ARUSHA: Wafanyakazi Hotel za Impala na Naura waandamana tena kwa Mkuu wa Wilaya, walia njaa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wafanyakazi zaidi ya 200 wa hotel za Impala na Naura Springs za jijini Arusha wameandamana tena katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha, ambapo maofisa wa TRA, NSSF Uhamiaji na Takukuru wanasikiliza kilio chao.

Madai yao wanautuhumu uongozi wa Impala na Naura kushindwa kuwalipa mishahara yao ya miezi mitano makato katika mfuko wa hifadhi wa Nssf kutopelekwa,na mamlaka ya mapato ikidai kodi katika hotel hizo.

Wafanyakazi hao wanamtuhumu mkurugenzi wao Randy Mrema kuwanyima haki yao ya msingi ya Mishahara jambo ambalo limepelekea waishi maisha ya kubaingaiza.

Mapema Leo wakiwa katika ofisi hiyo ya DC walieleza matatizo yao ikiwemo suala la mishahara kutolipwa kwa miezi mitano na baadhi ya wafanyakazi waliopunguzwa hivi karibuni kutolipwa stahili zao.

Mkurugenzi wa hotel hizo Randy Mrema licha ya kupewa barua ya wito katika ofisini hiyo ya DC amekaidi wito huo kwa kisingizio kwamba yupo nje kwenye majukumu ya kikazi.

Hata hivyo baada ya kupigiwa simu na waandishi wa habari alidai yupo safari.kikazi ila alijibu kwa ujumbe wa simu kuwa ofisi hiyo ya dc haina mamlaka ya kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake.

"Nimesafiri kikazi. Hamna haja ya kikao kwasababu kwa mujibu wa sheria ofisi ya Tarafa au ya mkuu wa wilaya haina nguvu ya maswala ya madai. Sehemu zenye nguvu za madai ni CMA, high Court na court of appeals kwa mujibu wa sheria ya section 86(1) of the employment and labour relations Act. 2004. Tulituma pia barua kueleza changamoto, malipo ya watu waliyopewa and sheria ikoje baada ya kushtukizwa na wito wa ghafla."Amesema Randy
1574326379656.jpeg
 
Mkurugenzi wa hizo hoteli naona anajielewa. Sasa ni wakati kwa wafanyakazi kujifunza au kufundishwa sheria za kazi.
Wanasiasa wanatafuta kiki kwenye matatizo ya watu. Huyo mkuu wa wilaya wakiandamana watumishi wa umma kwenye wilaya yake atawatuma field force unit kuwapiga na kisha FFU kupewa posho.
 
Huyu jamaa anachemka mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani katika eneo lake, sasa linapotokea suala la uvunjifu wa amani lazima ahusike. Kundi kubwa hivi liandamane alafu akae kimyaa? Nadhani kiburi cha pesa kinamsumbua huyu jamaa pamoja na kuwa katoa ajira kwa watu wengi hivi lakini ni mpuuzi.
 
Ahhh huyu Randy ni kiboko hatetemeshwi na yoyote, na lolote naona kama amekata tamaa fulani hivi...hii nchi ugumu wa maisha ni matokeo ya haya
 
Huyu jamaa anachemka mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani katika eneo lake, sasa linapotokea suala la uvunjifu wa amani lazima ahusike. Kundi kubwa hivi liandamane alafu akae kimyaa? Nadhani kiburi cha pesa kinamsumbua huyu jamaa pamoja na kuwa katoa ajira kwa watu wengi hivi lakini ni mpuuzi.
Kweli kabisa, kama kuna uvunjifu wa amani kamata hao waliondamana bila kibali na aliyeandaa hayo maandamano.
 
Hao wafanyakazi wakatafute kazi nyingine au watafute mashamba walime hapo kazi hakuna.Hoteli zenyewe zinaendeshwa kibishi wageni wachache wanategemea mishahara itatoka wapi?
 
Back
Top Bottom