wakakosa maarifa ya kilimo yakawashinda kuzalisha mazao,nchi ikakubwa njaa.Wananchi wakaandamana kudai chakula,Nchi za magharibi zikaiwekea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi

Mzee Mugabe alikuwa amezeeka mno ameishaishiwa kumbukumbu na mkewe akajipachika madaraka akatawala nchi hiyo kiimla.
 
Zimbabwe ni different story.
Wakulima wazungu wengi wao wenye asili ya Uingereza walinyanganywa mashamba yao bila fidia.

Serikali ya Mugabe ikayagawa mashamba kwa marafiki zake badala ya wananchi waliokuwa hawana ardhi...
Clear and Loud
 
Hili limekaaje,Yaani tundu lissu na akili zake timamu,abebe maneno ya mtu asiye na akili timamu aende kuyapeleka kwa mtu mwenye akili timamu.
 
Back
Top Bottom