Duh pole mkuu ni fundisho hilo
Mimi leo yamenikuta lakini kwa aina nyingine
Iko hivi...
Kwenye biashara nnazo fanya natumia sana Instagram kutangaza na nalipia matangazo mara kwa mara,sasa kuna siku nimeweka hela Kwenye visa card yangu ili niweze kulipia tangazo
Nimeclick confirm payment,ikaonyesha malipo yamekamilika lakini hela haikukatwa kwenye account yangu lakini Instagram inaonesha tangazo limeshalipiwa,tangazo likaendelea kwahyo nikawa nimepata tangazo bure maana hela imebaki
Nilifurahi sana japokua haikuwa nia yangu kutowalipa ni wao wenyewe system zao zilijichanganya
Sasa leo nilitaka nilipie tangazo lingine nakutana na deni ile hela yao ya siku ile ambayo hawakuchukua ndo inabidi niilipe ili niweze kuendelea na matangazo mengine sina namna inabidi nilipe tu japokua inauma