Arusha yaongoza kwa umiliki wa Bastola

Arusha yaongoza kwa umiliki wa Bastola

Mara ya mwisho nilikistua mwaka mpya saa sita usiku.Hii inasaidia sana kupeleka taarifa kwa vijambaz njaa wakiona ungo wa DStv wanajua mwenye nyumba yuko vizuri wanakujaribu lakini wakijua una chuma si rahisi kuyaweka maisha yao reheni.

Chuma chako umemuazima nani?
 
Mkoa wa Arusha waripotiwa kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya raia wanaomiliki silaha aina ya Bastola. Mkoa huo ulio moja ya mikoa ya pembezoni mwa Nchi yaripotiwa kuwa na matukio ya kutishiana bastola hadharani na sehemu za mikusanyiko ya watu.


attachment.php


CHANZO: Mwananchi.


Kwasababu ni mkoa uliojaa malimbukeni na mabilionea wengi.
 
Mara ya mwisho nilikistua mwaka mpya saa sita usiku.Hii inasaidia sana kupeleka taarifa kwa vijambaz njaa wakiona ungo wa DStv wanajua mwenye nyumba yuko vizuri wanakujaribu lakini wakijua una chuma si rahisi kuyaweka maisha yao reheni.


Naogopa sana kumiliki hiko chuma.
Naogopa ndani ya nyumba kuna mtu atakuja kukigusa au kitatumika vibaya.
 
tatizo la arusha ni ushamba,bado wana ujanja wa kizamani kuchomana visu,kutishiana bastola nk.dar pia watu wanazo ila kimyakimya zip6 kwa kazi maalum
 
Mafunzo yangu kidogo ya kijeshi yananiambia milio ya bastola au risasi za Arusha sio milio halisi ya vile vyombo vya ukweli!

Ni wachache sana wenye vyombo vya Ukweli!

Chunguza mkuu!
 
Wakati mwingine ushamba tu. Unakuta mtu hana kumi lakini ana bastola
 
Wakati mwingine ushamba tu. Unakuta mtu hana kumi lakini ana bastola

hahaaa sasa ataibeba wapi maana huwezi kua n mzigo ukapanda hiace.........miaka y 2007 kurudi nyuma wengi waliokua wanamiliki walikua wauza madini mana mererani ilikua na ujambazi.......ila siku hizi mpka wamiliki wa mabucha wanazo huwa najiuliza sana akili zao zilivyozoea kuona damu si itakua majanga.......kiukweli jeshi la police ndio chanzo cha kutoa vibali holela bila kujua hata mtu anaishi wapi
 
ikiwa wamefata taratibu ni haki yao...ikiwa kinyume na taratibu..cyo haki kumiliki silaha kinyume na sheria
 
Back
Top Bottom