#COVID19 Arusha: Wananchi wajitokeza kwa wingi kupokea chanjo ya Corona

Laroi Butata

Member
Oct 28, 2020
91
103
Zoezi la kuzindua chanjo kwa mkoa wa Arusha hatimaye limefanyika na wananchi kadhaa kuhudhuria tukio hilo lililofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa ikiwepo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na viongozi wa dini limeshuhudiwa wananchi walijitokeza kwa wingi na hatimaye chanjo hiyo kuisha kwa kituo hicho.

Hapa ni baadhi ya picha wakati wa uzinduzi huo.

IMG_2135.JPG

Mh. John Mongera akiongea na Viongozi na wananchi walijitokeza kupata chanjo, hawapo pichani.

IMG_2137.JPG

Viongozi na wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha alipokuwa akiongea na hadhara kabla uzinduzi wa chanjo hiyo ya uviko.

IMG_2151.JPG
 
Nimeona kichupa cha chanjo kina namba flani flani. Namba hizo nimezifananisha na namba mfano wa cheti kinachotolewa kwa mnufaika wa chanjo. Je huo ndo utaratibu kuwa lazima ijulikane ni mtu flani alichoma chanjo kichupa namba flani?
 
Nilibahatika kuwepo issue ya namba kwenye kichupa kushabihishana na mpewa chanjo sikuiona.
 
Wapi wamejitokeza kwa wingi kama si propaganda za kuhamasisha kuchanjwa chanjo inayotiliwa mashaka duniani kote? Watu watachanja lakini si kwa kasi ya harakaharaka hivyo. Wanasubiria kuona madhara kwa waliotangulia kuchanjwa ndio na wao wakachanjwe
 
Nilibahatika kuwepo issue ya namba kwenye kichupa kushabihishana na mpewa chanjo sikuiona.
Vipi umepewa cheti? Ninapenda kuchua iwapo cheti kinachotolewa kina namba ya kichupa ambacho mtu kachanjwa?
 
Zoezi la kuzindua chanjo kwa mkoa wa Arusha hatimaye limefanyika na wananchi kadhaa kuhudhuria tukio hilo lililofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa ikiwepo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na viongozi wa dini limeshuhudiwa wananchi walijitokeza kwa wingi na hatimaye chanjo hiyo kuisha kwa kituo hicho.

Hapa ni baadhi ya picha wakati wa uzinduzi huo.

View attachment 1878446
Mh. John Mongera akiongea na Viongozi na wananchi walijitokeza kupata chanjo, hawapo pichani.

View attachment 1878448
Viongozi na wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha alipokuwa akiongea na hadhara kabla uzinduzi wa chanjo hiyo ya uviko.

View attachment 1878445
Hao ndo wananchi?mweee
 
Vipi umepewa cheti? Ninapenda kuchua iwapo cheti kinachotolewa kina namba ya kichupa ambacho mtu kachanjwa?
Hamna kitu kama hicho mkuu.

Yaani kinachofanyika wakati unachomwa sindano ya malaria ndicho hicho kinafanyika kwenye covid.

Tofauti ni moja, hii ya Covid19 inanyonywa yote kwenye kichupa na ukipenda unaweza kukiiba kichupa ukaondoka nacho.
 
Na mm hatimaye nimechanja leo.

brazaj umefanikisha?

Hongera sana chief:

Mkuu wangu comment #34 kwenye ule uzi original kuna yaliyojiri. Yumkini Tanzania ni Dar si huku kwingine:

IMG_20210803_193536_570.jpg

Bado ninapumulia mashine ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom