Matajiri wako kila mahali duniani lakini hawachangii maendeleo ya nchi zao-Hillary Clinton

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,987
22,515
Huyu mama kuna uwezekano mkubwa akawa rais ajaye either baada ya Obama ama Romney.Ila ninaamini itakuwa Obama.

Sisi wengi wa matajiri wetu ni mafisadi.Sisemi kuwa ni wote.Lakini ninavyofahamu,hata ufisadi ulikuwepo USA before,lakini uzuri wake ni kwamba walilisadia taifa miaka ile ya nyuma especially after the "Gilded age",watu kama kina rockefeller na wengineo ambao walikuwa mafisadi wakubwa,lakini kabla ya kubanwa,waliamuwa kukubali mabadiliko,na kuzitumia mali hizo kwa manufaa ya taifa lao.(ninayo mifano ama soma kuhusu Gilded age)

Marekani,kuna watu wameutumia mfumo wa ubepari kujitajirisha,lakini mfumo wa ubepari umewafanya wasiwe na huruma hata kidogo,na kuona kwamba huo utajiri wameupata kama vile hata masikini hawakuhusika.Hilo lilibadilishwa na federal government na ndiyo maana matajiri wana bifu nayo hadi leo.

Sasa wanaita regulations wanapobanwa haswa kuhusu kodi, na mara pengi kuzihusiha na socialism ama communism.Lakini ni ukweli ulio wazi kuwa Taifa la marekani bila kodi hizo lisingekuwepo hapa lilipo.Pia bila kuziba mianya ya ufisadi.

Sisi bado hatujajifunza na hata hatujafikia Gilded age kama wao.Kama ni maisha ya binadamu,tukijifananisha,level waliyoko wao ya kibepari,ni kama mtu mzima aliyezeeka na sisi ni kama mtoto anayetambaa.

Tatizo la kuiga kwetu,ni kwamba tunataka kumkimbiza mtoto anayetambaa kwa kujilinganisha na wao bila kujuwa kuwa ubepari nao una stages.Hilo linatufanya tusijuwe cha kufanya kuhusu mafisadi wetu na pia ukusanyaji kodi.

Sitaki kusema mengi kwa sasa,however cha muhimu,ni kwamba sisi ambao tunaufuata mfumo wa ubepari,hatujui kwamba ni mfumo ambao kuna wakati viongozi wanaingia madarakani kwenye mataifa hayo ya kibepari na kujaribu kuudhibiti ulafi wa mabepari,tabia ambayo ndiyo haswa msingi wa ubepari,yaani "Profit maximazation", bila kujali consequences ie slavery ama hata voluntary slavery na underpaid labors...kama ubepari ungeachiwa bila kudhibitiwa na serikali,basi hata utumwa ungelikuwepo hadi leo.

Tabia hiyo inapelekea kutokuajali na wakati mwingine kuhalalisha mambo ambayo kiutu ama kiubinaadam yanonekana kama ni "unyama" na kutokujali kuhusu maisha ya wengine.Kwa kifupi,iliwahi kutafsiriwa kama "The fittest survives"

Nataka niwaambie wana jamvi wenzangu,kuwa kwa wenzetu kuna kitu kinaitwa regulations.Kitu hicho miaka ya nyuma kilitafsiriwa kama vile ni usoshalisti ama ukomunisti.Sasa mambo yamebadilika.

Wenye kufuatilia siasa za marekani ambapo kuna mvutano huo uliopelekea mabepari wake waache kuwekeza kutokana na sera za Obama wanazoiita za kisoshalisti kwasababu ya regulations na kutaka matajiri walipwe kodi zaidi,wananchi wameamka na hawasikilizi hizo propaganda tena.Na ndiyo maana kuna mwamko miongoni mwao.

Kwasababu ya ukomavu wa kisiasa,ndiyo maana yale ambayo yangeliweza kuwa revolution(occupy wallstreet),yameweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa.Hilo limewezekana kutokana na wao kujenga mfumo ambao kuna vyama viwili tu vikubwa vyenye kupingana,pamoja na willingness ya kukubali kufanya mabadiliko bila umwagaji damu.

Kwanza niishie hapa kwa kusema hivi;Hata mama Clinton ambaye ni mfuasi wa ubepari,ameonyesha kwamba dunia ya sasa inahitaji mabadiliko.Siyo kama dunia ya zamani ambapo mafisadi (kwa upande wetu),na matajiri kwa upande wao,walilindwa.

Nasema hayo kwasababu sisi matajiri wetu wengi ni mafisadi,na wasio mafisadi ni wachache. Hilo limetokea kwa kuwa tumeuiga mfumo wa kibepari na walionufaika moja kwa moja ni viongozi wa kisiasa tofauti na wao.Wao kipindi kile ni kwamba wanasiasa walisaidiwa na mafisadi na siyo kwamba wanasiasa ndiyo walikuwa mafisadi.

Lakini kwetu wenye kutaka kuendelea kuwa madarakani,ni mafisadi,yaani wanasiasa ndiyo mafisadi wenyewe.Hilo linapelekea wao kuficha pesa.Kwa wenzetu,walizitumia ili kuwasaidia wanasiasa.Hilo bado lipo somehow.

Kwetu sisi,matajiri wako lakini hawana nguvu kama mafisadi.

Kwa wamarekani,kuna matajiri pia,lakini walianza na mafisadi,ila kuna matajiri ambao wako kwenye msimamo mmoja na mafisadi.Tofauti kubwa tuliyo nayo,ni kwamba mafisadi wao walikuwa ni zamani wakati ubepari ndo unaanza,wakina Carnegie, Rockefeller et al.Hao badala ya kunyongwa kama uchina,walijikuta wakitumia mabilioni yao kujenga nchi(ili kuwaokoa wanasiasa wasikose kura).Hilo liliwaokoa wansiasa hao(refrence to Chicago politicians).

Ujumbe wa mama Clinton ni wa kujifunza.Dunia imebadilika.Watu wanajilimbikizia mali bila kujali kuwa kuna masikini na kwamba dunia inahitaji mabadiliko.Tatizo ninaloliona,ni kwamba mafisadi wetu hawahitaji kubembelezwa kwasababu wana roho mbaya na ni wabinafsi.

Na ndiyo maana pesa zao wanaziweka uswisi na wala hawazifanyii shughuli za kujenga uchumi wala taifa.Kwa wenzetu enzi zile hawakufanya hayo.Ila kwasababu sasa hivi wanazipeleka huko uswisi pamoja na kupeleka biashara nje ili kukwepa kodi,basi ndiyo maana wanapigiwa kelele.

Kwa hali ilivyo,itakuwa vigumu sana kwa matajiri kuchukua uongozi wa nchi yao.Kwetu sisi matajiri ni mafisadi,na hivyo sichelei kusema kuwa ni vigumu kwa mafisadi kuchukua nchi,labda wachakachue.

Mwelekeo wa dunia kwa sasa ni wa tofauti taka wasitake mafisadi,hawawezi kuchukua madaraka kwasababu hata hao wafadhili wetu ambao wanajuwa jinsi ufisadi unavyoanza,wanaona kabisa kuwa mafisadi wa Afrika hawana manufaaa na wananchi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo mafisadi wao walichipukia.

Ni bora tufahamu kuwa walipopitia wao,sisi ndo tunapitia sasa hivi,hilo siyo siri,kwasababu mfumo wa ubepari sisi ndo tunauanza sasa hivi,lakini wao waliupitia karne nyingi zilizopita.Lakini sisi kwa kutokufahamu,tumeuiga mfumo wao bila kujuwa kwamba walifanya vitu gani kwenye stages za mwanzo za mfumo huo.

Hawakunyonga watu kama uchina,lakini mafisadi walikuwa responsible kulijenga taifa lao kwa fedha hizo walizozifisadi.Nitaweka mifano hai kama kuna ambao wanahitaji.Ama nitafanya hivyo kadri mjadala utakavyoendelea.

Kwasababu sasa kwa mabepari waliobobea kwenye mfumo wao hawaitwi tena mafisadi kutokana na mabadiliko waliyoyafanya na kuwabana kiaina licha ya kwamba walihakikisha wanatumia utajiri huo kuijenga nchi,sasa kuna vita hivyo kudai eti kuna regulations na hivyo wanadai eti wakatwe kodi kidogo kuliko hata masikini.Na mara pengine wanafungua accounts ama biashara sehemu kama cayman islands na pia kuajiri ama kupeleka bishara zao kwenye cheap labors ie huko India,uchina na kwingineko.Yote hayo ni tamaa kwa mlango wa "Profit maximazation"

Secretary of State Hillary Clinton offered a strongly-worded message to the rich at the Clinton Global Initiative Monday –- help grow your countries.

Mama pia alisisitiza kuwa matajiri na makampuni duniani kote walipe kodi inavyotakiwa ili kuweza kusaidia nchi hizo.Nimesema hivyo kwasababu nilishtushwa sana na kampuni ambazo zinakuja kuwekeza nchini halafu eti hazilipi kodi licha ya utajiri wao.Na hilo limechangia kwenye umasikini wetu.

Kama mataifa tajiri kama USA wanapigia kelele kodi hizo,sisi tumekuwa nani tuwasamehe?Uzuri mmoja ni kwamba mabadiliko hayo yameanzia huko,na sisi tunahitaji kuyafuata.Thanks to Clinton Global Initiative.Wamegunduwa kuwa matatizo yanatokana na matajiri kwa upande wao (kwakuwa historia yao ni richer),na mafisadi kwa upande wetu (kwasababu nchi yetu ni changa ukilinganisha naza kwao), kwenye mfumo wa ubepari ambao ndiyo unaozaa matajiri wakupindukia na pia masikini wa aina hiyo hiyo.(wa kupindikia)

Clinton urged struggling countries to tax equitably and to lean on the wealthy."One of the issues I have been preaching about around the world is collecting taxes in an equitable manner, especially from the elites in every country," Clinton said. “It is a fact that around the world the elites of every country are making money. There are rich people everywhere, and yet they do not contribute to the growth of their own countries.”

Mama Clinton ambaye naamini atakuwa rais ajaye wa marekani,ameweka wazi kuwa matajiri hawafanyi wanachotakiwa kufanya.Kwetu sisi ni mafisadi...

“They don't invest in public schools and public hospitals and other kinds of development internally,” Clinton said of the elite. “So, it means for leaders telling powerful people things they don't want to hear. It means being transparent about budgets and revenues and bringing corruption to light.”

Sipendi kuongezea mengi,link hiyo hapo chini,tujadiliane.

U.N. General Assembly 2012: LIVE video of the speeches - One News Page [US]
 
Kuna mwenye kufahamu kama makampuni ya wawekezaji yanaingia kwenye kundi la hao "wealthy" anaowazungumzia?Maana we are a struggling Nation na misaada inaelekea kuwa itakatwa...
Clinton says the U.S. will help struggling nations become self-sufficient rather than offering traditional aid. She says taxing the wealthy would bolster such growth.
 
Ebu tuangalie jinsi mafisadi wakubwa walivyogeuka kwa msaada wa serikali,wakaamuwa kuijenga marekani,sisi vipi?

Although he stood just under five foot tall, Andrew Carnegie (1835-1919), as a dealmaker and corporate capitalist, consistently outgunned J.D. Rockerfeller and J.P. Morgan, the two other giants of the Gilded Age.
Carnegie was a remarkable dealmaker, salesman and negotiator who outwitted Rockerfeller and Morgan in most of their big deals. He was often unscrupulous. His business dealings were often unethical though not necessarily illegal at the time.
Carnegie is best known as a union buster. Yet early in his career he was lauded when a proposal for a farsighted deal to steelworkers tying wages to profits, so that both the bosses and the workers would share in good times and in bad. The union agreed to cut wages and increase working hours during a market downturn.
However, when the boom time returned, Carnegie reneged on his promises. The steel workers went on strike calling him a liar, hypocrite and scoundrel.
Carnegie believed it was contrary to the "laws of civilization" to pay workers more than the minimum they needed. To pay workers more than they needed was to "encourage the slothful, the drunken and unworthy."
The great benefactor who bequeathed libraries, museums and vocational schools to the nation was happy to see his chief manager call in the Pinkerton guards who fired on striking workers.
President Teddy Roosevelt believed that, "if Carnegie had employed his fortune and his time to doing justice to the steelworkers who gave him his fortune, he would have accomplished a thousand times what he accomplished" with his generous philanthropy.
I agree with Roosevelt. What do you think?
Andrew Carnegie: Master deal maker and robber baron | The Naked Negotiator
 
Back
Top Bottom