Asante Hillary Clinton na Obama waafrica wanauzwa katika soko huru Libya

IGaddfi alikuwa mnyama hakufaa kuongoza, kuondolewa Gaddafi kumesababisha nchi iwe ya unyama zaidi kwa sababu kuna power vacuum katika nchi yenye wahuni wengi, watu wa West walitumia mwanya wa ubinadamu kumuondoa Gaddafi kwa sababu zao na Gaddafi aliwapa sababu za halali za kumuondoa kwa ujinga wake wa kusema atawafuatilia wapinzanibwake nyumba hata nyumba kuwafanyia kitu mbaya.

Kusema Gaddafi alikuwa kiongizi mzuri kwa sababu kawalipa watu posho wakati kaua wa Libya kibao ni kutielewa mauaji aliyoyafanya Gaddafi. Gaddafi kaua watu wengibsana Libya. Gaddafi kabsponsor terrorism dunia nzima.

Jamani someni hivyo vitabu ndiyo tuje tujadiliane kwa sababu kwa sasa naona kama najadiliana na mtu ambaye hana habari kamili na anamtetea Gaddafi kwa mahaba tu.
Tumevisoma mkuu, ila sidhani kama ilikuwa njia bora kumuondoa, yale yale ya Iraq, mauaji yanayotokea sasa ni mara 10 zaidi..Wapi na wapi?! Wangewaachia wananchi wenyewe waamue, sivyo hivi..
 
Tumevisoma mkuu, ila sidhani kama ilikuwa njia bora kumuondoa, yale yale ya Iraq, mauaji yanayotokea sasa ni mara 10 zaidi..Wapi na wapi?! Wangewaachia wananchi wenyewe waamue, sivyo hivi..
Nchi zinastahili kuwa na viongozi bora kabisa wanaowezekana kuwepo?
 
Demokrasia huwa sio suluhisho la matatizo ya nchi. Tatizo ni endapo mtapata dictata mjinga ambaye hafanyi mambo ya maendeleo anambwelambela tu. Ila kichwa kikipatikana mambo huwa safi
 
Kwanza nianzie kwa kusema sikukubali utawala wa Obama nchini USA, Hata kipindi anagombea mara ya kwanza mwaka 2008 kuna waafrica wasiojitambua walidhani akiwa rais basi mambo mengi ya Africa yamenyooka , mpaka wengine walijiarika katika kuapishwa kwake mambo ya aibu kabisa,

Obama kalikuwa kanafiki sana na mkitaka kujua kwamba matatizo mengi ya Africa kamesababisha aka kazee,

Kitendo cha kuivamia Libya na kumuondoa Qhadafi kimesababisha matatizo mengi mno, ona sasa Libya wamekosa cha kufanya mpaka wanahisi kuuza binadamu ndo itawapatia hela,

Kwa kushirikiana na.Clinton kalihakikisha kwamba Libya inakuwa dismantled,

Nashangaa vyombo vya habari vya USA havijaongelea suala ili hasa vile alivyokuwa anavitumia Hillary Clinton kumchafua Trump, mbona wako kimya? Wanajua huyu mama pia ni bomu,

Upande wa viongozi wa Africa nao wamekaa tu wanakula kodi za wananchi, yaan sioni maana ya muungano wa nchi huru za Africa, ni unafiki tu,

Magufuli nawewe hujatoa neno juu ya mauaji hayo na uuzwaji wa watu Libya,
Pitia video ya mnada ni dk 2


Weka bundle ya kutosha uone mambo hapa ni hatari



Brittany

then bado kuna makondoo ya kiafrika bado yawafagilia hawa waarabu.
 
Ww umeng'ang'ania umesoma umesoma , ukweli huko wazi , kwani aliyeandika vitabu si binadamu ? Yaani Leo mtu akiandika kitabu kuwa tz ndio nchi yenye maisha bora kuliko Sweden utaamini ? Kwa kuwa ameandika
Wewe hujui tofauti ya "uko" na "huko", halafu unataka kujadili utawala wa Gaddafi na usahihi wake?

Hapo tu unanionesha huna uwezo wa kujadili unachotaka kujadili.
 
Huwa sijui kwa nini hao walipoanza kumsumbua Gaddafi iliniuma.. na hadi leo yanayojiri nchini humo yananisikitisha sana.

Inasikitisha kuona hata hawakimbiliii kuwasaidia hao wanaotaka kwenda majuu kwa kupitia nchi hiyo.. huku tangu enzi za Gaddafi walipita pia kama kawaida na hatukusikia haya ya mnyanyaso kwa levo hii ya sasa hivi.
Hakika
 
Back
Top Bottom