Asante JPM kwa kutufundisha vitu viwili Imani na kuwa na Msimamo usioyumbishwa

eliamero

New Member
May 2, 2012
1
20
Watanzania tunayobahati kwa Mungu kuruhusu Magufuli kuwa Raisi wetu. Nakumbuka kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 katika nyumba za ibada kulikuwa na maombi maalum yaliyo kuwa yakifanyika kwa ajili ya kumpata rais ajae wa Tanzania baada ya uongozi wa awamu ya nne. Nipende kusema kuwa sala na maombi yaliyofanyika Mungu alisikiliza na kuyajibu kwa kuruhusu Magufuli awe raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Uongozi wa raisi Magufuli umeifundisha Dunia mambo makuu makubwa mawili:

1. Kumtegemea Mungu ni jambo la kwanza kwa mwanadamu yoyote kwani maarifa, science, busara na hekima zinatoka kwake.

Kati janga la korona tumeona namna ambavyo raisi wetu alisimamia/anavyosimamia imani. Raisi alionyesha/anaonyesha kiwango kikubwa kabisa cha imani kwa Mungu. Anafundisha kuwa kama Mungu anasema 'Njooni kwangu ninyi nyote mnaoelemewa na kusumbuliwa na mizigo nami nitawapumzisha'

Iweje leo kwa sababu tu ya Korona raisi aamuru au ahimize kufunga Makanisa na Misikiti?

• Watu washindwe kumwabudu na kumwomba Mungu kuwaondolea magumu mbalimbali wanayokutana nayo katika maisha.
• Watu wakose huduma ya kiroho kutoka kwa viongozi wao wa dini
• Watu wakae majumbani wafe wakiwa katika dibwi la dhambi kwa kukosa huduma ya injili kutoka katika madhabahu ya Bwana.

Raisi ni mwanasiasa lakini katika janga la korona Mungu anamtumia kama mtumishi na kupitia yeye wengi wamekua kiimani. Kumbuka maneno ya Mungu yanasema 'atakae kuiokoa nafsi yake ataingamiza, nae aliye tayari kuipoteza kwa ajili yangu ataiokoa'

Mapambano ya korona kwa Tanzania yametanguliwa na Maombi. Maombi yanatangulia ili kufungua maono ya kisayansi na ugunduzi na njia mbalimbali za tiba pamoja na kinga. Rais alihimiza watanzania Wote kuomba kwa siku tatu wakati wa kuanza mapambano na amehimiza kumshukuru Mungu kwa siku tatu kwa mambo makubwa aliyotutendea.

Ubinafsi wa mwanadamu unaonekana pale anaposhindwa kusimamia imani yake kwa kuwa na woga wa kudhurika wakati akiitetea imani Kanisani au Msikitini. Kwa hili JPM ametuonyesha njia. Naamini hata viongozi wa dini wamejifunza jambo kubwa.

2. Jambo kubwa la pili tulilojifunza kwa raisi Magufuli ni Msimamo usioyumba
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna kipindi kwa hivi karibuni kwa viongozi wa nchi mbalimbali kilichokuwa na maamuzi magumu kama hiki kipindi cha korona. Kupigana na adui asie onekana kwa macho na usiekuwa na uzoefunae na usiekuwa na uhakika na taarifa zinazo mhusu.

Kila nchi ilikuwa na wakati wa kujitafakari na kufanya maamuzi. Hapa tuliona nchi mbalimbali duniani zikichukua hatua kali za kufunga shughuli mbalimbali na kutaka watukukaa ndani. Tuliona/tunaona ushawishi wa kila namna ukiwemo wa mikopo kutoka WB ili nchi kuchukua hatua kali hata kama haziendani na uhalisia wa mazingira baina ya nchi na nchi. Baadhi ya viongozi wali copy na kupest njia za mataifa Mengine.

Kwa Tanzania Raisi wetu alisimamia/anasimamia maono na kile anacho kiamini. Tukumbuke suala la imani aliyo nayo raisi wetu na ukumbuke kuwa maarifa yanatoka kwa Mungu. Naamini imani inamwezesha raisi wetu kupata maono na kuweza kuyasimamia.

Tulisikia kelele nyingi huku wengi wakidiriki kutudhalilisha kwenye media mbalimbali na kuona sisi hatufai na ni watu wasio jielewa. Tumshukuru jemadari wetu kwa kutoyumba wala kusumbuliwa na kelele kwani nyingi zilijikita kutuonea huruma (masilahi binafsi) kwa yatakayo tukuta kisa tunamshirikisha Mungu na kuendelea kusali Makanisani na kwenye Misikiti pamoja na kufanya shuhuli zetu za kila siku.

Raisi wetu linapokuja suala la nchi yupo tayari kupoteza hata marafiki zake wa karibu. Tunaona ni jinsi gani katika suala la korona raisi anavyo tanguliza maslahi ya nchi yetu mbele bila kuyumbishwa. Kuwa na msimamo kwa kile anachokiamini ni jambo la kuigwa na kila Mtanzania.

Mwisho.
Prof Lumumba alitumia msemo wa Magufulification of Africa. Ni ukweli usio pingika kuwa Afrika tunahitaji Magufuli wachache tu kuweza kubadilisha kabisa mtazamo wa dunia kuhusu Waafrika.

Niwasihi watanzania, raisi Magufuli anahitaji kuungwa mkono. Tujiunge wote kama taifa kumwomba Mungu azidi kumlinda raisi wetu. Tukatae kuwa watumwa wa fikra, kwa kuona kuwa ilitujikwamue kutoka katika janga lolote hususan korona lazima tusaidiwe kama walivyokuwa wana tuhadaa baadhi ya viongozi wa kisiasa.

Tupambane kwa pamoja , pale tunapoona changamoto tusiwe wepesi kushutumu tusonge mbele. Namwona raisi Magufuli akitufanya watanzania kuwa watu wenye heshma duniani. Nawaona viongozi wa Africa wakibadilika kifikra kwa chachu inayosambaa kitovu chake kikiwa ni Tanzania.

Mungu mbariki Raisi wetu na mpe ujasiri wa kuendelea kutenda makubwa katika nchi yetu. Simama nae usimwache pekeyake anapopambana kutukomboa kiuchumi na kifikra. Mungu ibariki Tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom