Arusha yaongoza kwa umiliki wa Bastola

Arusha yaongoza kwa umiliki wa Bastola

Joined
Mar 2, 2012
Posts
57
Reaction score
17
Mkoa wa Arusha waripotiwa kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya raia wanaomiliki silaha aina ya Bastola. Mkoa huo ulio moja ya mikoa ya pembezoni mwa Nchi yaripotiwa kuwa na matukio ya kutishiana bastola hadharani na sehemu za mikusanyiko ya watu.

attachment.php

CHANZO: Mwananchi.
 
Attachments

  • images (1).jpg
    images (1).jpg
    7.3 KB · Views: 2,102
Kama kuwa na kisu, shoka na panga ni kitu cha kawaida katika familia je kuna tatizo gani familia kumiliki bastola au kwa sababu ni silaha ya moto?
 
Arusha bastola ni kama manati tuu....
 
Arusha kuwa na bastola ni muhimu kwa sababu ya kupakana na Kenya ambako kuna kiwango kikubwa cha uhalifu
 
Mkoa wa Arusha waripotiwa kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya raia wanaomiliki silaha aina ya Bastola. Mkoa huo ulio moja ya mikoa ya pembezoni mwa Nchi yaripotiwa kuwa na matukio ya kutishiana bastola hadharani na sehemu za mikusanyiko ya watu.

attachment.php

CHANZO: Mwananchi.

Mara nayo yaongoza kwa kuwa na mapanga na sime.
Source mimi mwenyewe.
 
Mkoa wa Arusha waripotiwa kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya raia wanaomiliki silaha aina ya Bastola. Mkoa huo ulio moja ya mikoa ya pembezoni mwa Nchi yaripotiwa kuwa na matukio ya kutishiana bastola hadharani na sehemu za mikusanyiko ya watu.

attachment.php

CHANZO: Mwananchi.
Acha wivu kama haujamiliki yako haujipendi..Maminer bila hii kitu hatujiamini ni kama swala mbugani
 
Hii ni kweli nakumbuka mwaka mpya saa sita usiku kila nyumba nilisikia mlio wa chuma nikagundua watu wa A ni makini sana katika eneo la usalama.Kuna kipindi nadhani enzi la RPC Kombe ilikuwa ni rahisi sana kupata chuma ikiwa ulikuwa ukiishi Njiro ili kukabiliana na vibaka wa Ungalimited waliokuwa wakivuka mto Naura na kuingia Njiro kupora hovyo.Enzi hizo Njiro nyumba zilikuwa chahce sana unakuta jirani yako wa karibu anaishi mita 1,500 ! wakikutokea hakuna msaada wa karibu ndio ikabidi tutafute chuma na Mbwa wa ukweli.

Vibaka wa Ungalimited walikuwa wanavamia nyumba tatu kwa siku halafu wako kama 30 wakikuta hadi chakula wanakula hali ilikuwa mbaya sana kidogo nirejee Soweto kwa woga lakini tukagangamala tukaunda vikundi vya ulinzi na baadhi ya watu wakakimbilia kununua bastola.
 
Arusha Kuna wafabiashara wengi wa madini so hiyo ni kawaida na wengi wanamiliki kwa halali tu.
 
ukitaka kujua arusha wengi wanamiliki bastola njoo siku ya mwaka mpya ujionee mwenyewe,
 
Kati ya raia kumi wafanyabiashara sita ni wamiliki wa Bastola
 
Kwahiyo nikija na buku jero naweza pata yangu moja? 👂👂👂
 
Hii ni kweli nakumbuka mwaka mpya saa sita usiku kila nyumba nilisikia mlio wa chuma nikagundua watu wa A ni makini sana katika eneo la usalama.

Chuma chako umemuazima nani?
 
Back
Top Bottom