Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,798
Wafanyakazi zaidi ya 200 wa hotel za Impala na Naura Springs za jijini Arusha wameandamana tena katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha, ambapo maofisa wa TRA, NSSF Uhamiaji na Takukuru wanasikiliza kilio chao.
Madai yao wanautuhumu uongozi wa Impala na Naura kushindwa kuwalipa mishahara yao ya miezi mitano makato katika mfuko wa hifadhi wa Nssf kutopelekwa,na mamlaka ya mapato ikidai kodi katika hotel hizo.
Wafanyakazi hao wanamtuhumu mkurugenzi wao Randy Mrema kuwanyima haki yao ya msingi ya Mishahara jambo ambalo limepelekea waishi maisha ya kubaingaiza.
Mapema Leo wakiwa katika ofisi hiyo ya DC walieleza matatizo yao ikiwemo suala la mishahara kutolipwa kwa miezi mitano na baadhi ya wafanyakazi waliopunguzwa hivi karibuni kutolipwa stahili zao.
Mkurugenzi wa hotel hizo Randy Mrema licha ya kupewa barua ya wito katika ofisini hiyo ya DC amekaidi wito huo kwa kisingizio kwamba yupo nje kwenye majukumu ya kikazi.
Hata hivyo baada ya kupigiwa simu na waandishi wa habari alidai yupo safari.kikazi ila alijibu kwa ujumbe wa simu kuwa ofisi hiyo ya dc haina mamlaka ya kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake.
"Nimesafiri kikazi. Hamna haja ya kikao kwasababu kwa mujibu wa sheria ofisi ya Tarafa au ya mkuu wa wilaya haina nguvu ya maswala ya madai. Sehemu zenye nguvu za madai ni CMA, high Court na court of appeals kwa mujibu wa sheria ya section 86(1) of the employment and labour relations Act. 2004. Tulituma pia barua kueleza changamoto, malipo ya watu waliyopewa and sheria ikoje baada ya kushtukizwa na wito wa ghafla."Amesema Randy