Arusha: Rais Samia azindua kiwanda cha kisasa cha nyama

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Rais Samia Suluhu amezindua kiwanda kikubwa nchini cha kuchakata nyama cha Eliya Food Overseas Ltd, kilichopo wilayani Longido Mkoa Arusha chenye thamani ya Sh bilioni17 na kuahidi kumaliza changamoto ya Maji inayokikabili ifikapo desemba 5, mwaka huu .

Akiongea katika uzinduzi huo rais Samia amepongeza uwekezaji huo mkubwa nchini na kusema ni fursa Kwa wafugaji wa Wilaya ya Longido na Mkoa wa Arusha kuuza mifugo yao .

Rais Samia aliahidi kutatua changamoto zingine katika kiwanda hicho ,ikiwemo upatikanaji wa malighafi ya Nyama,Masoko ya Ngozi ,pamoja na kuwapatia elimu wananchi kuacha kuweka alama kwa kuchoma ngozi jambo linalopunguza thamani ya ngozi.

"Tumezichukua changamoto hizo ila suala la maji nataka pindi ifikapo desemba 5 mwaka huu yawe yanapatikana kiwandani hapo kwa uhakika viongozi wa mkoa na wilaya simamieni hilo " alisema

Rais Samia aliongeza kuwa kiwanda hicho kitakuwa kikisafirisha nyama nje ya nchi hivyo hivi sasa soko la mifugo ni la uhakika.

Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho, lrfhan Virjee alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata tani 20 za nyama ya ng'ombe sawa na Ng'ombe 500 kwa siku na tani 20 za nyama ya mbuzi na kondoo,Sawa na mbuzi 4000

"Kwa sasa kiwanda hiki kinafanya kazi kwa asilimia 30 ya uwezo wa kuchinja na kuchakata nyama kwa mifugo ya mbuzi na kondoo na asilimia 10 kwa mifugo ya ng'ombe"alisema

Virjee alimweleza rais kuwa lengo la kiwanda hicho ni kufikia uzalishaji wa asilimia 80 kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 na kukuza masoko mapya ya bidhaa zetu

Alisema mpaka sasa kiwanda kimeshatoa ajira 150 za moja kwa moja kwa Watanzania wakiwemo madaktari watatu wa wanyama kutoka serikalini wanaofanya kazi za ukaguzi wa afya na ubora wa mifugo hapo kiwandani.

Awali Waziri wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kiwanda hicho ndio kikubwa kwa sasa hapa nchini kati ya viwanda 10 vilivyopo nchini.

Virjee alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kuiomba serikali kusaidia upatikanaji wa ng'ombe wa bei nafuu kwa kuruhusiwa kununua mifugo kutoka moja kwa moja kwa wafugaji na hivyo kusaidia kuingia kwenye soko la ndani kwa bei nafuu.

Alisema kwa sasa wanauza Nyama katika masoko ya nchi za uarabuni ,Oman,Qatar,Kuweit,Bahrain ,Falme Za kiarabu(UAE) na Kenya.

Hata hivyo alimwomba Rais Samia kuharakisha mazungumzo na nchi ya China ili kufikia makubaliano ya ubora wa Nyama .

Aidha Virjee alimweleza Rais Samia Uwekezaji wa kiwanda Cha Maziwa Cha Kilimanjaro Dairy Milk LTD ,kilichopo Unga limited jijini Arusha ,ambapo alimwonyesha aina mbalimbali za maziwa wanazozalisha ambapo Rais Samia alifurahia bidhaa hizo muhimu Kwa jamii.

Kwa upande wake waziri wa viwanda Profesa Kitila Mkumbo alisema kiwanda hicho kwa Sasa ni kati ya viwanda vikubwa 618 vya kusindika Nyama hapa nchini na kwamba kiwanda hicho ni cha kwanza kwa ukubwa kati ya viwanda 10 vya kusindika Nyama nchini.

Ends.....

IMG_20211018_092916_396.jpg
IMG_20211018_090603_066.jpg
IMG_20211018_090645_731.jpg
IMG_20211018_090827_267.jpg
IMG_20211018_093108_371.jpg
 
Hao makada ni wana hisa kwenye kiwanda? Hongera zao sana. Itakuwa kwa mara ya kwanza wanaonyesha mfano wa kuanza kupanda ili kuvuna baadae
 
Hivi ndio viwanda vya kufungua, sio vile vya waziri yule aliyedai hata ukiwa na charehani moja ni kiwanda.

Tulichelewa sana soko la UARABUNI la Nyama. Yaani hawa wananunua nyama Danmarka wakati Longido ni kilomita chache tu toka UARABUNI.

Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipojaribu hilo alitupiwa mawe na wale ngangari wakidai eti UDINI, ahh tufike mahali tutenganishe udini na biashara. Vinginevyo hatuchomoki hata baada ya miaka 100 wacha hii 60 ya uhuru.

Kwa kasi hii, huyu mama mpaka anamaliza muda wake 2030 tutakuwa na viwanda mbali mbali vikubwa kama hivi zaidi ya 300. Ajira nje nje kwa wahitimu wa vyuo vikuu.
 
Naomba kuuliza. Hiki kiwanda kulianza kujengwa lini vile?
Sijui, lakini hata kama unamaanisha kuwa pengine kilianza kabla ya yeye kuwa Rais, bado kwangu inamaana kubwa sana kwake kukamilisha. Kwa maana kuna miradi mingi ilipigwa chini huko nyuma baada ya uongozi kubadilishwa, kama vile ujenzi wa nyumba National housing Magomeni ni kwingineko japo miradi hiyo ilifikia zaidi ya 50% ya utekelezaji wake. Sijagusa bandari ya Bagamoyo N.K
 
Wafanyabiashara wetu wengi wakubwa wabantu wamebakia kuwa wachuuzi tu (kufata bidhaa china na uturuki na kuja kuuza kariakoo) uthubutu wa kuanzisha viwanda wengi hawana
Na wakizileta bidhaa wanawapatia wamachinga. Akili ya wenye mtaji inaishia kuchuuza, akili ya nguvukazi ya vijana inaishia kuchuuza, wanasiasa wa vyama vyote wanatumia wamachinga kama mtaji.

Lakini kwa upande mwingine wabantu wakiwekeza wanafuatwa na wanasiasa ili waongezee cha juu, na cha juu akilipe mwananchi mwisho wa siku bidhaa inakosa ushindani wa bei biashara zinakufa ndani ya muda mfupi.
 
Africa roho mbaya sana. Hata hapo lazma Kuna wajuba wanapercent
 
Kwa hali ya Tanzania siamini kuwa kiwanda hicho kitadumu zaidi ya miaka 10 kutokana na sheria mbalimbali za kodi.
 
Hivi ndio viwanda vya kufungua, sio vile vya waziri yule aliyedai hata ukiwa na charehani moja ni kiwanda.

Tulichelewa sana soko la UARABUNI la Nyama. Yaani hawa wananunua nyama Danmarka wakati Longido ni kilomita chache tu toka UARABUNI.

Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipojaribu hilo alitupiwa mawe na wale ngangari wakidai eti UDINI, ahh tufike mahali tutenganishe udini na biashara. Vinginevyo hatuchomoki hata baada ya miaka 100 wacha hii 60 ya uhuru.

Kwa kasi hii, huyu mama mpaka anamaliza muda wake 2030 tutakuwa na viwanda mbali mbali vikubwa kama hivi zaidi ya 300. Ajira nje nje kwa wahitimu wa vyuo vikuu.
Rais Samia anahusikaje na ujenzi wa hiki kiwanda. Yani mtu kaitwa kuzindua alafu unamsifia yeye badala ya waliojenga kwa fedha zao. Kwani SSH asingezindua kingebomoka?

Isaya ameoa kwa gharama zake, kwenye harusi kamuita Ashura aje kula ubwabwa bure ila cha ajabu wanakwaya wametunga nyimbo za kumsifia na kumpongeza Ashura.
 
Huuu mfano haki nimecheka
 
Pole sana, nakosa maneno ya busara ya kuandika bila kuchafua lugha. Najitahidi kuandika sentensi moja tu itayokuamsha.

Waswahili wanasema ukimchukia mtu kwanza mpe Jina baya. ..... Ni hivi, Dhana ujenzi wa kiwanda hiki ilikuwepo toka wakati wa utawala wa Mwinyi (Kelele za watu zikamshtua Mwinyi na kuachana na ujenzi huo), na nchi hizi za uarabuni zimejaribu tena na tena wakati wa Mkapa, Kikwete lakini hawakuambulia kitu kwa sababu tawala hizo ziliwaogopa watu. Ninachotaka kukueleza ni kuwa katika uwezekanaji wa hilo mkono wa serikali ni asilimia 80, na muwekezaji kamalizia hayo ni asilimia 20. Kwa vile kwa muwekezaji yeyote yule wa uhakika anafahamu kuwa soko lipo wazi hivyo pesa yake inarudi mchana kweupe.

Na Miradi kama hiyo ipo lukuki ofisini- serikalini, lakini uoga wa serikali ndio tabu. Moja kati ya miradi iliyolala mikononi mwa serikali ni MRADI WA GESI - Pengine tuanzie hapo kama una hoja.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom